Maneno Meier
JF-Expert Member
- May 12, 2013
- 2,469
- 1,697
Niende moja kwa moja kwenye mada yangu ya leo ninayotaka kuizungumzia.
Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wetu, nakuomba chonde chonde kuuangalia upya mradi wa BRT unao endelea kujengwa jijini Dar es salaam. Kwa uzoefu mkubwa nilio nao na analysis yangu ndogo niliyo ifanya naona kuwa huu mradi hautakuwa na impact yoyote kubwa kwenye maisha ya wakazi wa jiji la Dar es salaam katika;
1. Kumpunguza tatizo la usafiri jijini
2. Kutoa ajira nyingi kwa vijana
3. Kuleta transformation yoyote ile ya kiteknolojia ambayo itawawezesha vijana kupanua bongo zao na
4. Uharibifu wa mazingira kwa nishati inayotokana na matumizi ya mafuta mengi ya diesel
Mama nafikiri umeshatembelea nchi nyingi za ulimwengu na kuona miji yake yenye wakazi wengi. Kwenye hizo nchi nafikiri umeona pia jinsi gani wenzetu walivyo jitahidi kuondoa tatizo la usafiri wa abiria wanao kwenda kazini asubuhi na kurudi majumbani kwao baada ya kazi. Sambamba na usafiri wa mabasi ya public, commuter trains au niseme under ground na street trains au trams zimetamalaki sana.
Sisemi tujenge underground trains ila tu ningependa kusisitiza kuwa sambamba na mabasi ya mwendo kasi, commuter trains nazo zingepewa kipau mbele kikubwa katika kukabiliana na tatizo la usafiri wa abiria katika mji unao kua kwa kasi sana kama Dar es salaam. Mabasi ya mwendo kasi peke yake kwa jiji letu sitegemei kama yatakidhi mahitaji yanayo takiwa huko mbeleni.
Ni jambo ambalo sote tunajua kuwa Tanzania na hasa mji wa Dar es salaam unakabiliwa na uhaba mkubwa sana wa ajira kwa vijana wetu wanao maliza shulr na vyuo. Na serikali naona haina mbinu kubwa ya kutatua tatizo hili mbali na kutegemea wawekezaji wa sekta binafsi kutoka nje na ambao sio wengi wanaomiminika nchini.
Nafikiri tumeshuhudia wenyewe jinsi treni ya umeme ilivyopokelewa kwa miyo mkubjufu na watanzania na kusisitiza kumalizika kwa SGR ili watanzania waone matokeo yake.
Commuter trains na karakana zake zitasaidia kupunguza uhaba wa ajira kwa vijana na vile vile ni chachu ya vijana kuweza kupanua uwezo wao wa kufikiri kuhusina na teknolojia hii mpya kwao.
Connections kati ya miji kama Bagamoyo , Kibaha, Mkuranga na Kisarawe na Station yetu ya Tanzanite na Magufuli Bus Terminal, ingekuwa ni rahisi sana. Lakini kwa vile tuna waziri wa ujenzi na watu wa mipango miji ambao hawana vision, inakuwa shida sana kwa nchi kama Tanzania kupiga hatua kubwa na za haraka kiteknolojia.
Nashindwa kuelewa Mama Samia mipango ya serikali ya kusafirisha abiria jijini pindi SGR yetu ya Mwanza, Kigoma na nchi jirani itakapo kuwa imemalizika. Mji utakuwa haupitiki kwa foleni za magari na msongamano wa watu watakao pata nafasi ya kuja Dar haraka kufanya biashara kutoka mikoani na nchi jirani.
Jiji halina budi kujipanga sasa jinsi ya kukabiliana na changamoto la baadae. Tuna watu wa aina gani Mama ambao hata ile fikra ya kutambua nini matokeo ya baadae?
Mama sisi tunakutegemea wewe sana, kwani tunaimani ya kuwa una ile spirit ya kipenzi chetu Hayati Rais Magufuli. Haya mambo usipoyafanya wewe sidhani kama kuna mwingine atakaye kuwa na spirit yako na Hayati Rais Magufuli.
Swala jingine kubwa linalo tufanya tujenge usafiri wa commuter trains kwa haraka ni uharibifu wa mazingira. Kwa vile usafiri wa mabasi unachochea sana kwenye uharibifu wa mazingira kwa nishati inayotumia ya diesel haina budi kutafuta njia mbadala wa kuondokana na tatizo la uchafuzi wa hali ya hewa jijini.
Hivi haya mabasi yetu ya mwendo kasi yana partickel Filter na catalylizer ili kupunguza air polution?