Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

6 Pack

JF-Expert Member
Apr 17, 2022
1,826
4,076
KWANZA HIVI NDIO VYEO VYAKE

1) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2) Mkuu wa nchi na kiongozi namba moja kwa pande zote mbili za Muungano.
3) Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama.

Hivyo ni vyeo ambavyo vinamruhusu mheshimiwa Rais kuchukua hatua kwa mtu yoyote wa serikalini ambae anafanya kazi yake kinyume na sheria za nchi, aidha kwa yule anaeiibia serikali, anaetoa rushwa, anaepokea au kuchelewesha mipango ya serikali hasa inayohusu maendeleo nk.

Inasikitisha sana mtu mwenye vyeo hivyo anashindwa, au anasita kuwachukulia hatua kali za kuagiza wakamatwe na kufunguliwa mashtaka wale wote waliopatikana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma serikalini na badala yake Rais eti anawaomba tu waachie nafasi zao bila kufungwa au kurudisha fedha hizo ili zikatumike katika mambo mengine ya kimaendeleo.

Hata wale aliosema kwamba kila report zinapofika watu hao hao hukutwa na tuhuma zile zile ilitakiwa wakamtwe kwa tuhuma ile ile ya kwanza na kubanwa vizuri walipozipeleka fedha zetu, badala ya kutaka eti washushwe vyeo au kuhamishwa ofisi.

Yani mwizi wa ndala akamatwe na kufungwa huku mwanasheria wa serikali akitafuna kodi zetu kwa kuendesha kesi yake, afu yule anayeiibia serikali mabilioni ya shilingi ahamishwe tu kituo ili akaendelee na utafunaji wa fedha zetu huko katika ofisi nyingine. Ni kwanini asifukuzwe kazi ili nafasi yake ichukuliwe na mtu mungine na ukizingatia kuna watu wengi wana elimu zao mitaani lakini kazi hawana?

Lakini pia sio aishie kufukuzwa tu bali afunguliwe kesi ya uhujumu uchumi na mali zake zote zitaifishwe na kurudishwa katika mikono ya wananchi.

China imeweza kupiga hatua duniani baada ya viongozi wa nchi hiyo kusimamia vyema kodi za wananchi wao kwa kutoa adhabu kali kwa yeyote atakaejaribu kugusa fedha za serikali. Pia hata Rwanda ipo vizuri baada ya raisi wa nchi hiyo kukitumia vyema cheo chake.

Rais na amiri jeshi mkuu ukibaki kulalamika, unafikiri mawaziri na viongozi wengine wa kawaida wataweza kuwa na uwezo wa kujiamini kuchukua hatua kweli.

Kama kulalamika umeshalalamika kwa zaidi ya miaka miwili sasa lakini upigaji ni ule ule. Sasa kabla ya kuwaambia watu na hili mkalitizame, tunakuomba na wewe kwanza ujitizame kwamba hiyo ndio njia sahihi ya kuendelea ku deal na mafisadi.

Hebu tumia nguvu zako ulizopewa na katiba yetu kuwachukulia hatua wabadhilifu wa kodi zetu, kabla na sisi hatujaingia barabarani kama wakenya.

Ukicheka na nyani shambani usishangae kuvuna mabua.
 
CCM ni janga kubwa Sana hapa nchini.

Solution ya hiyo "laana" ni kuipiga chini CCM katika uchaguzi ujao
Binafsi naona vyama vyote Tanzania au Afrika nzima vimeanzishwa kwa lengo kutafuna fedha za wananchi, ndomaana ukivichunguza vyama vyote vya upinzani na tawala, hata uendeshaji wao ni wa upigaji upigaji tu.

Cha kufanya ni kuwa na wagombea huru ambao watagombea uongozi bila kupitia chama chochote cha siasa. Maana wanasiasa wote ni wezi, waongo na wanafiki.
 
Tatizo wala si SSH. Bali ni mfumo uliomfikisha hapo. Wengine wanadai Bora JPM lakini Mimi nasema mfumo kwenye Taifa la mamilioni ya watu haubadilishwi na mtu mmoja.
Fanyeni overhaul ya mfumo mzima uliotengenezwa na ccm.
Otherwise mtawalaumu sana wezi na Rais wenu.
Kwa hii mifumo iliyopo hata akija malaika mkuu Gabriel baada ya miezi kadhaa atakuwa mpiga Dili zaidi ya hawa waliopo!
 
Mifumo ipi mkuu? Kwamba raisi kumsimamisha kazi au kumfukuza kazi mtu alietafuna fedha za umma na kuagiza vyombo vya ulinzi vimkamate na kumhoji na ikiwezekana afikishwe mahakamani nayo inahitaji kubadilisha mfumo?
 
Sasa Mkuu... Utawasimamisha wangapi uache wangapi? Rais mwenyewe anakwambia yanaanzia ndani hayo!

Zamani kipindi hatuna uhakika wa sabuni chawa walikuwa ni marafiki zetu. Sasa ukiwa hujui mtabaki kama nyani wale wanavofanya leo mnaanza kutafuta chawa mmoja mmoja. Nakwambia walikuwa hawaishi asee.

Wazazi wenye akili walikuwa wanachukua nguo zote na kuziloweka kwenye maji moto. Basi mtakuwa na amani kwa muda kadhaa!

Hiyo ndo overhaul ninayozungumzia... Yaliyopo kote kote TTCL, TRC, ATCL, BANDARI, TRA, Benki, etc ni matokeo ya mfumo.

Ondoa mfumo ulete unafuu
 
Nchi inaendeshwa kwa kufuata katiba. Rais akiamua kutumia madaraka yake unavyotaka si tutarudi kwenye mambo ya awamu ya 5? Vyombo vya dola ndo vinatakiwa viwakamate wahusika na kuwapeleka mahakamani. Tukisema Mama aanze kutumia ubabe hakutakalika. Tumshukuru sana kwa kuamua kufuata utawala wa kisheria.
 
Vyombo vya dola haviwakamati na mwamuzi wa mwisho ni raisi
 
Mifumo ipi mkuu? Kwamba raisi kumsimamisha kazi au kumfukuza kazi mtu alietafuna fedha za umma na kuagiza vyombo vya ulinzi vimkamate na kumhoji na ikiwezekana afikishwe mahakamani nayo inahitaji kubadilisha mfumo?
Sindio mfumo wenyewe wa katiba unavyotaka Uwajibishaji. Tatizo La wabongo unafiki mwingi. Mbongo ukimkazia asiyumbe anakuona mnoko.
 
Back
Top Bottom