Rais Samia, chonde chonde

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,724
29,961
Chonde chonde rais wangu kuwa makini na wanaotamba kuwa wanakupenda

Chonde chonde rais wangu kumbuka asilimia kubwa ya watu wa bara wanawachukia wa visiwani

Chonde chonde rais wangu usiridhike na taarifa unazosogezewa mezani ukaziamini bika ya kuzifanyia uhakiki

Chonde chonde rais wangu usikubali kugombanishwa na wastaafu

Chonde chonde rais wangu usidhani wanaokusaidia wanafanya iwwpasavyo kufanya. Waangalie juu chini kisha fanya maamuzi

Chonde chonde rais wangu linda katiba iliyopo kwa kuruhusu vyama vya siasa kufanyakazi zao na mikutano bila zuio la dola

Chonde chonde rais wangu epukana na wazee kama yule aliyesema kuwa wwzuri wanaishi zaidi ya wabaya kwa sababu hayo ni makufuru mbele ya Mungu

Chonde chonde rais wangu kuwa muangalifu humo ndani ya CCM watu wana miungu yao inayoamua kesi kwa kuua wasiowataka. Jitenge nao usiwakaribishe kwenye karamu wataharibu sherehe

Chonde chonde rais wangu. Tanzania ni ya Watanzania hivyo nakusihi wapatie uhuru wao

Ndimi MwanaCCM ambaye amechoshwa na siasa za hila na wizi wa kura
 
Chonde chonde rais wangu epukana na wazee kama yule aliyesema kuwa wwzuri wanaishi zaidi ya wabaya kwa sababu hayo ni makufuru mbele ya Mungu.
Yamjaayo mtu moyoni mwake ndiyo ya mtokayo.
Wisdom, wisdom, wisdom ni kitu kidogo Lakini ni silaha kubwa katika maisha ya ujana na uzee.

He should be forgiven but not forgotten.
Non-sense Kamba.
 
Siku hizi sitaki kuvujisha sana ila angejua kwamba mama ni mzanzibar yuko makin na Wazanzibar kuliko wa Bara sitafunguka zaidi…..
Dua zetu Raia wema zimlinde Mama na remnants za ule Utawala wa yule Dhalimu.

Semeni Amin.
 
Yamjaayo mtu moyoni mwake ndiyo ya mtokayo.
Wisdom, wisdom, wisdom ni kitu kidogo Lakini ni silaha kubwa katika maisha ya ujana na uzee.

He should be forgiven but not forgotten.
Non-sense Kamba.
Kama nchi kumsamehe maana yake ni kuamini CCM ina uwezo wa kuongoza nchi kwenye huu ulimwengu unaohitaji misuli ya akili.

Mstaafu anaongea vile unategemea uongozi wake ulikuwaje?

Mungu ambariki sana Maxence Melo Mubyazi kwa kutuwekea jukwaa huru linalolinda uhuru wa maoni....

Tungeyasemea wapi haya
 
Ningekuwa Rais Samia ili kuoneshwa sijafurahishwa na kauli za Mzee Makamba namfuta mwanae uwaziri halafu namkatama namuweka kizuizini ili aone hii nchi siyo ya kufurahia kifo cha rais aliyekuwa madarakani.
CCM haina kiongozi mwenye uthubutu wa kuheshimisha nchi.

Sijasema kuwa Rais hawezi kufanya ulichoshauri lakini nimesema CCM haina mwenye uthubutu wa kufanya hayo.

Uthubutu wao sasa ni kuwakalisha viatu kwenye mitambo ya kudukua ili kututafuta sisi tunaokata network kila sekunde.

Tunalinda HATAMU hatulindi legitimacy ya nchi
 
Ni shairi au ni unafiki

Who hate who you idiot?

Mmetunyima ardhi siye hatuwezi ridhi ,mmetunyima tujenge makanisa ,mmetunyima haki yetu kama watz halafu chonde chonde fool .

Misikiti kibao bara,mnaiendesha mutakavyoo,mnaweka miliki ardhi mnajitoa Kwa Raha zenu bado chonde chonde mpuuzi huyuuu .

Kerooo peleka huko na dishi lako lililoyumba
 
Ingekuwa watu wa bara wanawachukia sana watu wa visiwani wangewaachia waendelee kuishi bila bughudha yeyote Tanzania Bara? Au unajua kuna maeneo, biashara, shule, vyuo, hospitali huku bara ambako mzanzibari anabaguliwa? Kuna mzanzibari amezuiwa kumiliki ardhi na watanzania bara kwa sababu tu ni mzanzibari? Au kuna aliyekatiliwa kuoa au kuolewa na mtanzania bara kwa sababu tu ni mzanzibari?

Ninachojua mimi wazanzibari ( sijui kama ni majority) ndio wana matatizo na watanzania bara na kuna sheria zao ambazo hazimpi usawa mtu wa bara na mzanzibari akiwa Zanzibar! Najua vile vile kuwa hali haikuwa shwari kati ya waunguja na wapemba.

Kwenye hili la chuki mnatuonea sisi mnaotuita machogo katika kuthibitisha mapenzi yenu kwetu.

Amandla....
 
Ni shairi au ni unafiki

Who hate who you idiot????
Mmetunyima ardhi siye hatuwezi ridhi ,mmetunyima tujenge makanisa ,mmetunyima haki yetu kama watz halafu chonde chonde fool .

Misikiti kibao bara,mnaiendesha mutakavyoo,mnaweka miliki ardhi mnajitoa Kwa Raha zenu bado chonde chonde mpuuzi huyuuu .

Kerooo peleka huko na dishi lako lililoyumba
Barikiwa mkuu
 
Back
Top Bottom