Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema aliyekuwa Waziri wa Afya na Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama alikuwa mstari wa mbele kuwatumikia Wananchi, Mwalimu wa uongozi na Mtu mwenye hofu ya Mungu na kwamba yeye alimuita kiraka kwakuwa kila Wizara aliyomuweka aliifanya kazi yake vizuri.
Akiongea wakati wa misa ya kumuaga Jenista Mhagama Jijini Dodoma leo December 13,2025, Rais Samia amesema “Katika maisha ninayoyafahamu ya Marehemu Jenista Mhagama sitosita kusema alikuwa Kiongozi Jasiri na Mlezi wa wengi ndani na nje ya Bunge, alikuwa mstari wa mbele kuwatumikia Wananchi wa Jjmbo lake na Watanzania kwa ujumla”
“Alikuwa nguzo ya matumaini kwa Wanawake na Vijana na mwenye hofu ya Mungu, alikuwa Mwalimu wa taaluma na Mwalimu katika uongozi alitumia kipawa chake cha ualimu kulea na kusimamia Mawaziri, Wabunge na Mawaziri walimuheshimu na yeye alijiheshimisha, ametoa mchango mkubwa kwenye Chama na Serikali”
“Mhagama alikuwa Mtu asiye na mzaha lakini Mcheshi, alikuwa Mnyenyekevu kwa Mungu wake, mambo yaliyofanya akapendwa na Watu walio chini yake na Viongozi wote, Jenista alipata fursa ya kufanya kazi chini ya uongozi wangu kama Waziri kwenye Wizara mbalimbali, na nilimpa jina la kiraka kwamba kila nilipomuweka alifanya kazi vizuri, Waheshimiwa Wabunge na Mawaziri hususani wale wapya niwaase kufuata nyayo zake”