waziri2020
Senior Member
- May 31, 2019
- 190
- 451
Mbunge mstaafu wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, James Ole Milya leo Agosti 3 mwaka 2020 amechomwa chanjo ya Uviko -19 kama njia mojawapo ya kujikinga na ugonjwa huo hatari duniani.
Ole Milya amejipatia chanjo hiyo aina ya Jansen kutoka kampuni ya Johnson & Johnson katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mt Meru ambapo aliambatana na baadhi ya wakazi wa jijini Arusha.
Akizungumza muda mfupi Mara baada ya kupatiwa chanjo hiyo Ole Milya alisema kwamba kwanza ameamua kuchanja kama njia mojawapo ya kujikinga na maradhi ya Uviko-19 .
Ole Milya alitaja sababu nyingine iliyomsukuma ni kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kupambana na janga la Uviko -19 duniani.
Ole Milya alisisitiza kuwa kama Rais Samia amepata chanjo hiyo yeye ni nani wa kuipinga na kuwataka watanzania kuondokana na hofu kwa kuwa Rais Samia ambaye alimtaja kuwa ni mfariji mkuu wa taifa(comforter in chief) alishawahakikishia kwa vitendo usalama wa chanjo hiyo.
"Kama Rais Samia amechanjwa Mimi ni nani wa kukataa?Mimi ni kiongozi ni lazima nionyeshe mfano kwa wengine wito wangu wa watanzania tuondoe hofu twende tukapate chanjo" alisema Ole Milya
Mwisho.