PreGE2025 Rais Samia atoa mkono wa Eid kwa watoto yatima Kagera

PreGE2025 Rais Samia atoa mkono wa Eid kwa watoto yatima Kagera

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Ikiwa yamesalia masaa machache kuelekea sikukuu ya Eid Al- Fitri ikiashiria kutamatika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa mkono wa Eid kwa vituo vyote vya kulelea Watoto mkoani Kagera hapo jana tarehe 29/03/2025.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa wakati wa kukabidhi Sadaka hiyo amesema kuwa Rais Samia amekuwa na utamaduni wa kuwakumbuka Watoto hao na sasa ametoa vitu vitakavyowawezesha kusherehekea vyema na kufurahia.

Baadhi ya viongozi kutoka kwenye vituo vya kulelea Watoto hao wamemshukuru Rais Samia kwa kuwa na moyo wa kutoa na kuwlikumbuka kundi hili ambalo nalo linatakiwa kufurahia sikukuu hizi.

Nao Watoto wamemshukuru Rais Samia shukrani zilizoambatana na dua maalumu ya kumuombea afya njema na umri mrefu wenye manufaa.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Back
Top Bottom