Rais Samia rejesha hadhi ya Ukuu wa Wilaya

Niwie radhi mkuu, kama umeguswa na Uzi huu, sikumlenga MTU Bali ni ushauri kwa maslahi mapana ya nchi na hatma ya uongozi wa Tanzania.
Wala hujanilenga. Shida umezunguka..! Ungesema Fulani bin Fulani aliharibu au la.
 
Tunataka cheo cha DC kifutwe kibaki cha DAS
Tunataka DC awe na sifa zifuatazo
1. Elimu kuanzia digrii.
2. Mtanzania
3. Umri kuanzia miaka 30
4. Hana rekodi ya makosa.


Mtu akitimiza hayo awe na sifa zifuatazo:

1. Awe mwajiriwa wa serikali au shirika binafsi au chama cha siasa na kutumikia Taasisi yake angalau miaka 5

2. Kama ni kiongozi wa chama (asiye mwajiriwa) awe amehudumu kwa vipindi viwili na hana skendo ya rushwa, ubaguzi na ulevi.

3. Wastaafu wa utumishi wa umma na binafsi hata wakiwa na f6 wateuliwe
 
U-DC ni cheo kikubwa na chenye heshima kwani ndiye mwakilishi wa Rais kwenye eneo husika.

Ndani ya miongo miwili iliyopita tulianza kushuhudia wakiteuliwa watu wa ajabu ajabu na ndiyo maana sasa tunashudia matukio ya ajabu ambayo hayajawahi kushuhudiwa tangu nchi yetu ipate Uhuru.

Hili limesababiswa na teuzi bila kuzingatia haiba na heshima ya cheo hicho kwa vigezo vya mipango-kando, slay queens, play boys nepotism nk na kufanya cheo hicho nyeti sana kupoteza heshima yake.

Enzi za akina Jakaya Mrisho Kikwete, Jenerali Ulimwengu na wengineo wakiwa wakuu wa wilaya, U-DC ulikuwa ni U-DC kweli kweli.

Ushauri wangu ingawa siyo nia yangu kuwamharibia MTU yeyote, niombe miongoni mwa vigezo vya uteuzi wa nafasi hyo, basi ndoa iwe ni kigezo muhimu sana kabla ya uteuzi.

Kuna mtu aliwahi kukosa nafasi kwenye kampuni fulani kubwa pamoja na kuwa na qualification zote, akakosa kwa sababu ya ndoa.

Nawasalimia kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Kazi iendeleee.
Hoja inahitaji maboresho. DC ni mtawala, yaani adminsitrator. Kazi ya utawala inahusisha stadi zifuatazo:
  • planning
  • organising,
  • motivating,
  • communicating,
  • monitoring,
  • evaluating,
  • controlling
  • etc
Stadi hizi hupatikana lini, wapi na kwa vipi?

Ualimu wa somo, ualimu wa darasa, ualimu wa bweni, uhariri wa chumba cha habari, ukuu wa idara, udaktari, uparoko, uaskofu, uanandoa, hutoa stadi hizi kwa wahusika.

Kwa hiyo, sio sahihi kuinua uanandoa dhidi ya uzoefu baki.

Pili, kuna wajane, wagane, mahanithi, watalikiwa, na watu kama hao, wenye sifa za kuwa watawala.

Kwa hiyo, ndoa sio kigezo huru kwa ajili ya kuteua watawala.

Hizi ndio sababu sheria zetu hazilazimishi watu kufunga ndoa.

kwa hiyo, siungi mkono hoja.

Nadhani hoja hii inaanzia katika itikadi ya genitalism.
 
Wako wapi waheshimiwa hawa?

MHE. CAPT. S.A. MPEMBNWE

MHE. S. SIWALE

MHE. COL.L. MAKUNENGE
 
Back
Top Bottom