Rais Samia kumbe unalijua hilo?

Rais Samia kumbe unalijua hilo?

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
23,349
Reaction score
28,510
Rais Samia: "Ukiwa public figure usipoonekana lazima watu wajiulize"

Kwa kulijua hilo ulikuwepo ulazima ws sisi wananchi kujulishwa alipo mtumishi wetu ambaye hayupo kwenye nafasi hiyo kwa ajili yenu.

Tatizo linakuja mnapotuona sisi wananchi ni watu wadogo sana hatulazimiki kujua kiongozi alipo!

Makamu wa Rais anayo ofisi hivyo kuna wananchi huhitaji awahudumie yeye binafsi kutokana na mamlaka yake.

Kisa hiki cha kutoweka kimyakimya kwa Makamu wa Rais kinatokana na kutokutumika kwa katiba.

Nchi inaendeshwa bila katiba kila kiongozi anafanya atakavyo akiamini hakuna wakumfanya kitu isipokuwa rais tu!

Mheshimiwa Rais ikikupendeza tujulisheni alikokwenda Makamu wa Rais.
 
Watanzania sio wajibikaji kiasi hicho, ni kutaka kupata taarifa za kuwafurahisha, za kifo kama kawaida kwa masikini, mbona wengi hajui hata wa bunge wao na hawahoji wako wapi
 
Mimi sijawahi kumtafuta mbunge kutokana na katiba yetu kutompa mbunge mamlaka ya maamuzi kwenye eneo lake, mimi naomba na mbunge anaomba sisi sote tunaomba! Makamu wa rais ana wadhifa muhimu sana kwenye nchi inayotumia katiba kujiendesha, makamu wa rais anayo mamlaka kikatiba japo hapa tumekoroga CCM na serikali kwenye chungu kimoja huku CCM ikijimilikisha nchi. Katika kipindi alichokosekana ofisini kuna wengi walikwazika kuhudumiwa matatizo ambayo yangetatuliwa na yeye kutokana na mamlaka yake.
 
Muahakilishi wako ni mbunge sio makamu wa Raisi
 
Amini hivyo ila ukweli ni serikali ina mipango yake bila kuwasiliana na mbunge, na kulijua hilo mbunge huenda bungeni bila kuonana na mimi kwanza na hata akirudi hanijulishi alichokifanya, pia alikwisha hama huku kwetu.
 
Watanzania sio wajibikaji kiasi hicho, ni kutaka kupata taarifa za kuwafurahisha, za kifo kama kawaida kwa masikini, mbona wengi hajui hata wa bunge wao na hawahoji wako wapi
Wewe utakuwa na roho ya shetani usiwapakazie watz roho mchafu, ni nani angefurahia kifo cha Dr. Philip Mpango ktk nchi yetu? Dr. Mpango kwa uelewa wangu pamoja na kwamba binadamu huwezi pendwa na wote lakini Dr. Mpango hajafikia na hatofikia hicho kiwango cha kuchukiwa na watz hadi aombewe kifo. Watu walitaka kujua yu wapi makamu wa raisi na si vinginevyo kama kuna mliokuwa mnamwombea kifo labda huko kwenu ccm makao makuu ya shetwani mbulula mkubwa weye.
 
Rais Samia: "Ukiwa public figure usipoonekana lazima watu wajiulize"

Kwa kulijua hilo ulikuwepo ulazima ws sisi wananchi kujulishwa alipo mtumishi wetu ambaye hayupo kwenye nafasi hiyo kwa ajili yenu.

Tatizo linakuja mnapotuona sisi wananchi ni watu wadogo sana hatulazimiki kujua kiongozi alipo!

Makamu wa Rais anayo ofisi hivyo kuna wananchi huhitaji awahudumie yeye binafsi kutokana na mamlaka yake.

Kisa hiki cha kutoweka kimyakimya kwa Makamu wa Rais kinatokana na kutokutumika kwa katiba.

Nchi inaendeshwa bila katiba kila kiongozi anafanya atakavyo akiamini hakuna wakumfanya kitu isipokuwa rais tu!

Mheshimiwa Rais ikikupendeza tujulisheni alikokwenda Makamu wa Rais.
Wakumbuke....hao wanalipwa kodi za wananchi wasijisahau......wakajiona Miungu watu
 
Watanzania sio wajibikaji kiasi hicho, ni kutaka kupata taarifa za kuwafurahisha, za kifo kama kawaida kwa masikini, mbona wengi hajui hata wa bunge wao na hawahoji wako wapi
Ni kosa kuwa maskini? Ni kosa kufurahia Kifo cha mtu?
 
Amini hivyo ila ukweli ni serikali ina mipango yake bila kuwasiliana na mbunge, na kulijua hilo mbunge huenda bungeni bila kuonana na mimi kwanza na hata akirudi hanijulishi alichokifanya, pia alikwisha hama huku kwetu.
Mbunge hana mamlaka yeyote zaidi ya kwenda kufikisha maombi ya matatizo ya maendeleo ya jimbo lake ili ikiwapendeza wenye mamlaka wayatatue yale matatizo !!
Kwahiyo Mbunge hawezi kulinganishwa na Public figure ambaye ndiye Namba mbili kwa ukubwa katika Nchi !!

Uzuri ni kwamba Public figure namba moja ameliona hilo na ameshalitolea ufafanuzi kwamba asipoonekana public figure kwa muda mrefu lazima watu watajadili na kuuliza kulikoni !!
Asante Mhe Rais 🙏🙏
Case closed !!
 
Sio kosa kua masikini ila ni dhambi kua na roho mbaya ndo inao sababisha kufurahia kifo cha mtu mgine.
Wapi wamesema ni roho mbaya kufurahia kifo cha mtu? Mungu angemhitaji abaki duniani asingemchukua. Vifo ni sehemu ya maisha ni lazima tufe na tuliowakwaza watafurahia na watu wetu wa karibu watalia.
 
Back
Top Bottom