Rais Samia Suluhu azindua mtambo wa kisasa taasisi ya moyo Jakaya Kikwete. Asema Kazi ilifanyika Awamu ya Tano

Kuna kitu bado hakiingii akilini. Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete inasifika sana au inasifiwa sana na Serikali kuwa inao madaktari bingwa na vifaa vya kisasa.

Sasa ikawaje basi Magufuli akafa kwa tatizo la "moyo" tena akiwa hospitali ya Mzena?

Kwanini Magufuli alipopata matatizo ya moyo hakupelekwa hapa kwenye Taasisi hii ya Moyo Jakaya Kikwete yenye madaktari bingwa na vifaa vya kisasa??
 
Kuna kitu bado hakiingii akilini. Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete inasifika sana au inasifiwa sana na Serikali kuwa inao madaktari bingwa na vifaa vya kisasa.

Sasa ikawaje basi Magufuli akafa kwa tatizo la "moyo" tena akiwa hospitali ya Mzena ?

Kwanini Magufuli alipopata matatizo ya moyo hakupelekwa hapa kwenye Taasisi hii ya Moyo Jakaya Kikwete yenye madaktari bingwa na vifaa vya kisasa?????
Kuna tofauti ya Corona na ugonjwa wa moyo!
 
Usiwe mtumwa wa fedha au financial mercenary yaani kila jambo unalithaminisha kifedha tu. Thaminisha na mambo mengine kama kuokoa maisha, kurahisisha matibabu, kuongeza ajira, ujuzi na maarifa,kupunguza umaskini,utegemezi wa nje,kuitangaza nchi n.k.
Haya
 
Mambo yanaendelea huko tufuatilie kasi ni ile ile kazi iendelee.

========

Rais Samia Suluhu ameongoza shughuli za kuzindua Mitambo na kwa sasa zoezi linaloendelea salamu za watu mbali mbali. Alianza Professa Janabi ambae ametambulisha watu wote anaofanya nao kazi kila siku. Dkt. Janabi ametambulisha madaktari Bingwa wa Moyo nchini na kuelezea 'succession plan' kwenye taasisi yao endapo yeye ataondoka ama baadhi ya watu katika taasisi hiyo.

Baada ya Dkt. Janabi alifata Mkuu wa Mkoa wa Dar, Amos Makalla ambae ameongea kwa mara ya kwanza leo mbele ya Rais tangu kuteuliwa. Amos Makalla amemshukuru Rais Samia kumteua kuwa mkuu wa Mkoa wa Dar na kusema kwake ni nyumbani sehemu aliyozaliwa na kukulia. Makalla ameahidi kuendelea kukomesha Ujambazi Dar es Salaam.

Kisha akafata mkuu wa bodi ya Taasisi ya Jakaya Kikwete na kuelezea ndoto zake za kutibu magonjwa ya Moyo nchini na wengine kumkejeli mpaka ndoto zake kuwa kweli. Mwenyekiti ameelezea ndoto yake ya kuweza kuwa na watu mikoani watakaokuwa na uwezo wa kutibu magonjwa ya Moyo.

Anaongea Rais Samia na anasema kazi anayozindua leo ilifanyika awamu ya Tano na kumpongeza Hayati Rais Magufuli. Rais Samia amesema ameona uchawi unaofanyika ndani ya taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete. Amesema Tanzania inajisifu kwa kupunguza vifo vya watoto.

Rais Samia amesema eneo la Jakaya Kikwete limesaidia kupunguza vifo vya watoto. Amesema wagonjwa 5959 wamepata matibabu na watu 11 pekee wamefariki baada ya Upasuaji ikiwa ni asilimia 0.2 pekee. Ameongeza kusema mitambo pekee haitoshi kwani inaongozwa na watu na kuitumia ipasavyo.

Anasema ukisikia kusimamishwa moyo unakufa kabla haujasimamishwa lakini ndani ya taasisi ya Jakaya Kikwete unasimamishwa mpaka masaa sita.

Ameeleza kuzibeba changamoto zao na wanaenda kuzifanyia kazi.

Rais Samia amesema mcheza kwao hutuzwa na serikali itaangalia Maslahi yao.

Rais Samia Suluhu amewaahidi Bilioni mbili kutoka Serikalini kama walivyoomba kwa ajili ya kujenga jengo jipya, wao Taasisi ya moyo watatoa bilioni 2 kukamilisha bilioni 4 kwa ajili ya ujenzi huo



Waungwana wanajua kuchagua maneno kwa hekima. Sifa huwapa wenzao. Ila wale wengine sasa - "yaani wameniachia kila kitu hewa; nchi ilikuwa imechezewa sana; yaani hata mwenda wazimu hawezi kusaini mkataba huu!"

Hiiiiii bagosha!

Ama kweli akili za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Waungwana wanajua kuchagua maneno kwa hekima. Sifa huwapa wenzao. Ila wale wengine sasa - "yaani wameniachia kila kitu hewa; nchi ilikuwa imechezewa sana; yaani hata mwenda wazimu hawezi kusaini mkataba huu!"

Hiiiiii bagosha!

Ama kweli akili za kuambiwa changamoto na za kwako.
Kwhyo wew unataka useme mtangulizi wake hajaacha kibubu kinono?
JK aliiacha nchi inanuka rushwa hazina hamna, sasa ulitaka uungwana kusema yasiyo kuwepo?
Overall jamaa hakuwa politician, alikuwa kiongozi na hakuwa mnafiki kama Akina Nchemba, Gambo. Mhongo, hakusita kusema ukweli penye ukweli
Eti uungwana, Nyie ndio mmekaliwa vchwani hadi Leo na mkoloni,
Siasa zenu za kutafta kujipendekeza kumsifia kiongozi ni zaidi ya umalaya,
Samia hawezi kubeza kazi ya boss wake ili hali inaonekana kwa Umma, asbiri afanye yake
 
Kwhyo wew unataka useme mtangulizi wake hajaacha kibubu kinono?
JK aliiacha nchi inanuka rushwa hazina hamna, sasa ulitaka uungwana kusema yasiyo kuwepo...
Sukuma Genge na lahaja za kiswahili wapi na wapi?

Kajifunzeni kiswahili mjue japo communication skills!
 
Mwinyi alizindua ya Nyerere, Mkapa akazindua ya Mwinyi, Kikwete akazindua ya Mkapa na marehemu Magufuli akazindua ya Kikwete hiyvo si ajabu Samia nae kufungua ya Magufuli wote wanatekeleza ilani moja ya chama cha mapinduzi kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania!
Mmeanza kusema ukweli? Wakati Mwendazake anazindua miradi iliyoanzishwa na JK mlimpamba yeye binafsi mkiamaanisha kaianzisha yeye! Hata alipoazindua iliyowahi kuzinduliwa na Mtangulizi wake bado mlipisha shangwe za sifa. Leo mmeachiwa toka kifungo cha fikra mnatueleza mapya?
 
Back
Top Bottom