carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 343
- 899
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuondoka nchini leo, Novemba 10, 2026, kuelekea jijini Antalya, Uturuki, kuhudhuria Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari S. Machumu, akiwa nchini Uturuki, Rais Samia atahudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali (Antalya Leaders’ Summit), pamoja na kushiriki kikao cha ngazi ya juu kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia barani Afrika.
Aidha, Rais Samia anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake, Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan, kwa mazungumzo yatakayohusu masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya mataifa hayo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiagana na viongozi mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere JNIA) Jijini Dar es Salaam, tarehe 10 Novemba, 2026 kabla ya kuondoka kuelekea Jijini Antalya, Uturuki, kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya
Tabianchi (COP31).