Rais Samia Suluhu Hassan akutane na wakosoaji wote wa CCM na Serikali yake

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
7,567
9,026
Wandugu kwa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ameonyesha uungwana kwa kukubali kukutana na vyama vya upinzani kwa maslahi mapana ya nchi, tayari ameshakutana na wazee wa Dar es Salaam. Kwa uungwana huo aliouonyesha kujali makundi mbalimbali na kupata mawazo, kero, ushauri ninatabiri atafika mbali na kufanikiwa iwapo atakubali ushauri kutoka kwa Mtanzania yeyote yule na kutoka popote pale, ndani ya nchi au nje.

Kwakuwa ameahidi kuteua Mtanzania yeyote yule mwenye weledi bila kujali chama atakacho, mimi namshauri akutane na sisi wakosoaji wakubwa wa CCM na serikali tuliopo mtandaoni, kuanzia sisi tuliopo JF, Twitter, Instagram, Facebook ili apate michango, maoni, ushauri, mapendekezo na kero mbalimbali zilizopo nchini ili azifanyie kazi na kazi yake itakuwa nyepesi sana maana kwenye mitandao humu kuna watu wa aina tofauti tofauti wenye elimu na ujuzi tofauti.

Ushauri kwa kuwa zama za vitisho, utekaji zinaelekea kupotea au kuisha wawakilishi wote waliopo mitandaoni tuende ikulu tumevaa mask zilizoandikwa ID zetu kama utambulisho. Angalizo wanaoogopa kwenda hawalazimishwi wakae kushoto hii ni nchi yetu sote.

Jahazi litaongozwa na mimi Chief Kabikula, baadhi ya ajenda ni Katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, uchumi, ajira, demokrasia, utawala bora, uwekezaji, mahusiano ya kimataifa, Kuachiwa wafungwa wa kisiasa na watu wote waliopo jela au rumande kwa makosa yaliyotokana na uchaguzi mkuu na uchaguzi wa serikali za mitaa na mada nyingine mtakazopendekeza wakuu.
 
Ili iweje? Hao ni wachonganishi pia wasio na jema hata kidogo. Mimi ni megundua sio watu wema, walikuwa wanamsema Magufuli weee baada ya samia kuingia hata bado mwaka hujaisha washaanza mambo ya ajabu ajabu.
 
Ili iweje? Hao ni wachonganishi pia wasio na jema hata kidogo. Mimi ni megundua sio watu wema,walikuwa wanamsema magufuli weee baada ya samia kuingia hata bado mwaka hujaisha washaanza mambo ya ajabu ajabu
Utajuaje wachonganishi wakati hata hawajatoa hoja zao, hii nchi mawazo ya kuwa CCM pekee ndio watailetea maendeleo yameisha feli miaka sitini ya uhuru mawazo yao pekee yametumika tumefika wapi? Tumepata nini?
 
Wakosoaji wa serikali zote duniani huwa wana pointi za maana za kujenga, wakosoaji wa mtandaoni wapo na Wana hoja nzuri tu, constructive criticism, ndio maana mama anapitia Sana mitandao kujua kinasemwa, anyway mitandaoni Kuna watu wengi wenye taaluma tofauti tofauti hivyo Kuna mawazo mazuri tu kwa mtu mwelewa.
 
Kama kweli wakosoaji wa serikali na CCM mitandaoni wako serious basi wajitokeze watoe ya moyoni sio blablaa mtandaoni wakampe mdma madini live.
 
Wandugu kwa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ameonyesha uungwana kwa kukubali kukutana na vyama vya upinzani kwa maslahi mapana ya nchi, tayari ameshakutana na wazee wa Dar es Salaam. Kwa uungwana huo aliouonyesha kujali makundi mbalimbali na kupata mawazo, kero, ushauri ninatabiri atafika mbali na kufanikiwa iwapo atakubali ushauri kutoka kwa Mtanzania yeyote yule na kutoka popote pale, ndani ya nchi au nje.

Kwakuwa ameahidi kuteua Mtanzania yeyote yule mwenye weledi bila kujali chama atakacho, mimi namshauri akutane na sisi wakosoaji wakubwa wa CCM na serikali tuliopo mtandaoni, kuanzia sisi tuliopo JF, Twitter, Instagram, Facebook ili apate michango, maoni, ushauri, mapendekezo na kero mbalimbali zilizopo nchini ili azifanyie kazi na kazi yake itakuwa nyepesi sana maana kwenye mitandao humu kuna watu wa aina tofauti tofauti wenye elimu na ujuzi tofauti.

Ushauri kwa kuwa zama za vitisho, utekaji zinaelekea kupotea au kuisha wawakilishi wote waliopo mitandaoni tuende ikulu tumevaa mask zilizoandikwa ID zetu kama utambulisho. Angalizo wanaoogopa kwenda hawalazimishwi wakae kushoto hii ni nchi yetu sote.

Jahazi litaongozwa na mimi Chief Kabikula, baadhi ya ajenda ni Katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, uchumi, ajira, demokrasia, utawala bora, uwekezaji, mahusiano ya kimataifa, Kuachiwa wafungwa wa kisiasa na watu wote waliopo jela au rumande kwa makosa yaliyotokana na uchaguzi mkuu na uchaguzi wa serikali za mitaa na mada nyingine mtakazopendekeza wakuu.

Naunga mkono hoja, akiafiki hilo niko tayari kwenda. Ili uruhusiwe kuingia unalogin kwenye Id yako.
 
Wale wanaojiamini kujenga hoja na kuzitetea , fursa ndio hii sio muishie kukosoa mtandaoni tu , twendeni tukaonane na mama ana kwa ana mimi najua atakubali tu .
 
Back
Top Bottom