Rais Samia anapendwa sana Mitaani na mamilioni ya Watanzania

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,262
9,714
Ndugu zangu watanzania,

Nilikuwa kimya kidogo nikiendelea na shughuli zangu za utafutaji maeneo mbalimbali yaliyoniwezesha kuonana na watanzania wa makundi yote. Nimeingia na kuendelea kufika ndani kabisa vijijini,nimepita miji midogo midogo na maeneo mbalimbali yaliyo na mikusanyiko ya watanzania.

Kwa hakika mh Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania, Nembo ya Taifa, mama mchapa kazi, mvumilivu, mwenye misimamo thabiti, asiye yumba wala kuyumbishwa, mwenye Dhamira na mapenzi ya dhati kwa Taifa letu, aliyelibeba Taifa katika kifua na moyo wake, mwenye maono na dira inayoeleweka na aliyeliheshimisha Taifa letu mama Samia suluhu Hassani anapendwa sanaa tena sana na mamilioni ya Watanzania, Anakubalika sana mama yetu, Anaungwa mkono na Watanzania wengi sana, anaombewa sana makanisani, misikitini na kila mmoja kwa imani yake.

Watanzania wengi sana wanafunga na kuomba kwa ajili ya Rais Samia,Wanaomba ili mwenyezi Mungu aendelee kumjalia afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania, wanaomba na kufunga ili mwenyezi Mungu aendelee kumtangulia katika utumishi wake wa kuwatumikia Watanzania, wanafunga na kuomba ili mwenyezi Mungu Aendelee kulipatia Taifa letu Neema na baraka katika kila eneo na kutukinga na lolote linaloweza kutuvuruga kama Taifa.

Katika kufuatilia na kuzungumza nao, Watanzania wanasema wanampenda na kumuunga mkono Rais wetu mpendwa kutokana na uongozi wa Rais wetu katika miaka yake hii amefanikiwa kugusa maisha ya mamilioni ya Watanzania.

Amegusa maisha ya Watanzania wanyonge wakipato cha chini mpaka wa juu kabisa, amefanya juhudi kubwa sana kuhakikisha kuwa watanzania wanyonge wanawezeshwa kisera na kibajeti kuinuka kiuchumi na kuupiga teke umaskini, amewekeza mabilioni kwa mabilioni ya pesa kuhakikisha kuwa analeta Tabasamu, matumaini na furaha katika mioyo ya watanzania wanyonge.

Ameendelea kuhakikisha wa kipato cha juu wanaendelea kufanya vyema ili wachangie katika kutoa na kutengeneza fursa za ajira, kulipa kodi na kukuza mitaji yao kwa kuweka mazingira mazuri ya kiuwekezaji na kibiashara.

Katu na kamwe Rais wetu mpendwa hajawahi kuwa na mawazo ya kumuinua mnyonge kwa kumshusha aliye juu, siku zote Rais wetu mpendwa amekuwa mwenye kutengeneza mazingira wezeshi kwa kila mtu mwenye kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa kuinuka kiuchumi, amefanya na kuweka mazingira mazuri kwa kila mtu kufaidika na jasho lake, kila mwenye kufanya kazi na kujituma anayo nafasi ya kupiga hatua kimaendeleo.

Hii ndio sababu Rais Samia kupendwa na mamilioni ya Watanzania, huwezi ukakuta mitaani na vijijini watanzania wakisema vibaya juu ya Rais Samia, Hakuna mwenye chuki na Rais Samia, kila mmoja anasema Rais Samia ni nuru ya Watanzania, ni nyota iletayo matumaini, ni daraja la matumaini kuwavusha wanyonge, ni njia kwa wenye kuhitaji kutimiza ndoto zao, ni chemchemi kwa wenye kiu ya maendeleo, ni faraja kwa watanzania, ni Taa katikati ya Giza.

Rais Samia anaendelea kuishi katika mioyo ya Watanzania, mamilioni ya Watanzania wanaendelea kupeperusha jinaa la mama yetu mioyoni mwao, wanaendelea kuandamana mioyoni mwao pasipo kibali wala kikomo kumuunga mkono mama yetu Rais Samia. Amefanya makubwa ya kuacha alama katika maisha ya wengi. Ndio maana anaendelea kutetewa na kulindwa kimaombi na mamilioni ya Watanzania.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

The struggle is real, kweli mtaani kugumu.

Wazungu husema 'the end justifies the means'. Endelea na jitihada mwamba, mwisho wa siku kinachoangaliwa ni matokeo ya mwisho ya jitihada zako. Watakuona tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom