Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,697
- 9,048
Mama yetu wa Taifa, mpendwa wetu nani kama Mama?
Umeanza vzr sana ktk siku zako 100 kwa kusimamia Haki, Sheria, Amani, Upendo na Mshikamano. Katika siku 100 tumehuhudia kesi za kubambikiwa zikifutwa, watu waliodhulumiwa wakirudishiwa haki zao, wapinzani wakijumuishwa kwene Serikali yako etc.
Kasoro imeanza kujitokeza juzi wakti CHADEMA na uongozi wake walipotangaza kufanya Kongamano la ndani kuhusu Katiba mpya!
Kitendo cha kuwakamata Viongozi Waandamizi wa CHADEMA huku Mwenyekiti Mhe. Freeman Aikael Mbowe akikamatwa na kurudishwa Dar @ KUJIBU KESI/TUHUMA ZA UGAIDI KUTAKA KUUA VIONGOZI WA KITAIFA ni DOA KUBWA KWA UTAWALA WAKO MAMA YANGU.
Nina shawishika kabisa haya siyo mawazo yako! Tatizo ninalo liona hapa ni MAHAFIDHINA WA CCM ambao wameanza KUKUPOTOSHA ili upoteze mwelekeo ili urudi kulekule kwa mtangulizi wako Hayati Magufuli. Mama siasa zinahitaji uvumilivu, upendo na mshikamano. Usije ukakubali Mahafidhina wa CCM waanze kukuyumbisha. Wengi wana hofu ya kupoteza maharaja!
Usikubali Mahafidhina waanze kukuyumbisha wakilitumia JESHI LA POLISI kukuchonganisha na Watanzania hasa Wapinzani. Haiwezekani Mhe. Mbowe akamatwe na RPC MWANZA kwa madai ya mkutano wa ndani @ usio na kibali!! Halafu Ghafla polisi wakabadilisha maelezo kuwa MHE. MBOWE AMERUDISHWA DAR ANAKODAIWA ALIPANGA MAUAJI YA VIONGOZI WA SERIKALI!! Huu uongo na utengenezaji wa matukio ili kuwanyamazisha Wapinzani utali gharimu Taifa.
Kwa sasa kuna hasira za Watz kuanza KUBAMBIKIWA UTITIRI WA KODI KWENYE MIAMALA YA SIMU NA MAFUTA YA MAGARI! Ulishatoa maelekezo kwa Mawaziri husika kuangalia kodi hizi. Lakini ujue kuna tabia ya Mawaziri Mahafidhina ndani ya CCM kubadilisha mtazamo/mwelekeo wa Watz ili waache kufuatilia mambo ya msingi yanayowagusa.
Hii ni aibu kubwa kwa Serikali inayotaka kuongoza nchi kwa MATUKIO YA KUBUMBA.
Wasaalamu.