Rais Samia: Nitasimama na wananchi

Rais Samia: Nitasimama na wananchi

Mitaani huku maisha hayashikiki ajira hakuna sijui atasimama na wananchi wawapi.
 
Wananchi gani? Au hawa aliowabebesha zigo la kuiendesha serikali yake huku yeye akila maisha bila kujali.
Hatumhitaji!!! Hatumhitaji mwanasiasa yeyote. Tunasimama wenyewe kwa umoja wetu Kama watanzania waliotelekezwa na serikali yao.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuna makundi ndani ya serikali ambayo wanafanya wanayoyajua na kulaumu kuwa ufisadi umerudi awamu ya sita wakati wao ndio wako hovyo

Amesema mambo ya hovyo hayajafanyika hawamu ya sita yamefanyika huko nyuma na gari bovu wanaliangushia awamu ya sita, jambo ambalo hatokubali
Kwani wakati ufisadi unafanyika yeye alikuwa katika tawala za mbele?,ameshindwa kuelewa kwa baadhi ya tawala alizoziita za nyuma ilikuwa ni marufuku kusema ufisadi unaofanyika ukithubutu adhabu yake ilikuwa ni risasi ukihurumiwa unatumbuliwa?.
 
Nenda kalikumbatie kaburi huko Chato, acha kumsumbua Raisi wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan
Kama nakuona vile unavyotoka mapovu....Rais ni watanzania wewe nani kudhani unamiliki?
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuna makundi ndani ya serikali ambayo wanafanya wanayoyajua na kulaumu kuwa ufisadi umerudi awamu ya sita wakati wao ndio wako hovyo

Amesema mambo ya hovyo hayajafanyika hawamu ya sita yamefanyika huko nyuma na gari bovu wanaliangushia awamu ya sita, jambo ambalo hatokubali

Rais amesema hatakubali jambo hilo kwa kuwa ameapa kusimamia za wananchi na atasimama na wananchi
Anasimama na Wananchi gani???

Anasimama na Wananchi hawa hawa ambao awamu ya Sita wamewaongezea Tozo???. Wakiuliza wanaambiwa wahamie Burundi.

Wananchi hawa hawa ambai ktk awamu ya Sita gharama ya bidhaa zote zimepanda Bei na raisi amekaa amekaa kimya.

Atuambie anasimama na Wananchi gani.
 
Mh. Rais Samia, wakati akikemea wanaotaka kuipaka matope Serikali yake, alisema, "sitakubali, nitasimama na wananchi".

Mimi nakubaliana sana na kauli hii, mashaka yangu ni namna ya kuiishi.

Ikumbukwe kwamba, Rais Samia wakati anaingia madarakani, nchi ilikuwa kwenye kiu na njaa kali ya haki, njaa na kiu kali ya demokrasia na uhuru wa watu. Ni kipindi ambacho kulikuwa na kundi kubwa la watu waliokuwepo mahabusu za polisi kwa kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi, utakatishaji fedha haramu, ugaidi, uchochezi na uuzaji wa madawa ya kulevya. Ni kipindi ambacho shughuli za kisiasa zilikuwa zimezuiwa, isipokuwa kwa CCM pekee.

Ni kipindi ambacho, kutokana na mateso na njama mbalimbali dhidi ya yeyote anayeonesha kuikosoa Serikali au Rais, maisha yake yalikuwa kwenye mashaka makubwa. Ni kipindi ambacho watu kupotea, kutekwa, kuteswa na hata kuuawa, halikuonekana ni jambo la ajabu. Ni kipindi ambacho uhuru wa fikra ulikuwa umewekwa komeo la chuma isipokuwa kwa wale wanaoweza kuishi kwa unafiki wa kumsifia Rais kwa kila jambo.

Ni kipindi ambacho kwa mara ya kwanza, Waziri aliwahi kumtaja Rais kama Mungu, RC alitamka kuwa Mungu anatakiwa kumshukuru Rais, na Waziri Mwingine alisema wazi kuwa Rais ni kaka Yesu Kristo Masihi. Hiki ndicho Rais Samia anakabidhuwa madaraka ya Urais akiwa mwanamama wa kwanza kushika nafasi hiyo.

Rais Samia ameingia kwenye madaraka, huku ile infrastructure iliyotengeneza na kupalilia uovu mbalimba ikiwa ipo vile vile. Nina imani kubwa ni infrastructure hii ndiyo iliyomwingiza chaka Rais Samia, mpaka kufikia kutamka kuwa Mbowe ni gaidi. Ni infrastructure hii ndiyo inayoendelea na kesi za kubambikia watu, ushahidi wa kutengeneza, kuwa na majaji ambao maamuzi yao ni ya kuleta mashaka makubwa.

Rais Samia, alipoanza kufanya mabadiliko mbalimbali, alishangilia, alisifiwa na kukubalika na watu wengi wa makundi mbalimbali bila ya kujali vyama vyao vya kisiasa, dini zao, makabila yao au maeneo watokayo.

Uungwaji wake mkono, bila hata ya takwimu, kwa uwazi kabisa, uliporomoka ghafla baada ya kuonekana kuwa ameungana au ameagiza Mbowe kubambikiwa kesi. Jambo hili liliwaudhi sana wapenda haki wote na watu wanaoheshimu nafsi zao, bila ya kujali watu hao ni wafuasi wa vyama vya upinzani au CCM au hawana chama, na kwa upande mwingine, ndiyo jambo lililoleta mashaka makubwa kwa mataifa ya nje, kama kweli Rais Samia ana dhamira ya dhati ya kutaka kujrnga Tanzania ya haki.

Kama Rais Samia anataka kusimama na wananchi, basi ni lazima asimame katika haki, asimame kwenye misingi ya demokrasia na uhuru wa maoni wa watu na vyombo vya habari. Maana katika hayo, Watanzania wote wenye dhamira njema na nchi yao. Lazima Rais Samia, usimame kwenye upande unaoeleweka, ama usimame na watu wa haki au na waovu, hakuna neutral position kwenye hili. Lazima uamue unataka usifiwe na ukubaliwe na waovu au watu wema.

Rais Samia utambue kuwa waovu ni wachache sana, japo sauti zao zinaweza kuwa na uwezo wa kusikika sana kwa sababu ya nguvu walizokuwa nazo kwenye mfumo wa uovu. Ukisimama na wananchi, tena kwa haki na kwa dhamira njema, hakuna wa kukutisha, kubabaisha wala kukupa hofu. Ondokana na magofu ya maadui wa kurithi, yatakuangukia usipate wa kukuchomoa.

Mungu akujalie hekima ya kuangalia zaidi kesho na keshokutwa kuliko kuangalia tu leo.
 
Hadi sasa bado najiuliza sipati jibu, hivi yeye han akili mpaka ashindwe kujua hili ni sahihi au sio sahihi?
 
Back
Top Bottom