Rais Samia Suluhu kuzungumza na Wazee wa Dar es Salaam Ijumaa Mei 7, 2021

Napambana nami nizeekee Dar Es Salaam in shaa Allaah.
Kuna heshima kuwa Mzee wa Dar es Salaam.

Kuna anaebisha?
 
Mataga kutoka sukuma gang amepanic
 
wazee wabaki kuwa washauri raisi atafute jukwaa la vijana aongee na vijana namna ya kuchangamkia fursa hizi za wakenya
 
Hivi wazee wapo Dar Es Salaam TU? maana hatujawahi kusikia viongozi wa Juu wakitaka kuzungumza na wazee wa mikoani, au mikoani wapo vijana tu
 
Unalazimisha sana Lisu na Lema warudi Tz. vipi walikuahidi kukuoa?
 
Sawa. Wazee wa CCM kama kawa.
 
Mkuu, nami naona ni vyema hili suala la JIJI kuwa ni wilaya ya Ilala tu halina afya mzuri. Pamoja na Mh. Rais kutaka kurithi baadhi ya ambayo ya mtangulizi wake, lakini kwa hili naona aliangalie upya. Kama anapenda kuwe na JIJI na wilaya za Ilala, Kinondoni, Temeke ziendelee kuwepo, mimi kwa mtazamo wangu napendekeza kama ifuavyo:Eneo kuanzia Chuo cha U vuvi Kunduchi kufuata barabara hadi Mbuyuni (junction ya barabara ya Bagamoyo na Kunduchi Beach) unakuja hadi Lugalo, Chuo cha Ardhi, Chuo Kikuu Chuo cha Maji, Mabibo Hostel, Tabata Segerea, Airport, TAZARA, Veterinary, National Stadium (Mgulani), Chuo cha Uhasibu, hadi Daraja la Kikwete na Kigamboni. Eneo hilo linafaa kwa kuanza na JIJI LA DAR-ES-SALAAM. Nakaribisha maboresho.
 
Dikteta aliwadharau sn
tangu enzi za nyerere hadi kikwete, walikua na utaratibu wa kuzungumza nao wazee wa pwani hawa.
jiwe yeye hakujua aliwakumbatia wazee wa chato,akawasahau wazee wa pwani.

na nakuhakikishia akimaliza kuzungumza na wazee wa dar, mbio za mwenge zinafunguliwa upya.
 
Kazi kweli
 
Hakuna jipya hapo atakaloongea huyo mama SSH zaidi tu ya ahadi na porojo. Ifike mahali tuwe tunaona "utekelezaji" wa mambo kuliko "ngonjera" za kujirudia rudia.
Kwa kumbukumbu zangu kila Rais amekuwa akikaa na kuongea na wazee lakini sijaona changamoto zinazowakabili wazee zikitatuliwa hata robo tu bado.

Tanzania tuna safari ndefu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…