Rais Samia Suluhu kuzungumza na Wazee wa Dar es Salaam Ijumaa Mei 7, 2021

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271


Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa Mei 7, 2021 anatarajia kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mkutano utakaofanyika ukumbi wa Mlimani City na kuhusisha wazee takriban 900.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Mei 6, 2021 na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge aliyebainisha kuwa kulikuwa na utaratibu maalum wa kuwapata wazee hao na kwamba wengine wanapaswa kufuatilia mkutano huo kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

"Tunaomba sana waliopata mwaliko wahudhurie mkutano huu, Tunatarajia ikifika saa nane kamili wazee wote watakuwa wameshafika. Na utaratibu wa jinsi ya kufika utatolewa kwani kutakuwa na magari yameandaliwa.”

"Tunamshukuru Rais kwa kuchagua Mkoa huu kwa sababu angeenda Mkoa wowote lakini amechagua Dar es Salaam. Ninaamini kuongea na wazee hao atakuwa ameongea na wazee wa Tanzania nzima," amesema.

Wazee.jpg
 
Mama Samia usiache kuhoji Lisu na Lema wanarudi lini Tanzania.

Walituaminisha wamekimbia nchi na kwenda kulelewa na wanaume wa kizungu kama wakimbizi kwa sababu hapa nchini walikuwa wanatishiwa maisha na mwendazake.

Sasa hivi mwendazake hayupo je ni lini mtaacha kuishi kwa kulelewa na wazungu Ulaya mrudi Tanzania kujenga nchi na kula kwa jasho lenu? Tunahoji haya kwa sababu tunaona mko kimyaaa.

Mkiendelea kukaa kimya watu watajua mlikimbia nchi kwa masilahi yenu na siyo kwa kutishiwa maisha na mwendazake. Kwanza wewe Lema ulilipa lile deni lako la million 400 lililosomwa na spika Ndugai bungeni?

Rudi ulipe madeni ya watu.

Na wewe mzee wa MIGA Lisu rudi hutawakuta Acacia uliokuwa unawatetea sana utakuta kampuni mpya ya madini inayoitwa TWIGA
 
Back
Top Bottom