Rais Samia arudisha matumaini Mbarali

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
944
Ni kuhusu mgogoro wa ardhi katika eneo la Bonde la Mto Usangu. Akubali Wananchi kuendelea kulima

Na MWANDISHI WETU, Mbarali

MAKAMU Makamu Mwenyekti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahaman Kinana amewaambia wananchi wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amekubali ombi lao la kuendelea na shughuli za kilimo katika eneo lililozuiwa kupitia tangazo la Serikali la GN 28, kama ilivyokubaliwa mwaka jana.

Tangu kutolewa kwa katazo hilo, wananchi wamekuwa wakilalamika kuwa mchakato wa kufikia maamuzi hayo haukuwa shirikishi na kuiomba serikali kuliondoa katazo hilo ambalo linaathiri ustawi wa maisha yao na kipato.

Akizungumza wakati akihitimisha kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya, zilizofanyika katika Kijiji cha Chimala, Makamu Mwenyekiti Kinana alisema mgombea Ubunge wa CCM Bahati Ndingo, Madiwani wa CCM, Viongozi wa CCM na wananchi walimueleza amuombe Rais Samia waendelee kulima wakati suala hilo linazungumzwa.

“Nimemueleza Rais jana kuwa wananchi wa Mbarali wanaomba waendelee kulima kwa sababu msimu unaanza mwezi ujao (Oktoba) na Rais akasema sawa waendelee, kwa yale maeneo yote yaliyoruhusiwa mwaka jana Rais amekubali mwendelee kulima,” alisema.

Akizungumzia ombi la mgombea ubunge kuhusu ujenzi wa barabara iliyokaa muda mrefu kutoka Lujewa, Madibila hadi Mafinga, Kinana alisema atawasiliana na wahusika (Waziri wa Ujenzi) ili ujenzi wa barabara hiyo uanze kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

F6Vb-qwWwAAXjfV.jpg
F6Vb-qyXMAATgqw.jpg
F6Vb-qwWkAAcD07.jpg
F6Vb-q5WEAAowwI.jpg
 
Kupoteza fedha tu.

Kwani CCM wasingefanya kampeni mgombea wao asingetangazwa mshindi?
 
SAWA.
Ila hii katiba yetu ni ya hovyo sana.
Kwa hiyo uchaguzi umebatilisha maamuzi yaliyopelekea kuwafukuza katika bonde Hilo?.
Given that they decided correctly.
 
Back
Top Bottom