Waziri2025
Senior Member
- Sep 2, 2019
- 148
- 379
Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Arusha kupitia kitengo kidogo Cha Malalamiko kinachosimamiwa na katibu tawala wilayani hapo,kimegeuka mahakama kwa kutoa maamuzi ya ovyo yaliyojaa Rushwa huku Haki ikipindishwa kwa maslahi yao.
Hatua hiyo imekuja kutokana na migogoro kadhaa inayoletwa katika dawati hilo la malalamiko chini ya katibu tawala wa wilaya hiyo(Das),Hanan Bafagih ambaye amekuwa alitoa maamuzi ya ovyo yenye maslahi yake bila kuzingatia kwamba Kuna nafasi nyingine iwapo mlalamikaji/ mlalamikiwa hakuridhika.
Hivi karibuni katibu tawala huyo ,Hanan Bafagih mwenye asili ya kiarabu aliamuru kubomolewa kwa banda lililojengwa katika eneo la mgogoro baada ya kusikiliza mgogoro wa ndugu baina ya Joseph Elisha na Mama yake mzazi Endesh Elisha.
Mama Endesh alikuwa akimlalamikia mwanaye (Joseph) kuvamia eneo lake. Hata hivyo Joseph katika utetezi wake alidai kwamba suala hilo lilishasikikizwa na wazee wa ukoo(Boma)pamoja a Baraza la kata ambao waliamua Banda hilo la ng'ombe wa kisasa lisibomolewe baada ya kujiridhisha kwamba eneo hilo marehemu alimkabidhi Joseph Kama Mtoto wa mwisho wa kiume kwa ajili ya kumtunza mama yake.
Pamoja na utetezi huo DAS hakuzingatia hata wosia wa marehemu unaoelekeza kwamba eneo hilo alikabidhiwa Mtoto wa mwisho ambaye ni Joseph, badala yake alitoa uamuzi wa kumwondoa kwa kubomoa Banda la Ng'ombe na kumtambua Mama yake (Endesh) kuwa ni mmiliki halali.
Pamoja na hayo hoja ya Msingi hapa mamlaka ya ofisi ya DAS kwenda kubomoa makazi ya mtu inatoka wapi ,nijuavyo Mimi mahakama pekee ndio yenye mamlaka ya kutoa maamuzi kama hayo tena kwa kuzingatia order ya mahakama.
Huu ni uonevu na matumizi mabaya ya ofisi yake lazima Das atambue mipaka yake kitengo cha Malalamiko hakina mamlaka ya kubomoa makazi ya mtu.
Tunaomba Rais Samia Suluhu aangalie utendaji wa ofisi ya DAS Arusha inanuka Rushwa na ikiwezekana amwondoshe Arusha, maana serikali ya leo sio ya Jana.
View attachment 1835613