Kuelekea 2025 Rais Samia anasepa na kijiji kwa Kijiji Morogoro

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

mapessa

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
654
1,158
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. Ziara hii ni muendelezo wa ziara zake za kutembelea mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa ajili ya kuzindua miradi ya kimkakati, kuhamasisha maendeleo na kitatua kero za wananchi.

Wakati Rais akifanya ziara mbalimbali za nje ya Nchi, kuna wapinzani walikua wanapiga kelele kuwa rais hatulii nyumbani.

Sasa mwenye nyumba karudi wamekaa kimya huko wakiwa hawaamini kinachoendelea.

Wapinzani wamefuta kabisa ziara zao za mikoani na kuhamishia kampeni zao mitandaoni huko wakilazimisha ajenda zisizo na mashiko kwa mustakabali wa wananchi.

Wakati wapinzani wakihangaika na nani awe kiongozi wa TLS, Rais amekua anafanya mambo ya kuwagusa wananchi moja kwa moja.

Mfano, leo akiwa Morogoro, Rais Samia Suluhu Hassan amezindua kampeni ya "Tutunzane Mvomero".

Kampeni hii inalenga kumaliza migogoro kati ya wafugaji na wakulima. Yani wakati rais anatatua migogoro, wapinzani wao wana hamasisha migogoro mitandaoni. Ajabu sana.

Rais Samia amefungua barabara ya Rudewa-Kilosa yenye urefu wa kilomita 25. Barabara hii itaongeza urahisi wa usafiri na usafirishaji wa bidhaa. Wakati Rais anajenga mabarabara ili kuwaunganisha Watanzania, wapinzani watatumia barabara hizo hizo kupita na kujaribu kuleta utengano kati ya Watanzania.

Rais anajenga huko wengine wakijaribu bila mafanikio kubomoa.

Rais Samia ameendeleza juhudi za kuimarisha sekta ya sukari kwa kuzindua bwawa la kubwa Afrika Mashariki la kiwanda cha Sukari Mtibwa.

Mradi huu utasaidia kupunguza utegemezi wa sukari kutoka nje na kuongeza ajira. Wakati Rais Samia anajaribu kupunguza utegemezi, wapinzani wanaendelea kuombea miradi mbalimbali ya kimkakati ifeli ili Watanzania na nchi iendelee kuwa tegemezi.

Kinacho tia moyo ni kwamba wakati wao kwenye majukwaa yao wanashindwa kukusanya hata watu mia, ziara za Rais Samia zinaleta pamoja ma-elfu na ma-elfu ya Watanzania wanaofika kumuona rais wao na wengine mamilioni wakifuatilia kupitia vyombo vya habari.

Vijana wa Gen Z wa Kitanzania wanaita hii "Kusepa na Kijiji". Mnataka ushahidi? Linganisheni tu picha za ziara ya rais na picha za makongamano ya mabwana wale.

PIA SOMA
- Rais Samia anatarajiwa kufanya ziara ya siku sita mkoani Morogoro mwanzoni mwa mwezi Agosti

71a17783-0a63-4e20-81b5-6989030b5919.jpeg
3865a6aa-7a41-484e-b5e5-fa2b2ad3aec7.jpeg
f6067ed8-63c7-4b97-ab98-9bad114c8e28.jpeg
4ed13a5b-5da9-416c-b6cf-5ff2f1e8e2e5.jpeg
ef9a46b6-69db-4797-9384-1df13e098b39.jpeg
68133758-28ac-4179-a21e-c804d99a08bd.jpeg
cba20c15-9f9f-4fbd-bb1e-ad5273b5ed88.jpeg
 
Mama anaendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania.watanzania wanaendelea kumlaki na kumpokea kwa maelfu kwa maelfu kila anapopita.kwa hakika Rais Samia ni mpango wa Mungu Mwenyewe.
 
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. Ziara hii ni muendelezo wa ziara zake za kutembelea mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa ajili ya kuzindua miradi ya kimkakati, kuhamasisha maendeleo na kitatua kero za wananchi.
Nilidhani anapita kusikiliza na kutatua kero za wananchi
 
Wakati Rais anajenga mabarabara ili kuwaunganisha Watanzania, wapinzani watatumia barabara hizo hizo kupita na kujaribu kuleta utengano kati ya Watanzania.
Hapa ndipo panaakisi ufinyu wa kufikiri, tambua kuwa wanaosoma hizi habari siyo wajinga, fedha zinazojenga barabara ni za kodi za watanzania, kama ni za Rais basi afute tozo zote ajenge kwa mshara wake ndipo mje na thread za hivi
 
Back
Top Bottom