Rais Samia bingwa wa siasa Tanzania

NTIGAHELA

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
362
254
"Siasa Ina sura Nyingi, Vijana Tubadilike Tuwe Watu Wa Logic Tukashinde Mihemko Yetu." -ntigahela, Mwanaharakati Huru.

Vijana Tumekariri, Tunaendeshwa na Mihemko ya Kisiasa, Yaani Tunaamini Lugha Kali, Uhasama wa Kiitikadi ndio Upinzani Hasa, Kumbe Siasa Yenyewe Inasura nyingi, inarangi nyingi na inaladha nyingi_ leo mnagombana Kesho mnapatana na ugovi wa Kisiasa si wangumi na mawe ni ugovi wa Hoja kwa Maneno mengine siasa ni Ushawishi. Kwenye siasa kuna kushawishi na kushawishiwa.

Tukumbuke Kuwa CHADEMA, NCCR, ACT, UDP nk ni kipimo cha uwezo wetu kifikra na usahihi wa itikadi, falsafa, na sera zetu. Tunaweza kuwa CHADEMA na tukawa hatupo sahihi Kiitikadi, kifalsafa, kisera na kimtazamo hata tukiliganishwa na ccm, kumbe kusikiliza Wengine ni Bora kuliko kuongea Muda Wote hata ukidhani Upo sahihi 100% wape Wengine nafasi waseme ujinga wao since sometimes mad man can say truth.

Pamoja na Kwamba Tunaamini kwamba CCM ni mashetani kuna wakati ccm wanakuwa na Dhamira ya Dhati ya Kulijenga Taifa letu kwa ushirikiano. Maisha ama tuseme kasumba ya kukariri Kwenye siasa haifai, ni rigid thoughts kujiaminisha kwamba Chadema pekee, ACT pekee au CCM pekee ndio inauwezo na fikra za kuisukuma Mbele Tanzania kimaendeleo. Waasisi wa vyama vingi hawakuwa vilaza Kiasi hicho kwamba wawe na vyama vingi jina kwa malengo ya chama kimoja kuhonzi/kujimilikisha Maamuzi ya Nchi kwa kudhani chenyewe ni chama pekee chenye Dhamira Njema.

Viongozi wa Vyama vyetu vya CCM Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais wetu Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa pamoja Tena siasa sio uhodari wa kubishana Bali siasa ni kushawishi na kushawishiwa kihoja.

Hivyo si jambo baya Kiasi cha kupiga picha mbowe na SAMIA pamoja
kushawishiwa na Mh. Suluhu. Ni Siasa tu, kinachoendelea ni nadra au tuseme hakiwezekani kotokea Kwenye Nchi inayoongozwa ama tuseme kutawaliwa na mtu mwenye Sifa za kujimwambafai Yaani dikteta.

Mama anasimamia Kauli yake ya kwamba tufanye siasa za kistaarabu. Wanasiasa Kukaa Meza Moja na Kujadiliana ni Ustaarabu wa Hali ya Juu, ni kielelezo tosha kwamba Nchi Yetu ina Wanasiasa waliopevuka Kisiasa. Tuna kila sababu ya Kuipongeza Serikali iliyopo madarakani. Kunasomo hapa tunapaswa kujifunza, kwamba AKILI ni muhimu Kwenye Uongozi kuliko Nguvu.

Kwa Maana Hiyo tunapokosoa au kushauri hatunabudi kuweka chini manguvu ili tutumie AKILI pekee. Kwani ndio silaha sahihi ya siasa za kistaarabu.

Toa Maoni yako...
 
Tunataka katiba mpya ambayo itaondoa mifumo ya kishetani
Katiba mpya wakati ubongo umepigwa njaa kali na stress haina msaada wowote.

Tuelekeze nguvu kwa kuboresha maisha ya watu na miundombinu.
 
Kama una njaa sana hamia Burundi
Katiba mpya wakati ubongo umepigwa njaa kali na stress haina msaada wowote.

Tuelekeze nguvu kwa kuboresha maisha ya watu na miundombinu.
 
Utawala wake umebadilisha kabisaa upepo wa kisiasa ambao kwakweli kabla ya hapo siasa zilikuwa za chuki na migogoro mikubwa sana. Ameimarisha demokrasia. Sasa viongozi wa kisiasa wanashindana kwa hoja sio matusi.

Rais anajumuika na chama Cha upinzani na kuwahutubia kwa hoja sio matusi., kwakweli mama sio mtu wa kawaida ni kiongozi wa kipekeee sana sana ni zaidi ya dokta anafaa kuitwa profesa.

Huyu ndiye Mama jasiri Tanzania na Afrika kwa ujumla, anaye amini kushindana kwa hoja
 
Profesa, dokta mheshimiwa,Mama,Rais Samia🐒🐒🐒

 
HONGERA MAMA SAMIA UTAWALA WAKO UMEONDOSHA GIZA NENE NA KULETA NURU, MWANGAZA NA TUMAINI KWA WATANZANIA WOTE, BARA NA VISIWANI.
Naungana na mtoa mada ispokuwa binafsi sioni ni aina gani ya shahada ya kumfaa, naona kama shahada zote bado ni ndogo sana.
 
HONGERA MAMA SAMIA UTAWALA WAKO UMEONDOSHA GIZA NENE NA KULETA NURU, MWANGAZA NA TUMAINI KWA WATANZANIA WOTE, BARA NA VISIWANI.
Naungana na mtoa mada ispokuwa binafsi sioni ni aina gani ya shahada ya kumfaa, naona kama shahada zote bado ni ndogo sana.
Hongera zake
 
Back
Top Bottom