#COVID19 Rais Samia atupa kijembe kwa wapinga chanjo ya UVIKO-19. Asema hauwezi kushindana na Mwanadamu mwenye kinywa

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,730
10,033
“Kuna Mwanangu (Goodluck Gozbert) aliimba ‘hauwezi kushindana na Mwanadamu mwenye kinywa’, mwenye kinywa atasema tu anayotaka kusema lakini ukweli utabaki palepale, chanjo hizi za Covid-19 zinasaidia kupunguza maumivu na hatari ya vifo kwa Watu".

“Chanjo hatusemi ni kinga kabisakabisa lakini hata Covid-19 ikikupata inakupata polepole, risk za kufa kwa wingi zinapungua, niwaombe Wanamichezo Kama mnataka kuendelea na michezo vizuri chanjeni, Mimi Mama yenu, Mkuu wenu, sitapeleka Jamii yangu kwenye hatari”.

“Chanjo ni muhimu, niwape mfano kuna Watu tumechanja nao lakini kwa bahati mbaya virusi vya Corona vikawanyemelea, wamekwenda tu vizuri na shughuli zao unampigia simu anasema niko vizuri baada ya siku tatu, nne ameenda kupima hakuna hicho kitu”.
 
Sio kinywa, ni hoja!!! Nyie watu vipi lakini???!!!!!, kinywa kinachotoa hoja inabidi ushindane nacho kwa hoja!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!, sio vijembe!!!!!!!
Tukiwauliza mtuambie , side effects za hizi chanjo baada ya miaka mitano kwa aliyechoma na kwa watoto wake atakaowazaa ni zipi, wanabaki kutoa macho kama panya aliyebanwa kwenye mlango...
 
“Kuna Mwanangu (Goodluck Gozbert) aliimba ‘hauwezi kushindana na Mwanadamu mwenye kinywa’, mwenye kinywa atasema tu anayotaka kusema lakini ukweli utabaki palepale, chanjo hizi za Covid-19 zinasaidia kupunguza maumivu na hatari ya vifo kwa Watu”———Rais Samia
 
KWANZA KILA UKICHANJWA UNALAZIMISHWA KUSAINI KUWA LIKITOKEA LA KUTOKEA BASI USIHITAKI SERIKALI..WHY? KWANINI UKICHANJWA KWANINI UNALAZIMIKA KUVAA BARAKOA? BADALA YA SERIKALI KUJIBU HOJA WAMEBAKI KULIALIA NA KUSEMA INAONGEZA HADI NGUVU ZA KUGONGWA
 
KWANZA KILA UKICHANJWA UNALAZIMISHWA KUSAINI KUWA LIKITOKEA LA KUTOKEA BASI USIHITAKI SERIKALI..WHY? KWANINI UKICHANJWA KWANINI UNALAZIMIKA KUVAA BARAKOA? BADALA YA SERIKALI KUJIBU HOJA WAMEBAKI KULIALIA NA KUSEMA INAONGEZA HADI NGUVU ZA KUGONGWA
Kwa na ww uko na Bishop Gwajima?
 
1f99c.png
 
Uzi umepoooooooooaaaaaa, yaani huwezi amini jinsi watu wanavyoogopa kujibu hoja, ni hoja kwa hoja tu.
 
Back
Top Bottom