Kwa taarifa yako, hata kama huu mkataba wa bandari ungesainiwa kati ya Tanzania na Vatican ningeupinga.
Hata kama ungesainiwa na kampuni inayomilikiwa na serikali ya Kikristo kama ilivyo kule UK ningeupinga.
Nashangaa unajitoa ufahamu: Hayati Apson alikataa mkataba wa kuuza Kigamboni kwa Wamarekani kwa kuwa ungetengeneza
Koloni la Walowezi wa Kimarekani nchini Tanzania, na hivyo kufinya enzi (sovereignty) ya Tanzania.
Mimi na wenzangu tunapinga ujenzi wa
Makoloni ya Walowezi wa Kigenini nchini Tanzania, bila kujali kama mlowezi ni Mkristo, Muislamu, Mwarabu, Mzungu, Mkorea, Mchina, Mhindi, Mmarekani, na kadhalika.
Hivyo ndivyo vijana wote tuliopita mikononi mwa walimu nguli kama vile
Peter Nyamanchi Tyienyi (Kamisaa wa Dawati la Siasa ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa aliyemrithi Lyatonga Mrema) tulivyofunzwa na kuamini hadi leo.
Nyie vijana wa
TISS-Vodafasta shida tupu!
Critical thinking inawapinga chenga sana, kiasi kwamba mnanajisi ofisi nyeti, hata baada ya Baba wa Taifa kuwakumbusha kwamba
Ikulu ni Mahali Patakatifu!.
Take it from us: Hatukubali
enzi ya Tanzania kuuzwa kwa
vipande vya fedha kwa Waarabu, Wazungu, Wamarekani, Waingereza, Wachina au watu wengine wowote. Ni kwa sababu hii tunamshangaa waziri Mkuu Kassim majaliwa anayeendelea na mradi wa kufanya kazi kama
PRO wa
Walowezi wa Kiarabu nchini Tanzania. Anatukera!
Finally: Read this text loudly....
View attachment 2675507