Rais Samia apongezwa kila kona ya nchi kwa msimamo wake wa kupeleka maendeleo kila mahali pasipo ubaguzi wala chuki

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,311
9,740
Ndugu zangu Watanzania,

Rais Samia anaendelea kujizolea sifa, kuandikwa jina lake kwa wino wa dhahabu katika mioyo ya Watanzania, kuacha alama za kukumbukwa na Watanzania kutokana na misimamo yake ya kizalendo na kibinadamu kwa Watanzania. Rais Samia kwa ujasiri, uchungu, ushupavu, uzalendo na msimamo wa hali ya juu sana amekataa kata kata kuingiza, kubariki na kuweka masuala ya upendeleo na ubaguzi katika kuwapelekea wananchi miradi ya maendeleo kwa misingi ya uchama au ubaguzi wa aina yoyote ile.

Rais Samia anatambua kuwa yeye ni Rais wa Watanzania wote, anatambua ya kuwa kila Mtanzania ana lipa kodi kwa njia tofauti tofauti, kila Mtanzania ana haki ya kuchagua chama akipendacho kulingana na sera za chama husika na kila Mtanzania ana haki ya kupelekewa huduma muhimu na serikali yake kutokana na haki asili ya kuwa Mtanzania wa kuzaliwa na anayelipa kodi.

Rais Samia anaona siyo haki wala siyo sawa wala siyo utamaduni wetu wa kuanza kupanda mbegu ya kubaguana kwa misingi ya kisiasa, anajua mbegu hii ikipandwa haitaishia hapa tu, anajua mbegu hii ikiachwa italitafuna Taifa lote vizazi na vizazi, ndio maana hayupo tayari kushiriki katika dhambi hii ya kuliangamiza Taifa.

Rais Samia amekemea na kujiuliza kwanini uwatese watoto wasio na hatia kwa kuwanyima fursa ya elimu kwa kutojengewa shule kisa tu eneo lao lina wapinzani wengi? Kosa lao nini hao watoto? Kwanini waadhibiwe kwa makosa ya wazazi wao? Kwanini uchepushe miradi kisa tu eneo hilo lina upinzani? Je hao siyo Watanzania? Je hawalipi kodi? Kama hutaki kuwapa miradi wanayostahili kwanini uende ukusanye kodi kwao? Kwanini uwabughudhi, watii sheria wakati huwatambui kuwa ni wananchi wako? Ni vipi sasa watarudisha moyo wa kuipenda serikali na chama ikiwa huonyeshi kuwajali na kuwathamini? Kwanini usiwapelekee maendeleo ili wajute kuwaunga mkono upinzani na kuanza kukuunga mkono wewe?

Kwa hakika, Rais Samia amedhihirisha usemi usemao kuwa mwenye haki akitawala na kuwa na mamlaka, nchi yote na watu wote hufurahi na kuishi kwa furaha, lakini muovu akitawala nchi hububujikwa kwa machozi na kutawala kwa vilio na mateso kwa watu. Rais Samia ni mama wa haki, ndio maana nchi ina amani, furaha, upendo, tabasamu na vicheko kila kona ya Taifa letu.

Rai kwa viongozi wote wa serikali na watumishi wa umma ni kuhakikisha ya kuwa mnatenda haki kwa watu wote pasipo ubaguzi wa aina yoyote ile na kwa misingi ya aina yoyote ile. Mama yetu na Rais wetu ni mcha Mungu na mwenye hofu ya Mungu, na hayupo tayari kushiriki au kubariki dhambi ya ubaguzi kwa misingi ya aina yoyote ile. Amedhamiria kuliungaisha Taifa letu na kujenga umoja wa kitaifa pasipo ubaguzi wala chuki, hataki ushetani na vitendo vya kishetani ndani ya utawala wake, anataka haki na usawa kwa watu wote. Anataka Taifa linalozungumza lugha moja, hataki kuwapa watu adhabu kisa tofauti za kimtazamo na kisiasa.

Huyo ndiye Rais Samia, mama wa shoka, jasiri muongoza njia, shujaa wa Afrika, nembo ya Taifa, nuru ya wanyonge, mama na kiongozi mpambanaji, komandoo wa vita, simba wa nyika, na sauti ya Afrika na mtetezi wa wanyonge anayeendelea kulipa raha, tabasamu na furaha Taifa letu. Kwa hakika, Rais Samia ni zawadi kwetu Watanzania tunayopaswa kuitunza kwa wivu mkubwa sana. Ni dhahabu itembeayo, japo vipofu wa akili na macho wanaweza wasione haraka haraka.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais Samia Anaendelea kujizolea sifa ,kuandikwa jina lake kwa wino wa Dhahabu katika mioyo ya watanzania ,kuacha alama za kukumbukwa na watanzania kutokana na misimamo yake ya kizalendo na kibinadamu kwa watanzania. Rais Samia Kwa ujasiri,uchungu, ushupavu,uzalendo na msimamo wa hali ya juu sana amekataa kata kata kuingiza, Kubariki na kuweka masuala ya upendeleo na ubaguzi katika kuwapelekea wananchi miradi ya maendeleo kwa misingi ya uchama au ubaguzi wa aina yoyote ile.

Rais Samia anatambua kuwa yeye ni Rais wa watanzania wote,anatambua ya kuwa kila mtanzania ana lipa kodi kwa njia tofauti tofauti,kila mtanzania ana haki ya kuchagua chama akipendacho kulingana na sera za chama husika na kila mtanzania ana haki ya kupelekewa huduma muhimu na serikali yake kutokana na haki asili ya kuwa mtanzania wa kuzaliwa na anayelipa kodi.

Rais samia anaona siyo haki wala siyo sawa wala siyo utamaduni wetu wa kuanza kupanda mbegu ya kubaguana kwa misingi ya kisiasa,anajuwa mbegu hii ikipandwa haitaishia hapa tu,anajuwa mbegu hii ikiachwa italitafuna Taifa lote vizazi na vizazi,ndio maana hayupo Tayari kushiriki katika Dhambi hii ya kuliangamiza Taifa.

Rais samia amekemea na kujiuliza kwanini uwatese watoto wasio na Hatia kwa kuwanyima fursa ya Elimu kwa kutojengewa shule kisa tu Eneo lao Lina wapinzani wengi? Kosa lao Nini hao watoto? Kwanini waadhibiwe kwa makosa ya wazazi wao? Kwanini uchepushe miradi kisa tu Eneo hilo lina upinzani? Je hao siyo watanzania? Je hawalipi kodi? Kama hutaki kuwapa miradi wanayostahili kwanini uende ukusanye kodi kwao? Kwanini uwabughudhi watii sheria wakati huwatambui kuwa ni wananchi wako? Ni vipi sasa watarudisha moyo wa kuipenda serikali na chama ikiwa huonyeshi kuwajali na kuwathamini? Kwanini usiwapelekee maendeleo ili wajute kuwaunga mkono upinzani na kuanza kukuunga mkono wewe?

Kwa Hakika Rais Samia amedhihirisha usemi usemao kuwa Mwenye Haki akitawala na kuwa na mamlaka nchi yote na watu wote hufurahi na kuishi kwa Furaha,lakini muovu akitawala nchi hububujikwa kwa machozi na kutawala kwa vilio na mateso kwa watu.Rais samia ni mama wa Haki ndio maana nchi ina amani,furaha,upendo,Tabasamu na vicheko kila kona ya Taifa letu.

Rai kwa viongozi wote wa serikali na watumishi wa umma ni kuhakikisha ya kuwa mnatenda haki kwa watu wote pasipo ubaguzi wa aina yoyote ile na kwa misingi ya aina yoyote ile,Mama yetu na Rais wetu ni mcha Mungu na mwenye hofu ya Mungu na hayupo Tayari kushiriki au kubariki Dhambi ya ubaguzi kwa misingi ya aina yoyote ile,amedhamiria kuliungaisha Taifa letu na kujenga umoja wa kitaifa pasipo ubaguzi wala chuki,hataki ushetani na Vitendo vya kishetani ndani ya utawala wake,anataka haki na usawa kwa watu wote ,Anataka Taifa linalozungumza lugha moja ,hataki kuwapa watu adhabu kisa Tofauti za kimtazamo na kisiasa.

Huyo ndiye Rais samia mama wa shoka,Jasiri muongoza njia,Shujaa wa Afrika ,Nembo ya Taifa,Nuru ya wanyonge,Mama na kiongozi mpambanaji,Komandoo wa vita,Simba wa Nyika na Sauti ya Afrika na mtetezi wa wanyonge anayeendelea kulipa Raha, Tabasamu na furaha Taifa letu. Kwa hakika Rais samia ni zawadi kwetu watanzania tunayopaswa kuitunza kwa wivu mkubwa sana.Ni Dhahabu itembeayo japo vipofu wa akili na macho wanaweza wasione haraka haraka.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Aghhhhhh Again chawa njaa Lukas. Wakupe ukuu wa wilaya tupumuzike
 
Lucas mwashambwa,
Hapo Kuna HOJA Gani?

Unauemtaja anatetea na kukumbatia DP world, hao ni Watanzania anaowatetea na kuwakingia kifua ?

Ngorongoro wamama wenzie wanalia wakisema Bora wafe kuliko kuhamishwa Toka ardhi Yao!!

Wananchi Gani anaowatetea?
 
Hapo Kuna HOJA Gani?

Unauemtaja anatetea na kukumbatia DP world, hao ni Watanzania anaowatetea na kuwakingia kifua ?
Taifa letu litaendelea kuvutia wawekezaji na kuwakaribisha kuwekeza mitaji yao nchini.Na katika uwekezaji wowote ule itazingatia maslahi mapana ya Taifa letu.
 
Aghhhhhh Again chawa njaa Lukas. Wakupe ukuu wa wilaya tupumuzike
Mimi sina njaa,nina kula kwa jasho langu na kujipatia kipato na shibe tangu kwa kutumia nguvu za mikono yangu,kwa kufanya kazi na shughuli halali kabisa na zinazotambulika na kisheria. Siishi kwa kutegemea fadhila au hisani kutoka kwa mtu yeyote yule.
 
Taifa letu litaendelea kuvutia wawekezaji na kuwakaribisha kuwekeza mitaji yao nchini.Na katika uwekezaji wowote ule itazingatia maslahi mapana ya Taifa letu.
Wawekezaji wa kusafirishwa wanyama hai kwenda kuanzisha zoo kwao?

Ni uwekezaji huo au uporaji raslimali zetu?
 
Wawekezaji wa kusafirishwa wanyama hai kwenda kuanzisha zoo kwao?

Ni uwekezaji huo au uporaji raslimali zetu?
Wanyama wetu ni mali yetu ni urithi wetu tuliopewa na Mwenyezi Mungu na ndio maana wanaendelea kulindwa vizuri sana katika hifadhi zetu.
 
Wanyama wetu ni mali yetu ni urithi wetu tuliopewa na Mwenyezi Mungu na ndio maana wanaendelea kulindwa vizuri sana katika hifadhi zetu.
Mlinzi wa wanyama wetu ni Maasai anayeondolewa Kwa nguvu Ili waporaji waje kuwapakia waende nje Kwa RUSHWA!!!
 
Mlinzi wa wanyama wetu ni Maasai anayeondolewa Kwa nguvu Ili waporaji waje kuwapakia waende nje Kwa RUSHWA!!!
Acha kujitoa fahamu kwa hiyo hao ndio huwa wanapambana na majangila yenye silaha za kivita? Hujui serikali yetu inatumia pesa nyingi sana kulinda wanyama wetu dhidi ya majangili huko mbugani? Au unafikiri ni kazi Rahisi kama kuja kuropoka hapa jukwaani? Hujui unapokuwa umelala na kukoroma usiku kucha kuna watanzania wenzetu wanakuwa wanakesha wanapambana kulinda wanyama wetu?
 
Acha kujitoa fahamu kwa hiyo hao ndio huwa wanapambana na majangila yenye silaha za kivita? Hujui serikali yetu inatumia pesa nyingi sana kulinda wanyama wetu dhidi ya majangili huko mbugani? Au unafikiri ni kazi Rahisi kama kuja kuropoka hapa jukwaani? Hujui unapokuwa umelala na kukoroma usiku kucha kuna watanzania wenzetu wanakuwa wanakesha wanapambana kulinda wanyama wetu?
Narudia kusema, mlinzi wa wanyama wetu ni Maasai sababu Hali wanyama pori.

Majangili mnayahalalisha na kuyapa vibali vya uwindaji Kwa kutumia silaha Kisha wanapakia wanyama wetu hai na kupeleka uarabuni na ulaya!!
 
Duu!
JamiiForums-1659793415.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais mwenyewe kwa kinywa chake anakiri kuna matataizo mengi na hayashughulikiwi ipasavyo hivyo wananchi wanalalamika.
Maana yake Rais anatambua kabisa kuna matatizo na kibaya Mazezeta kama wewe yapo kusifia ujinga tu hayapo kutoa changamoto.
Sasa ona ungekuwa na akili timamu na wenzako mngejitahidi kumsaidia Rais kutokomeza matandao wa Wizi wa fedha za Umma huko kwenu Mbeya.
Rais angetamani kila siku wajitokeze watu wamuambie changamoto na sio kumsifia wakati ujinga upo.
Majitu kama wewe ndio sumu kwa Taifa hili, mnejikita kuongea ukweli mngemsaidia Rais, Sasa mnajisikiaje mmaposema nchi nzima imejaa furaha na vicheko halafu Rais akaja aka akasema mambo yapo hovyo?
Mangu awaadhibu nyinyi watu kwa unafiki wenu
 
Narudia kusema, mlinzi wa wanyama wetu ni Maasai sababu Hali wanyama pori.

Majangili mnayahalalisha na kuyapa vibali vya uwindaji Kwa kutumia silaha Kisha wanapakia wanyama wetu hai na kupeleka uarabuni na ulaya!!
Acha kuropoka ndugu yangu pasipo ushahidi .Embu weka hapa ushahidi wa kinyaraka wa hivyo vibali vinavyotolewa na serikali yetu kuwapa majangili
 
Acha kuropoka ndugu yangu pasipo ushahidi .Embu weka hapa ushahidi wa kinyaraka wa hivyo vibali vinavyotolewa na serikali yetu kuwapa majangili
Wanaosafirisha wanyama wetu hai Kwa vibali Rasmi ni majangili wanaolindwa!!

Wewe hullioni Hilo?
 
Jamani hivi mnataka wote wamchukie keasababu wewe na ndugu zako mnamchukia!! Vhuki zipo kila mahali hats wewe kuna watu wanakuchukia lakini pia wapo wanaokukubali. Usilazimishe hii dunia huwezi kukubalika na watu wote.
 
Wanaosafirisha wanyama wetu hai Kwa vibali Rasmi ni majangili wanaolindwa!!

Wewe hullioni Hilo?
Hakuna bangili anayeweza kulindwa na Serikali yetu.kama unao ushahidi weka hapa mtu aliyelindwa kwa kufanya Vitendo vya ujangili au kufadhili au kuwezesha au kuchochea ujangili.weka ushahidi na siyo kuandika blaa blaa tu.
 
Back
Top Bottom