Rais Samia muondoe DAS wa Arusha

Rais Samia muondoe DAS wa Arusha

Kama huyo ni mama mzazi, umemkosea sana, haikupaswa hata kuwe kuna usuluhishi, muheshimu mama ndugu, umebahatika kuwa nae.
 
Nilikuwa Arusha juzi kutolea ushahid wa Jambo fulan mahakamani

Kiikwel katika kesi zilizosikilizwa pale mahakaman 80% n za ugomvi wa ardhi inaonekana Kuna shida Sana ya ardhi Arusha
 
Wewe mleta mada acha majungu. Wewe ungekuwa ndio hiyo DAS unatatua mgogoro wa ardhi wa mtu na mama yake ungefanyaje? Kwanza huyo mtoto angekuwa na busara, kama ardhi aliachiwa na baba ili amuhudumie mama na mama hataki, angenuachia mama hiyo ardhi halafu akatafute ishu nyingine.

Kitendo tu cha kupelekana serikalini mama na mtoto kwa ardhi ya baba, kisha mtoto anakomaa ni aibu kwa mtoto. Hata mimi ningekuwa ndio muamuzi hapo, ningesimama zaidi upande wa mama kuliko mtoto.

Kwa hiyo mtoto anataka akasimame mahakamani na mama yake kuhusu ardhi ya baba? Dah!
Mkuu siyo majungu, mkoa wa Arusha kwa kurithisha boma wanaongoza, ndiyo maana vijana hawana stress na maisha, kijana akipata 2000 anarizika, that's why unaona watafutaji wengi ni kinamama.

Vijana ni goigoi sana, although watu wasiowafahamu wanaona ni wapiganaji NOTHING, wengi wanapewa ka..eneo hapo hapo kwao anajenga getto lake maisha mujarabu no stress !.
 
Pole sana bwana Josefu. Mimi tangu nilipokuwa mdogo sikutaka kabisa kusikia kitu kinachoitwa urithi! Haya ndiyo matatizo yake. Migogoro huwa haiishi.

Bora nitafute cha kwangu. Ila siyo cha urithi.
Kama GENTAMYCINE nikisema nitegemee ( nisubirie ) Urithi wa Nyumba ya Mzazi nina uhakika akinikabidhi na sehemu ilipo Bei ya Chini nikiamua Kuiuza basi ni ama Tsn Millioni 900 na mpaka Tsh Bilioni 2 ( kutokana na Eneo ilipo ) na Upyatu ( Umasikini ) wangu huu mkubwa nilionao sasa utakuwa ni Historia.

Ila nakumbuka mwaka 2003 GENTAMYCINE nikiwa nazungumza na Mzazi wangu nilimwambia kuwa Asante pekee ambayo nampa ni Kunizaa, Kunilea vyema, Kunisomesha vizuri na Kunirithisha Akili zake nyingi na Kubwa ila sitaki na sihitaji anirithshe Nyumba yake Kubwa ila akinirithisha tu Vitabu vyake anavyopenda Kusoma ili viniongezee Maarifa zaidi Kichwani nitamshukuru mno.

Nilipomwambia hivyo nae akaniuliza kwanini nimeamua hivyo nikamjibu kuwa Yeye alipambana hadi kuwa Mtu mkubwa nchini Serikalni hasa Awamu za Nyerere, Mwinyi na Mkapa na Maendeleo aliyonayo hivyo na Mimi Mwanae nataka nipambane Mwenyewe hadi nije Kufanikiwa hata kama nikifanikiwa nikiwa na Miaka 50 naelekea Uzeeni na hakuishia tu Kunielewa bali pia alinipongeza sana.

Na hivi ninavyoandkka hii post si kwamba labda GENTAMYCINE nina Maisha mazuri bali nina Changamoto nyingi tu za Kimaisha ambazo kama nikitska Msaada wa 'Kutoboa' Kimaisha kwa Msaada wa Mzazi wangu basi Maisha yangu leo hii hii yanabadilika na kuwa mazuri ila sitaki, sijakata tamaa baxo na naendelea Kupambana nikiamini Kauli ya Kiimani ( Sisi Wakristo ) isemayo Mungu huwa hawahi wala hachelewi.

Na nakumbuka baadae nikapigilia Msumari wa mwisho Kwake Mzazi wangu kuwa akiona anakaribia Kufa basi Mali zake zote aseme ( aandike ) kuwa akifa ziuzwe na Pesa itakayopatikana ipelekwe Kusaidia Watoto Yatima, Wazee ( hasa Wajane ) na Wagojwa Wakubwa ziwasaidie Kimatibabu.

Hakuna Kitu naogopa kama Mali za Urithi na nimeshona Watoto wengi wa Wakubwa ( VIP's ) Tanzania ambao waliachiwa Mali za Urithi na Wazazi wao na leo hii zote zimepukutika na Maisha yao ni Magumu 'maradufu' yangu GENTAMYCINE huku wengine sasa wakiwa ni Mashoga, Wabwia Unga na Majambazi pia.

95% ya Watoto ( Watu ) ambao Wanarithishwa Mali na Wazazi wao huziharibu na huishia Kugombana, kuwa na Migogoro, Kurogana na hata Kuuana huku 24/7 wakishinda Mahakamani kwa Kesi za Mirathi na ni 5% Wakirithishwa Mali na Wazazi wao ndiyo hufanya Maendeleo ya maana na nina Mifano 'very Vivid' juu ya hili ( haya ) niyaandikayo hapa.

Najua Siku moja nami nitakuwa Mtu TZ.
 
Mtoto anajitafutia mkosi, huwezi kugombana na Mama aliyekutunza tumboni mwake na akakuzaa.

Huyu chalii kama anaweza kumvimbia Mama mzazi inaonekana kwake kumharibu mtu ni kitendo cha sekunde tano tu.

Haya masuala ya kutoheshimu wazazi ndio yamewatia nuksi vijana wengi wa mikoa ya kanda ya ziwa, unakutana na mtu sehemu unaongea nae kwa hali ya kawaida tu lakini unauhisi unyama fulani wa ndani ya nafsi yake kumbe damu ya bibi aliyeuwawa kikatili inaendelea kumtesa.
Huko kanda ya ziwa ni tatizo, ndio kulitupatia rais aliyepita hivi karibuni na kutufanyia unyama wa hatari. Kumbe hata ww haya matatizo unayaelewa, nadhani sasa umeungana na sisi kwenye kile kilio chetu kuwa tuliongozwa na mtu mnyama toka kanda ya Ziwa.
 
Huko kanda ya ziwa ni tatizo, ndio kulitupatia rais aliyepita hivi karibuni na kutufanyia unyama wa hatari. Kumbe hata ww haya matatizo unayaelewa, nadhani sasa umeungana na sisi kwenye kile kilio chetu kuwa tuliongozwa na mtu mnyama toka kanda ya Ziwa.
Nyerere alitufundisha kupendana na upendo siku zote huvumilia na hauangalii upungufu wa mtu.

Kanda ya ziwa kuwa na ukatili kwa wazee hakuzifanyi kanda nyinginezo kuwa na binadamu wenye kufanana na malaika, kanda nyingine pia zina watu wenye upungufu mwingi tu.

Tanzania kuweza kufikisha miaka 60 ya uhuru ni kwa sababu waanzilishi wa taifa hili walitufundisha maana ya upendo kwa vitendo.

JPM ni Rais imara sana ukiona anachukiwa ujue dozi iliwaingia hao wanaomchukia.
 
Huyo Joseph Hana adabu anagombanaje na mamake kisa ardhi na Arusha maugomvi ya ardhi huwa ni mengi Sana na kukomoana.
 
Nilikuwa Arusha juzi kutolea ushahid wa Jambo fulan mahakamani

Kiikwel katika kesi zilizosikilizwa pale mahakaman 80% n za ugomvi wa ardhi inaonekana Kuna shida Sana ya ardhi Arusha
Arusha Wana ujinga wa ardhi Sana wanajibana sehemu Moja Hadi ndugu wamegombana,nchi hii yetu yenyewe mapori makubwa why wabanane sehemu Moja. Nchi hii sehemu watu wanapata shida ni Arusha na hii inachangiwa na ushamba flani ulioko.
 
Nimesoma
Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Arusha kupitia kitengo kidogo Cha Malalamiko kinachosimamiwa na katibu tawala wilayani hapo,kimegeuka mahakama kwa kutoa maamuzi ya ovyo yaliyojaa Rushwa huku Haki ikipindishwa kwa maslahi yao.

Hatua hiyo imekuja kutokana na migogoro kadhaa inayoletwa katika dawati hilo la malalamiko chini ya katibu tawala wa wilaya hiyo(Das),Hanan Bafagih ambaye amekuwa alitoa maamuzi ya ovyo yenye maslahi yake bila kuzingatia kwamba Kuna nafasi nyingine iwapo mlalamikaji/ mlalamikiwa hakuridhika.

Hivi karibuni katibu tawala huyo ,Hanan Bafagih mwenye asili ya kiarabu aliamuru kubomolewa kwa banda lililojengwa katika eneo la mgogoro baada ya kusikiliza mgogoro wa ndugu baina ya Joseph Elisha na Mama yake mzazi Endesh Elisha.

Mama Endesh alikuwa akimlalamikia mwanaye (Joseph) kuvamia eneo lake. Hata hivyo Joseph katika utetezi wake alidai kwamba suala hilo lilishasikikizwa na wazee wa ukoo(Boma)pamoja a Baraza la kata ambao waliamua Banda hilo la ng'ombe wa kisasa lisibomolewe baada ya kujiridhisha kwamba eneo hilo marehemu alimkabidhi Joseph Kama Mtoto wa mwisho wa kiume kwa ajili ya kumtunza mama yake.

Pamoja na utetezi huo DAS hakuzingatia hata wosia wa marehemu unaoelekeza kwamba eneo hilo alikabidhiwa Mtoto wa mwisho ambaye ni Joseph, badala yake alitoa uamuzi wa kumwondoa kwa kubomoa Banda la Ng'ombe na kumtambua Mama yake (Endesh) kuwa ni mmiliki halali.

Pamoja na hayo hoja ya Msingi hapa mamlaka ya ofisi ya DAS kwenda kubomoa makazi ya mtu inatoka wapi ,nijuavyo Mimi mahakama pekee ndio yenye mamlaka ya kutoa maamuzi kama hayo tena kwa kuzingatia order ya mahakama.

Huu ni uonevu na matumizi mabaya ya ofisi yake lazima Das atambue mipaka yake kitengo cha Malalamiko hakina mamlaka ya kubomoa makazi ya mtu.

Tunaomba Rais Samia Suluhu aangalie utendaji wa ofisi ya DAS Arusha inanuka Rushwa na ikiwezekana amwondoshe Arusha, maana serikali ya leo sio ya Jana.

View attachment 1835559View attachment 1835561View attachment 1835562
View attachment 1835613
Ni nini kauli ya mkuu wa wilaya ya Arusha? Amri ya kubomoa huwa inatakiwa kutolewa wapi na nani? Baada ya amri hiyo kutolewa ni akina nani wanapewa mamlaka ya kubomoa? Je huwa kunatolewa notice ya kubomoa ?
 
Nyerere alitufundisha kupendana na upendo siku zote huvumilia na hauangalii upungufu wa mtu.

Kanda ya ziwa kuwa na ukatili kwa wazee hakuzifanyi kanda nyinginezo kuwa na binadamu wenye kufanana na malaika, kanda nyingine pia zina watu wenye upungufu mwingi tu.

Tanzania kuweza kufikisha miaka 60 ya uhuru ni kwa sababu waanzilishi wa taifa hili walitufundisha maana ya upendo kwa vitendo.

JPM ni Rais imara sana ukiona anachukiwa ujue dozi iliwaingia hao wanaomchukia.
Alikuwa dhalimu fullstop.
 
Back
Top Bottom