Rais Samia, ni sawa kutaka tuanze upya lakini lazima tuwe na pa kuanzia

Chadema wakati inapigania hoja ya ufisadi ilikua on fire leo hii wapo kupiginia madudu yasioeleweka eti tuzo za BET na kuonyesha mavazi kila jumamosi na kutunisha mfuko wa mwenyekiti kwa kadi za kikoba aibu yao!

Mada hii ni kubwa na ya kufikirisha kuliko huu utoto ulioandika hapa. Ni vyema shule zifunguliwe mapema urudi shule kuliko kuingiza utoto kwenye mada za wakubwa.
 
Anza kuomba msamaha wewe kwanza humu kwenye jukwaa la mficho kisha nenda hadharani ufanye hivyo hivyo ili kutia nguvu hoja yako bila hivyo hizo ni siasa tu ambazo zinashamiri kwa kuendekeza unafiki, uzandiki na majungu

Hii mada imebeba ukweli unaoumiza, na kwakuwa dhamira yako inakusuta, namna pekee ni kuupindisha ili wangalau makali ya ukweli huu yapungue. Hakuna mjadala kuwa Magu alikuwa kiongozi muovu, na aliachwa atakeleze uovu wake kutokana na katiba mbovu. Tunamshukuru Mungu kwa kuamua kumuondoa dunia maana imesababisha nchi hii kutokuendelea kumwaga damu
 
Pia utaratibu wa toba lazima utaje makosa yako yote hata uliyofanya gizani.
 
Magufuli alikuwa ni rais muuaji na hilo halina ubishi, kuna watu hadi leo haijulikani waliko na hakutaka kabisa mtu aongelee kutoweka kwao.

Thank God for his timely and a well deserved intervention to end the life of the ruthless butcher.
 
Malezi bora utoa familia bora familia bora utoa viongozi bora, watawala wa kiafrica ni zao la ukosefu wa malezi bora kwenye familia.
Mtoto aliyezoea kupigwa viboko ndio atii huyu lazima atakuwa dikteta akipewa leseni ya kuongozea watu.
 
Waliokomalia sheria ya kutoza faini ya shs 30,000 kwa bodaboda bado wamo bungeni, hao hao wanashangilia faini kushushwa; utadhani wakati ule ubongo ulikuwa umefunikwa kwa kitambaa, sasa umefunuliwa Tazama na hii
Ili uishi bungeni ni lzm uendane na mdundo
 
Chadema wakati inapigania hoja ya ufisadi ilikua on fire leo hii wapo kupiginia madudu yasioeleweka eti tuzo za BET na kuonyesha mavazi kila jumamosi na kutunisha mfuko wa mwenyekiti kwa kadi za kikoba aibu yao!
Hiki ulichoandika kinahusiana vipi na Mada iliyopo?
 
Kuna kitu kikubwa sana kwenye mamlaka na utakijua tu ukisha kuwa nayo. Ni utamu ambao ukionja kuachia ni kazi kubwa sana yataka moyo na neema ya Mungu.
Zao rahisi la mamlaka ni kiburi na dhulma. Wanaotambua hili hutawala kwa haki!
 
Shinda kubwa katika taifa letu ni unafiki na watu kuwa wazalendo kwa viongozi na sio taifa haya mambo yataendelea Mpaka siku wananchi watambue haki zao
 
well
 
uku ndiyo nini? Hata kiswahili kinawashinda, shuleni mlikwenda kujifunzia upumbavu nini? Neno ni huku
iko kiswahili chako tangu ukijue kwa ufasaha kimekusaidia nini??! zaidi ya ufakiri unaokuandama"
 
Hivi huwa hamna la maana kufanya?
Kujua ni lipi la maana na lipi siyo la maana inahitaji angalao kiwango fulani cha chini cha ufahamu. Kama hujakifikia, unaweza kuona kila ambacho watu wanajadili hakina maana, ila wakiongelea ubwabwa, biriani, hapo utaona wameongea cha maana, kwa sababu hata aliyepungukiwa akili, angalao anajua lazima ale.
 
Anza kuomba msamaha wewe kwanza humu kwenye jukwaa la mficho kisha nenda hadharani ufanye hivyo hivyo ili kutia nguvu hoja yako bila hivyo hizo ni siasa tu ambazo zinashamiri kwa kuendekeza unafiki, uzandiki na majungu
Ungewaacha kwanza wenye uelewa wajadili.
 
Km hukushangilia wewe wengine walishangilia...dunia hii ina mambo ndugu yangu..it is what it is...kwahio songa mbele..kesho unaeza chomwa chanjo ukapotea vilevile, who cares...utakuwa sio wa kwanza kufa...at the end of the day we will all die...
Hakuna asiyejua kuwa kifo kipo na ndiyo mwisho wa maisha ya kila mwanadamu aishiye hapa Duniani. Suala siyo kuishi au kufa, cha muhimu uliishi vipi ukiwa hai, uliwasaidiaje Dunia na Taifa lako kuwa mahali pema pa kuishi wanadamu wa leo na kesho? Ulikuja kuitengeneza au kuiharibu Dunia? Kama huwezi kuiboresha Dunia, kama huwezi kuchangia ustawi wa wanadamu na Dunia kwa ujumla, ni aheri usingelizaliwa.

Mwanadamu mwenye hekima, kwa muda mfupi aliopewa kuishi Duniani, hujenga kumbukumbu yake ya kukumbukwa kwa mema, na siyo kwa kuteka, kuua na kutesa wanadamu wenzake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…