Rais Samia ashiriki maadhimisho ya miaka 10 ya kuanzishwa kwa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC). Asisitiza Vijana kufundishwa aina zote tatu za vita

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki maadhimisho ya miaka 10 ya kuanzishwa kwa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC), leo tarehe 08 Septemba, 2022 jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa majeshi ya ulinzi (CDF) Jacob John Nkunda amesema dhamira ya kuanzisha chuo cha Taifa cha ulinzi ilikuwa ni kupunguza gharama za kupeleka maafisa wake nchi za nje pamoja na kuwafundisha maudhui yanayoendana na mazingira ya kitanzania.

Tangu kuanzishwa kwa chuo hiki mwaka 2012, mafunzo mengi yametolewa kwa washiriki mbalimbali ambao baada ya kuhitimu wamekuwa wanakiri umuhimu wa mafunzo haya hasa kwenye kuelewa maslahi mapana na taifa letu.

Naye Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa kusaidia ujenzi jengo la utawala na mafunzo na ameahidi kuendeleza uhusiano huo mzuri uliopo.

Akitoa hotuba yake ambapo alialikwa kama mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefurahishwa na aina mbalimbali za mafunzo yanayotolewa kwenye chuo hicho ikiweno yale yaliyohusisha mawaziri yaliyofanyikia siku za hivi karibuni.

Mafunzo haya yanalenga kujenga uzalendo na kuwafanya watu waisome dunia inavyokwenda hivyo kuwajengea utayari wa mambo yanayoweza kutokea baadae.

Mafunzo haya ni muhimu hasa katika mazingira ya sasa ambapo serikali imeamua kuifungua nchi.

Rais ameomba maafisa wa chuo hicho kukazia umuhimu wa kutoa mafunzo ya aina tatu za vita zinazo piganwa duniani kwa sasa ambazo ni vita za medani, mtandao na uchumi. Hii itasaidia kutengeneza vijana wenye utayari kwenye sekta zote za kidunia.
 
International hackers tutawaweza kweli? Nchi nyingi zinakutana na Ransomware na wanalipa.
 
Aina tatu za Vita vinavuopiganwa Tz
*Vita vya wingi na ukubwa wa kodi
*Vita vya uwepo, wingi na ukubwa wa tozo
*Vita vya mfumuko wa bei
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki maadhimisho ya miaka 10 ya kuanzishwa kwa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC), leo tarehe 08 Septemba, 2022 jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa majeshi ya ulinzi (CDF) Jacob John Nkunda amesema dhamira ya kuanzisha chuo cha Taifa cha ulinzi ilikuwa ni kupunguza gharama za kupeleka maafisa wake nchi za nje pamoja na kuwafundisha maudhui yanayoendana na mazingira ya kitanzania.

Tangu kuanzishwa kwa chuo hiki mwaka 2012, mafunzo mengi yametolewa kwa washiriki mbalimbali ambao baada ya kuhitimu wamekuwa wanakiri umuhimu wa mafunzo haya hasa kwenye kuelewa maslahi mapana na taifa letu.

Naye Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa kusaidia ujenzi jengo la utawala na mafunzo na ameahidi kuendeleza uhusiano huo mzuri uliopo.

Akitoa hotuba yake ambapo alialikwa kama mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefurahishwa na aina mbalimbali za mafunzo yanayotolewa kwenye chuo hicho ikiweno yale yaliyohusisha mawaziri yaliyofanyikia siku za hivi karibuni.

Mafunzo haya yanalenga kujenga uzalendo na kuwafanya watu waisome dunia inavyokwenda hivyo kuwajengea utayari wa mambo yanayoweza kutokea baadae.

Mafunzo haya ni muhimu hasa katika mazingira ya sasa ambapo serikali imeamua kuifungua nchi.

Rais ameomba maafisa wa chuo hicho kukazia umuhimu wa kutoa mafunzo ya aina tatu za vita zinazo piganwa duniani kwa sasa ambazo ni vita za medani, mtandao na uchumi. Hii itasaidia kutengeneza vijana wenye utayari kwenye sekta zote za kidunia.

Hongera sana mama
na kwa Jeshi la Anga kama watatumia zaidi watu wa liosoma Saiyansi ( Alevel) litakuwa na ufanisi wa hali ya juu sana. Nasema hivyo nikijua kuwa ukiwa na wataalamu 10 wenye msingi wa Physics (A-level) ufanisi wao ni sawa na jeshi la mamia ya watu. Mfano: Mahali adui anarusha makombora pengine 100; ukiwa na wataalamu hao unarusha moja tu au pengine mawili (unaokoa pesa, unaepusha uharibifu wa mali, na unaokoa maisha)
 
Back
Top Bottom