Chakwale
JF-Expert Member
- May 17, 2015
- 1,068
- 1,542
Katika pesa zilizotolewa na Rais Samia ktk miradi mbalimbali Nchini ikiwemo ya Elimu, Afya, Miundombinu nk kupitia IMF naunga mkono zaidi mradi wa Uchimbaji Visima.
Kuna pesa imetengwa kwa ajili ya ununuzi wa gari za Uchimbaji Visima ila idadi yake iliyotolewa ni ndogo ukilinganisha na mahitaji na umuhimu wake.
Maji ni tatizo kubwa sana Nchini mwetu hususani maeneo ya Vijijini na hata mijini pia. Adha, kero na usumbufu wake ni mkubwa kwa akina mama mana wao ndio wenye jukumu la utafutaji wa maji.
Mh. Rais Samia ww ni Mama, Rais na Mwanamke kama ambavyo unapenda kujitanabaisha,unajua kero tabu shida na masumbufu wanayopata kina Mama ktk utafutaji wa maji.
Kero hizi huhitaji kusimuliwa wala kuelezwa sababu Nina imani unazijua vyema mana umeziishi kabla hujafika huko uliko Leo.
Ila binadamu tumeumbwa na sahau nina kukumbusha tu Mh. Rais kulivalia njuga hili suala la maji nchini kama lilivyovaliwa njuga suala na kuondoa machinga maeneo yasiyo rasmi.
Ushauri Wangu,haya magari ya Uchimbaji Visima yaongezwe walau kila Wilaya Nchini yawepo magari matatu ambayo yatakuwa yanachimba Visima kwa bei Nafuu itakayokuwa Elekezi ila kila mwenye uwezo achimbe.
Visima vikiwa vingi hata wale wasio na uwezo wa kuchimbiwa majumbani mwao watanunua kwa wale waliochimba hivyo tatizo la maji kuwa historia. Uzuri wa haya magari hata kama yatamaliza kazi ya Uchimbaji yanaweza badilishiwa matumizi na kuendelea kufanya kazi nyingine za Umma.
Mh. Rais tunaweza kununua ndege, kujenga Reli Mpya ya kisasa SGR ambazo zinagharimu pesa nyingi mnoo lakini kama sisi wananchi wenu tunahangaika na mambo madogo madogo kama upatikanaji maji safi na Salama ni tatizo, hata hayo mnayoyafanya yanakuwa hayana maana saana sababu hizo ndege hazitusaidii.
Nina matumaini yangu ujumbe huu utakufikia Mh Rais na utaufanyia kazi, ni mm kijana Mzalendo.