Rais Samia kushuhudia Utiaji Saini wa Mkataba wa Bilioni 400 za Kujenga Skimu za Umwagiliaji hekta 95,000

Una mtaji? Utaweza kumudu usimamizi?

Siyo mnapiga pamba mjini halafu mnawaachia vibarua halafu wanatelekeza kazi.

Vijana wengi hampendi kukaa shamabani.
Kulima sijaanza leo, suala la usimamizi sio lazima kila wakati niwe shambani, majirani wa mashamba yangu ni rafiki zangu na ni wasimamizi wangu pia, muhimu niwape vocha kila wakihitaji, mambo mengine wanamaliza wenyewe hata nikiwa mjini.
 
Hizo mabilioni za hela zinakupotea sioni matunda bora yakitokea kama hakuna mfumo wezeshi wa utaratibu wa hizo hela.
Unless otherwise wahandliwe ma expert walio wekeza kwenye kilimo then wapewe Ruzuku lakini unawapa viwana na wamama wenye njaa, ili wawekeze kwenye irrigation systems ni ngumu sana
 
Hapo kwenye wamama sasa, wamama hao ni wale ambao hupewa mikopo isiyorejesheka ya pesa za halmashauri wanazotengewa wake wa viongozi wa CCM.
Hiyo skimu iko mkoa gani na ni kilimo cha mazao gani? Kama itakuwa chini ya JKT au magereza tutegemee kitaleta faida ila kama ni ya kugawana viongozi wa CCM hakitakuwa na faida.
Ingekuwa hivyo wangeacha kupewa..Hizo pesa walijipa viongozi wa Halmashauri Kwa kuchongesha majina ya wanawake kumbe ni wao..

Kama ukisikia juzi Kati kule Mwanza ,zote zilirudi.
 
Hizo mabilioni za hela zinakupotea sioni matunda bora yakitokea kama hakuna mfumo wezeshi wa utaratibu wa hizo hela.
Unless otherwise wahandliwe ma expert walio wekeza kwenye kilimo then wapewe Ruzuku lakini unawapa viwana na wamama wenye njaa, ili wawekeze kwenye irrigation systems ni ngumu sana
Utaratibu gani na hizo ni miradi ya umwagiliaji inaenda kujengwa..

Zitarejeshwa taratibu na watumiaji wa hizo skimu.
 
Vijana Changamkieni fursa , Serikali imeamua.kuwashika mikono 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220804-092800.png
    Screenshot_20220804-092800.png
    225.5 KB · Views: 5
  • Screenshot_20220804-092328.png
    Screenshot_20220804-092328.png
    52 KB · Views: 5
  • Screenshot_20220804-092357.png
    Screenshot_20220804-092357.png
    47.2 KB · Views: 5
J
Nawasalimu kwa jina la JMT..

Taarifa mpya ni kwamba Siku Rais wa JMT mh.Samia S.Hassan atashuhudia utiaji Saini wa Mkataba wa Ujenzi wa skimu ya umwagiliaji yenye ukubwa wa hekta 95,000 wenye thamani ya TSH.Bil.400.

Tukio hilo litafanyika siku ya kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane 8/8/2022.Hii ni Katika kutekeleza Ajenda 10/30 ya Mapinduzi ya Kilimo Cha Biashara.👇

View attachment 2312599
Jambo jema
 
4 August 2022

Waziri Aweso: Vyanzo Vya Maji Havilindwi Kwa Kukaa Ofisini na Kompyuta, Utakuwa Hautoshi

 
08 August 2022
Mbeya, Tanzania



More info :

08 August 2022

Rais, Samia Suluhu Hassan akizindua mradi wa maji Mbalizi mkoani Mbeya.

1659971512120.png



Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza kuwa, “Wizara ya Kilimo inatakiwa kuhakikisha inashiriki kikamilifu katika kuwasajili wakulima ambao watapatiwa ruzuku, na kuwataka wahusika kuhakikisha wanajisajili kwani baadaye vitatolewa vitambulisho vitakavyowasaidia kupata huduma.”

Akizungumzia miradi ya Kilimo, Rais Samia Hassan ameungana na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwa kusema miradi mingi ya kilimo inatakiwa iwanufaishe wakulima katika maeneo husika, na kuwataka maafisa ugani kuwa makini na matumizi ya rasilimali na vitendea kazi vya Serikali walivyopatiwa ili kuwahudumia wakulima.


Wakulima waaswa kuzingatia kilimo chenye tija​

5 hours ago
1659971812733.png




Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amewataka Wakulima nchini kuendelea kufuata maelekezo ya wataalamu wa Kilimo, ili kuweza kupata mazao yenye tija wakati wa mafuno ambayo yatawanufaisha kiuchumi na kuliingizia Taifa kipato.
Bashe ameyasema hayo hii leo Agosti 8, 2022 katika kilele cha cha maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane), ambayo yanafanyika katika uwanja wa John Mwakangale Mkoani Mbeya na kusema ulimaji wa mazao bila kuzingatia maelekezo ya wataalamu ni kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
Amesema, sambamba na hatua hiyo pia wakulima wanatakiwa kuwa makini na ununuaji wa mbolea zilizothibitishwa na kuanishwa na Serikali, ili kuweza kurutubisha ardhi na hivyo kujiwekea uhakika wa mavuno ya kutosha kwa chakula na biashara.

“Ni lazima kuzingatia maeloekezo ya wataalamu wa Kilimo, hii itasaidia kupata mavuno yenye tija, lakini pia tuzingatie ulimaji wa mbolea ambao utasaidia kutupatia wakulima mazao ya chakula na biashara na tuzingatie viuatilifu vilivyoainishwa na Serikali,” amesema Bashe.
Amesema, msimamo uliopo ni kubadili mifumo ya ununuzi pembejeo za kilimo za ruzuku baada ya Serikali kuja na mpango wa ujenzi wa viwanda vya mbolea nchini na kusema ni vyema kuweka umoja baina ya wakulima kwa kubadilishana taariza zinazolenga kuwasaidia kufikia malengo
 
Back
Top Bottom