Rais Samia Kumbuka Fao la Kujitoa

Wakulima nao wameanza kuingizwa ktk mfumo wa hifadhi ya jamii,
Tembelea ofisini utapata maelezo zaidi
Ili nao waingie kwenye mfumo wa kupigwa?
Kama let's say una wanachama 1000 wanalalamikia huduma mbovu,i.e hujawatoshereza kuhuduma,
na hao ni wafanyakazi,ambao kwa maneno yako umewaita mbumbumbu,je wakiingia wakulima
ambao most of them ni small scale farmers hao si ndo mtawapiga na kitu chenye ncha kali kichwani?

Ni vyema mboleshe huduma zenu kisha muongeze wateja,vinginevyo tutajua mnaongeza wigo wa upigaji.
 
KUONDOKEWA MAFAO YA KUJITOA NI KWA MANUFAA YA WANACHAMA

Nimesoma yote yaliyoandikwa na wadau na kugundua kwamba wote hawafahamu DHANA YA HIFADHI YA JAMII. Kwa sisi tuliopiya IFM, ninvyema tukatoa elimu kidogo kwa ndani gu zetu ambao hawaelewi vizuri jambo hili. Kwa taarifa, dhana msingi ya Hifadhi ya Jamii ni:-

“Kumfanya mtu kuweka akiba kidogokidogo wakati ana uwezo wa kutengeneza mapato ili akiba hiyo imfae wakati atakapokuwa hana uwezo wa kuzalisha mapato”.

Kwa NSSF, Sheria inamtaka Mwanachama kuchangia 10% tu ya mshahara wake; na Sheria hiyo hiyo inamlazimisha Mwajiri kuchangia 10% ya ziada kukamilisha akiba ya Mwanachama huyo. Kwa maana nyingine, Mwanachama asingepata hiyo 10% ya Mwajiri bila ya Sheria hii.

Akiba hii inapaswa kuendelea kujaziwa kwa kipindi chote cha Mwanachama akiwa na uwezo wa kufanya kazi. Wakati mtu anapochangia 10% ya mshahara wake, anabaki na 90% ya mapato yake. Kudundiliza huku kutaendelea kwa kutumia waajiri mbalimbali atakaofanya nao kazi katika maisha yake.

Kama ni mjasiriamali mzuri, atatumia kiasi kingine kidogo kutoka 90% ili kudunduliza mtaki kwa muda fulani na kuanza biashara. Kama atashindwa kufanya hivyo hadi siku anakosa ajira ndiyo aanze kupambania 10% aliyokuwa anaweka ili aanzisjie biashara, huyo siyo mjasiriamali. Na uwezekano mkubwa ni kwamba hata akizipata hazitamfikisha mbali na itambidi atafute kazi tena ya kuajiriwa.

Sasa wakati akifikia utu uzima na uwezo wa kuchakarika kufanya kazi haupo, ndiyo sasa ataanza kupata pensheni ya kila mwezi hadi mauti yatakapomchukua. Kama aliwahi kuanzisha biashara na ikafanikiwa, maisha yake ya uzeeni yatakuwa mazuri. Kama hakuwahi kuanzisha biashara, basi atakuwa na uhakika wa kupata mahitaji yake muhimu.

Fursa za kuanzisha biashara ziko nyingi tu kwa wajasiriamali waziri. Tukumbuke Bilionea Reginald Mengi alianzisha IPP wakati yeye ni mwajiriwa wa PWC mpaka pale kampuni yake ya IPP ilipokuwa kubwa sana ndipo akaacha kazi. Unaweza ukachangia SACCOS au ikaweka fedha zako Benki na baadae ukachukua mkopo kuanzisha biashara. Kama haya yote huyawezi, kuwa na uhakika hata akiba yako ya NSSF ya 10% haitakusaidia kitu.

Kila mfumo umeanzishwa kwa makusudi yake na taratibu husika lazima zifuatwe. Kama kwa bahati mbaya makusudi haya hatyajui vizuri tuepuke kufanya kosa na kuongea bila elimu na kuanza kuwatukana watu matusi wasiyostahili.
Kumbe mifuko ndio yenye kuamua ni lini mtu apewe chake.

Sasa tushauri ifanyike hivi....kila mwajiriwa akatwe 10% na mwajiri naye achangie 10% then hiyo pesa iwekwe kwenye akaunti ya akiba ambayo hawezi chukua hadi atakapoacha, achishwa, fariki au kustaafu kazi.

Benki waruhusiwe kuzizungusha kwa interest rate ndogo ambayo itatunisha fao la mwajiriwa...tuone kiburi kitatoka wapi na kupelekesha wastaafu kutatoka wapi!!
 
Hivi wakiofuta FAO la kujitoa si ni serikali ya awamu ya 4!? Na majority ya mawaziri wake ndio wapo kwenye stearing by now....!
 
KUNA MTU MMOJA PALE UBUNGO PLAZA ANAITWA ALLY MTOLEA ANAZUIA FEDHA ZANGU WAZI WAZI ILA KITAKACHOMPATA ATAJADILIANA NA MUNGU WAKE. MWAKA WA PILI HUU KAZIKALIA PASI SABABU.
Fanya mambo braza, fanya fasta washen*i kama hao wanaong'ania pesa za watu ni wa kukandamiza chini kabisa hadi wany*
 
Hoja yangu mnapokuwa mnapokea michango ya mhusika mbona hamuulizi usahihi wa majina? Na je ninyi hamna kitengo cha elimu kupita kwenye maofisi yanayoleta michango ili kuondoa tatizo hilo mapema?
Tunaojua,tunaelewa kwamba mnanufaika na umbumbumbu wetu ndo maana hamtoi elimu
Lakini kumbuka yana mwisho ndugu.Kabla hujaajiriwa hiyo nafasi alikalia mtu,jiulize yuko wapi hadi anakuachia unakalia wewe?
Hilo liwe funzo kwako kwamba kuna siku na wewe utaondoka watakaa wengine,na utaenda mtaani kukutana na uliowafanyia ufedhuri.

Siku ya kutoa pesa ndo umbumbu unaonekana?
Haya kuna mtu kalalamikia mnavyodai rushwa wazi wazi kwenye uzi mwingine,unamwambia aweke ushahidi hivi wewe ndo mfanyakazi pekee wa nssf kujibu hoja zate? kuanzia za malipo hadi za rushwa?
Ndugu nakushahuri badilika,unayowafanyia wenzio usipolipwa wewe uwe na uhakika yatawakuta wanao.

Unataka kuniambia na huyu aliyelalamika kuwa mnadai rushwa naye amekosea majina?
na kama amekosea majina ,akitoa rushwa,rushwa inarekebisha vipi jina ili liwe sahihi alipwe stahiki zake?

Niwashauri wafanyakazi wote wanaochangia mifuko hii,muwe na tabia ya kutembelea mifuko hii, ombeni
statement zenu,usisubiri siku ya kustaafu,fuatilia mapema ukutane na nyodo ukiwa bado una nguvu za kukimbizana nao
na kuchukua hatua mapema ili ujue na mahali pa kutoa taarifa unapofanyiwa ndivyo sivyo.
Statement unapata hata 5 minutes haziishi,kimbembe unapoanza kufuatilia hasa fao la kujitoa NSSF hawapendi.NSSF Ni Kama vile unaenda Ukraine trust me
 
Kwa hakika Mh Rais tunamuomba kulitazama hili.

Kijana anapoteza kazi pengine akiwa na miaka 35 lakini analazimishwa asubiri mpaka atakapofikisha miaka 55 ndio apate mafao yake ambayo pengine ni milioni 15.

Fedha hii anveipata mapema ingekuwa rabisi kijana kufungua biashara yake angali na nguvu na pengine akamuajiri mtu mwingine mmoja.

Lakini pia kijana ambaye amefanya kazi kwa muda na kuamua kuacha na kutumia mafao yake kufungua biashara itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wengine kwa kuwa kuna mtu ataajirjwa kuziba nafasi ya yule aliyeacha kazi,na pia aliyeacha kazi na kwenda kufungua biashara akimuajiri kijana mwingine mmoja atakuwa amepunguza namba ya wasio na ajira mtaani.

Kwa kufanya hivyo mapato ya serikali yataongezeka maana idadi ya walipa kodi itakuwa imeongezeka.Na maisha ya watu yataboreka.
 
Shinyangakwetu!

Wewe matako kweli hujui kitu chochote fao la kujitoa lipo na wafanyakazi wengi tuu walioachishwa kazi ndani ya miezi sita wanapata fao la kukosa ajira na ikifika miezi 18 mingine yaani baada ya kukamilisha jumla ya miezi 24 unapewa fao la kujitoa.

Acha kuwa mpumbafu na kupotosha watu kenge wewe@
Labda wewe ndo unapotosha. Mimi nimekaa zaidi ya miaka miwili na wameshupalia nitimize miaka 55 ndo nipewe. Kifupi, hilo fao halipo au linatolewa kimchongo.
 
Ni ujinga sana,unaacha kazi au kuachishwa kazi,huko NSSF una pesa zako ulizochangia kwa miaka kadhaa,ukiwaambia wakupe zote hawataki eti wanakupigia mahesabu wakupe kidogokidogo kwa miezi sita eti ukipata Ajira utaendelea kuchangia,nani aliyewaambia anataka kuendelea kuajiriwa??kati ya vitu vya kipumbavu nchi hii ni pamoja na suala hilo,halafu hao wafanyakazi wa NSSF wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wao Maka Mshomba wana viburi utadhani watashika hizo nafasi mpaka kaburini
 
Back
Top Bottom