Rais Samia Suluhu kuzungumza na Wazee wa Dar es Salaam Ijumaa Mei 7, 2021

Wazee wanatumia kama platform tu ya kuongea na nchi si unajuwa wazee wa majungu wako Dar hawana kazi ila kunywa kahawa na fitna huku kwingine wazee wako busy na kilimo.
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa Mei 7, 2021 anatarajia kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mkutano utakaofanyika ukumbi wa Mlimani City na kuhusisha wazee takribani 900.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Mei 6, 2021 na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge aliyebainisha kuwa kulikuwa na utaratibu maalum wa kuwapata wazee hao na kwamba wengine wanapaswa kufuatilia mkutano huo kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

"Tunaomba sana waliopata mwaliko wahudhurie mkutano huu, Tunatarajia ikifika saa nane kamili wazee wote watakuwa wameshafika. Na utaratibu wa jinsi ya kufika utatolewa kwani kutakuwa na magari yameandaliwa.”

"Tunamshukuru Rais kwa kuchagua Mkoa huu kwa sababu angeenda Mkoa wowote lakini amechagua Dar es Salaam. Ninaamini kuongea na wazee hao atakuwa ameongea na wazee wa Tanzania nzima," amesema.

Chanzo: Mwananchi.
 
Haha naona style ya kuongea na wazee imerudi....ni jambo jema lakini kuongea na wazee

Ova
 
Hivi wazee si wapo kwenye risk age/group yakuteswa na Coronavirus?

Ni hatari sana kuwakusanya kipindi hiki.
 
Back
Top Bottom