Rais Samia kushuhudia Utiaji Saini wa Mkataba wa Bilioni 400 za Kujenga Skimu za Umwagiliaji hekta 95,000

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,589
14,135
Nawasalimu kwa jina la JMT..

Taarifa mpya ni kwamba Siku Rais wa JMT mh.Samia S.Hassan atashuhudia utiaji Saini wa Mkataba wa Ujenzi wa skimu ya umwagiliaji yenye ukubwa wa hekta 95,000 wenye thamani ya TSH.Bil.400.

Tukio hilo litafanyika siku ya kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane 8/8/2022.Hii ni Katika kutekeleza Ajenda 10/30 ya Mapinduzi ya Kilimo Cha Biashara.👇

Screenshot_20220802-205444.png
 
Attachments

  • Screenshot_20220804-092517.png
    Screenshot_20220804-092517.png
    50.3 KB · Views: 4
Hizo skimu kama pangefanyika utaratibu iangaliwe namna bora ya kuwapa vijana/wanawake kwa kuwakodishia kwa masharti nafuu, zingekuwa na maana sana kwenye kuwainua kiuchumi.

Lakini sio mwisho wa siku matajiri wakiwemo wanasiasa waende huko kujimilikisha mamia ya hekari, halafu vijana wasio na ajira wageuzwe manamba, zitakuwa hazina maana wala hazitapunguza tatizo la umaskini.
 
Na walengwa ni Vijana haswaa na Wamama kama ulivyosema maana ni waaminifu.
 
Lengo la serikali ni kufikia Hekta 1,200,000 za umwagiliaji mwaka 2025.... source : Habari | NIRC - Tume ya Taifa ya Umwagiliaji

More : toka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
13 July 2022

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji yatangaza Ukombozi Kwa wakulima mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe na sasa Mbeya yanufaika na miradi mikubwa

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa, ameongoza kikao kazi cha mapitio ya mpango mkakati wa miaka mitano wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji. Uliohusisha wataalam na wahandisi wa Umwagiliaji nchini, mapema leo Jijini Dodoma

Miradi mikubwa 13 mkoa wa Mbeya itafunguliwa katikati ya mwezi agosti 2022.

Bilioni 216 shilingi za kiTanzania kutumika mkoani Mbeya kugharamia ya miradi hiyo itakayokuwa maeneo kama Mbarali, Kyela, Busekelo, Mbadibira, Mbuyuni n.k

Mikoa hiyo minne ya Katavi, Rukwa, Songwe na Mbeya inatazamia kufuta kabisa upungufu wa chakula nchini kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji na kuligeuza eneo hilo la nyanda za kusini magharibi kuwa kapu tegemezi la chakula kwa nchi (breadbasket) kulisha nchi na ziada kuuzwa nje ya nchi.
 
Hizo skimu kama pangefanyika utaratibu iangaliwe namna bora ya kuwapa vijana/wanawake kwa kuwakodishia kwa masharti nafuu, zingekuwa na maana sana kwenye kuwainua kiuchumi.

Lakini sio mwisho wa siku matajiri wakiwemo wanasiasa waende huko kujimilikisha mamia ya hekari, halafu vijana wasio na ajira wageuzwe manamba, zitakuwa hazina maana wala hazitapunguza tatizo la umaskini.
Una mtaji? Utaweza kumudu usimamizi?

Siyo mnapiga pamba mjini halafu mnawaachia vibarua halafu wanatelekeza kazi.

Vijana wengi hampendi kukaa shamabani.
 
Tukitaka kuinua Kilimo seriously,ni lazima 10-15% ya bajeti ya nchi iende kwenye Kilimo.Kilimo siyo Irrigation schemes tu,kuna mbegu bora,mbolea,viuatilifu, miundombinu ya barabara vijijini, Research and Development, huduma za ugani,Agro machineries nk.Sasa hiyo Bajeti ya sasa inakidhi mahitaji?
1/3 ya chakula Duniani inazalishwa na wakulima wadogo,Sasa hizo schemes wakipewa wakulima wadogo,niiteni fisi!
Tutaishia kubadili slogan na mipango hewa,mara siasa ni Kilimo, Kilimo uti wa mgongo,Kilimo kwanza na wasa 10/30.
 
Wafanye kila wilaya itapendeza.
Yaani nawaza hii kitu inashindikana nini sipati majibu. Uimara na legacy ya mama Samia ipo hapa bila chenga.......vijana wangejiajiri na tungenunua nyanza mpaka 100; afya na vicheko vingerejea!
 
Kila Wilaya tena? Unaangalia sehemu productive zenye mabonde na maji ya kutosha ambazo hazitatumia gharama kubwa
Kwani aiwezekani? Tunaweza sana kila wilaya nchini kuwa na bwawa na irrigation system sema bongo zimelala tu kwa mfano pesa za yale mandege ya Magufuli yasiyo na tija yangeweza kuchimba mabwawa au kutengeneza hizo system nchi nzima, na hapo tungeweza kupunguza ajira kwa vijana.
 
Tukitaka kuinua Kilimo seriously,ni lazima 10-15% ya bajeti ya nchi iende kwenye Kilimo.Kilimo siyo Irrigation schemes tu,kuna mbegu bora,mbolea,viuatilifu, miundombinu ya barabara vijijini, Research and Development, huduma za ugani,Agro machineries nk.Sasa hiyo Bajeti ya sasa inakidhi mahitaji?
1/3 ya chakula Duniani inazalishwa na wakulima wadogo,Sasa hizo schemes wakipewa wakulima wadogo,niiteni fisi!
Tutaishia kubadili slogan na mipango hewa,mara siasa ni Kilimo, Kilimo uti wa mgongo,Kilimo kwanza na wasa 10/30.
Kwa Bashe na Mama naona kuna mwanga wa kimatendo kabisaaa
 
Tukitaka kuinua Kilimo seriously,ni lazima 10-15% ya bajeti ya nchi iende kwenye Kilimo.Kilimo siyo Irrigation schemes tu,kuna mbegu bora,mbolea,viuatilifu, miundombinu ya barabara vijijini, Research and Development, huduma za ugani,Agro machineries nk.Sasa hiyo Bajeti ya sasa inakidhi mahitaji?
1/3 ya chakula Duniani inazalishwa na wakulima wadogo,Sasa hizo schemes wakipewa wakulima wadogo,niiteni fisi!
Tutaishia kubadili slogan na mipango hewa,mara siasa ni Kilimo, Kilimo uti wa mgongo,Kilimo kwanza na wasa 10/30.
Serikali haiwezi kufanya kwa tija kilimo cha umwagiliaji badala yake, iweke mazingira mazuri na kuwaleta wakulima kabambe toka SA na wale waliofukuzwa Zimbabwe waje wafanye mambo yao, na wala sio kuweka siasa tu kila siku kwenye kilimo...
 
Na walengwa ni Vijana haswaa na Wamama kama ulivyosema maana ni waaminifu.
Hapo kwenye wamama sasa, wamama hao ni wale ambao hupewa mikopo isiyorejesheka ya pesa za halmashauri wanazotengewa wake wa viongozi wa CCM.
Hiyo skimu iko mkoa gani na ni kilimo cha mazao gani? Kama itakuwa chini ya JKT au magereza tutegemee kitaleta faida ila kama ni ya kugawana viongozi wa CCM hakitakuwa na faida.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom