Rais Samia, bila mabadiliko ya msingi ya Sheria hutapata wawekezaji makini

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,529
41,045
Natambua kuwa Rais Samia anataka kuvutia uwekezaji wa ndani na nje lakini hajagusa maeneo ya msingi ambayo yanaangaliwa na wawekezaji.

1) Nchi ambayo sheria za kodi zinabadilishwa kila mwaka, kamwe haiwezi kuvutia uwekezaji mkubwa kutoka kwa wawekezaji makini
Kati ya vigezo vikubwa vinavyoangaliwa na wawekezaji ili wakawekeze wapi, namba moja ni stability of fiscal regime. Hakuna mwekezaji anayeweza kwenda kuwekeza mahali ambapo, unaamua kuwekeza, kodi ni nyingine, unaanza kutengeneza miundombinu yako, kodi imebadilishwa, unamalizia kujenga, kodi imebadilika, unaingiza mitambo kodi imebadilika. Nchi ya namna hiyo, wawekezaji utakaowapata ni wale wa kufanya uchuuzi. Wale wa kuagiza bidhaa China, Thailand, Uturuki na India. Hawa wanaangalia, kodi ikiwa mbaya, wanaacha kuagiza. Ndiyo maana mpaka leo hii, pamoja na kelele na vikao vingi vya kuvutia wawekezaji, mwekezaji wa mwisho mkubwa alikuwa Dangote, ambaye naye anajutia kwa nini aliamua kuja kuwekeza Tanzania.

2) Utawala wa Sheria. Hili ni eneo ambalo wawekezaji wanalitazama sana
Huwezi kwenda kuwekeza mahali ambapo hakuna utawala wa sheria. Rais anaweza kubadilisha chochote, Waziri anaweza kubadilisha chochote, DC, RC, RPC, OCD, anaweza kukusweka ndani wakati wowote bila kosa lolote, na bila kufuata sheria. Mwekezaji ambaye maisha yake yote hajawahi kukaa mahabusu, hajawahi kushtakiwa, anaheshimika kwao ja mahali pengine Duniani, anafika Tanzania, mjinga mmoja anatoa amri, weka huyo ndani, na anawekwa ndani. Mfano mzuri ni yule mkurugenzi wa kiwanda cha Tumbaku Morogoro aliyelazwa kwenye mahabusu za polisi kwa amri ya RCO, sababu tu TCO amepokea majungu toka kwa wafanyakazi. Kinachompa mtu uhakika wa anachokifanya ni sheria, na jinsi sheria hiyo inavyoheshimiwa na Serikali.

3) Kushindwa kuelewa competetiveness ya Dunia katika kuwapata wawekezaji
Dunia nzima, nchi tajiri na maskini, zote zinawatafuta wawekezaji. Kiongozi mkuu wa China kila wakati yupo Ulaya kutafuta wawekezaji wa kuwekeza China, Saudi Arabia timu yao ipo Marekani wakati wote kutafuta wawekezaji, UK inatafuta wawekezaji, Dubai wanatafuta wawekezaji. Nchi yetu Tanzania ina nini cha pekee ambacho tunaweza kusema ndiyo strength yetu dhidi ya nchi nyingine katika kuwapata wawekezaji?

Umeme wako bei juu na hauna uhakika, njia usafirishaji ni aghali na wakati fulani mbovu, malighafi nyingi hakuna, utawala wa sheria hauheshimiwi, kodi juu na zinazobadilika kila leo, ni nini cha pekee unachozidi wengine hata umfanye mwekezaji mkubwa asiende China, Brazil, Vietnam, Hong Kong Malaysia au UAE, badala yakeaje Tanzania?

Serikali ijifunze kutoka Uingereza waliowahi kukaa na sheria ya uwekezaji kwa zaidi ya miaka 50, bila kuibadilisha ili kuwapa confidence wawekezaji.

Serikali ijifunze toka Dubai, Ghana, Mauritius katika kuwa na kodi za chini na rafiki za kuvutia wawekezaji.

Serikali ijifunze toka Malaysia katika kuheshimu wawekezaji.

Serikali ijifunze toka Botswana na Namibia katika kuheshimu mikataba ya uwekezaji.

Serikali ijifunze toka Singapore katika kuhakikisha Serikali inaajili super intelligent people katika ofisi za Serikali, na hasa zinazoshughulika na uwekezaji, kodi na utawala badala ya kuteua makada wa chama, ambao wengi wao uelewa wao katika uchumi wa Dunia, biashara, uwekezaji na utawala bora, ni mdogo sana.

Mataifa hayo niliyoyataja yote yamefanikiwa sana katika kuvutia wawekezaji.

Rais kama unataka kuvutia uwekezaji, kuinua uchumi, kutengeneza ajira, kuongeza uwigo wa kodi na mapato ya Serikali, kwanza kwa haraka badilisha sheria mbalimbali zinazohusiana na uwekezaji, kodi, na utawala wa sheria ili kuhakikisha tunakuwa washindani imara katika kuvutia wawekezaji. Vinginevyo, utazunguka Dunia nzima, utafanya vikao na wawekezaji mbalimbali, watakusikiliza, watakupa heshima na matumaini, lakini mwishowe hutawapata. Wawekezaji siyo wajinga, wengine ni practical super intelligent people, hawaendi kuwekeza mahali kwa sababu Rais amesema au amewakaribisha bali wanaangalia utimilifu wa selection criteria.
 
State Fragility, Growth and Development.

Ni jinsi gani taifa lipo hatarini kiuchumi, kijamii, na kisiasa.

Je taifa litaendeleza uchumi wa kati ulowekwa chini ya usimamizi wa hayati JPM?

Na mwisho je nchi inasimamia malengo ya maendeleo ilojiwekea?

Taifa letu kwa sasa lipo njia panda katika maeneo yote matatu hapo juu.

Mfano ni kuhangaika na mfumo wa kodi za miamala mafuta na kadhalika.

Wawekezaji wengi wanadai "Right to Explore" badala ya "Permission to explore"

Huwezi kuja katika nchi ya watu ukataka uwe na haki ya kuchimba madini utakavyo na kisha usafirishe nje ya ya hiyo nchi mwenyeji kienyeji.

Lakini bado kuna njia kadhaa za kufatuta suluhu katika suala la kodi kwamba ni mfumo upi wa kodi uwe maalum kwa wawekezaji.

Hivyo sheria ni muhimu kuangaliwa kwa makini badala ya kuanza kufanyia marekebisho ya sheria ya madini ya 2017 ambayo inaionuafaisha Tanzania na wawekezaji kwa kugawana asilimia 50/50.
 
State Fragility, Growth and Development.

Ni jinsi gani taifa lipo hatarini kiuchumi, kijamii, na kisiasa...
Nadhani hukuielewa hiyo 50/50. 50/50 ni economic benefit, haimaanishi mgawanyo wa faida 50/50. 16% free carried shares haiwezi we kukupa 50% ya net profit.

Kuna nchi kama Botswana zina mpaka 50% ownership kwenye baadhi ya projects lakini hawapewi bure. Hiyo 50% serikali inalipia kwa kutochukua kodi mpaka kiasi ambacho Serikali ingelipia kupata 50, kinapokuwa kimelipwa. Na ndivyo ilivyo kwa Uganda kwenye mradi wa mafuta, ambao government owmership ni 15%.
 
Back
Top Bottom