Rais Samia anadanganywa sana Mapinduzi ya Kilimo ya Bashe

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,574
Reaction score
8,907
Inasikitisha sana hii nchi mtu anaweza Danganya hadi Maproff na wakaaa kimya ila ukweli wanaujua.

Bashe anazungumzia Block za Kilimo mara mapinduzi ya kilimo, hii ni hadaaa kubwa sana.

Huwezi zungumzia Mapinduzi ya Kilimo bila kuanza kuhakikisha vitu vifuatavyo;

1. Mapinduzi ya Elimu ya Kilimo- Kwa sasa kuna uhaba wa walimu wa Agricultire zile shule za michepuo ya kilimo zimebakia jina tu hakuna tena ile nguvu ya shule za Kilimo kama ilivyo kuwa enzi zile.

Vyuo vya kilimo- Tembelea vyuo hivi ya kilimo unaweza lia, vyuo ni tamabakia magofu tupu pale, Majengo choka mbaya, Wakufunzi wenyewe ni walisha kata tamaa, hakuna vifaa ya kujifunza na kufundishia.

Kama hujawekeza kwenye Elimu ya Kilimo, hayo pinduzi yanaletwa na nani?

2. Utafiti- Still bado hakuna uwekezaji wa maana kwenye utafiti wa mambo ya kikimo, taasisi za utafiti zina pesa tu ya kawaida.

3. Mapinduzi ya viwanda vya Kilimo ambavyo sana vitasababishwa na mapinduzi ya elimu za kilimo
Dhana za kilimo tunazo tumia asilimia 100 tunaagiza nje, wapi ile ZZK Mbeya? Si waliaha badilisha kuwa kiwanda cha Pombe?

4. Huwezi force watu wote vijana wakusanyike Dodoma na Kigoma kulima mazo mnayo taka nyie,

Kuna Kijana anataka kuwekeza labda kulima Tangawizi yuko Same huyu hana namna anapaswa kwenda kulima alzeti Dodoma kwenye zile Block.

Kijana yuko Rombo anataka kuwekeza zaidi kwenye kilimo cha migomba na yeye aende Dodoma?

Kijana yuko Rungwe pia huko Mbeya anataka kulima ndizi vipi aende Dododma.kwenye Block?

5. Je taasisi zote za Serikali zimeandaliwa kusapoti kilomo? Kuna Policy zimeandaliwa na wanapaswa kusaini? Ili basi wasapoti mapinduzi ya kilimo au ni hadaaa?

Vipi Policy ya TANESCO kuhusu kusapoti kililimo inasemaje?

Vipi policy ya TBS kwenye kukuza kilimo?
Vipi Policy ya mamlaka my be za maji safi na maji taka?

Vipi Policy ya Jeshi la Police hasa Trafiki, je wana mwongozo wa kusaidia kilimo hasa zile swagwa zao za kusimamisha simamisja magari hata yanayo wahisha mazao ya kilomo sokoni?

Commercial Bank kuna sehemu wanabanwa ili wasapoti Kilimo? au ni uamuzi wao?

Kama policy zipo je zisipo tekelezwa kuna watu wanawajibishwa?

Mapinduzi ya kilimo sio aina hio tunayo aminishwa na Bashe hapo, bado sana
 
Pamoja na mapungufu kidogo ya bashe,bado mimi ndio naona ndiye waziri bora wa kulimo toka tupate uhuru,na atakipeleka kilimo katika viwango vikubwa sana.
Huu ni ukweli uliowazi anadhamira njema ila tatizo wataalamu wetu wana read minds za wanasiasa badala ya kutoa technical assistance so anakuwa mislead kwakua wakati mwingine wataalamu wanatoa options ambazo hazipo viable wala si sustainable.

Pengine ni incapacity aliyoiona mstaafu CAG wetu Prof. Assad, kwenye technical personnel yetu, then kama nchi tunatakiwa kuwa makini kuliko kumwingiza Mh. Rais na wananchi kwenye crisis za mara kwa mara kwakupeleka models ambazo hazijahakikiwa at action research levels kujua pros and cos zake kwenye country level; implementation kama vile tozo zilivyo sababisha sintofahamu mpaka leo.
 
Block farming ilitakiwa uangalie eneo fulani linakubali mtama, wezesha watu wa huko waime huo mtama, na eneo fulani linakubali vitunguu wezesha huko watu watalima kwa wingi, shida za kuingiza siasa kwenye mambo ya msingi ni hatari sana
 
Inasikitisha sana hii nchi mtu anaweza Danganya hadi Maproff na wakaaa kimya ila ukweli wanaujua.

Bashe anazungumzia Block za Kilimo mara mapinduzi ya kilimo, hii ni hadaaa kubwa sana.

Huwezi zungumzia Mapinduzi ya Kilimo bila kuanza kuhakikisha vitu vifuatavyo;

1. Mapinduzi ya Elimu ya Kilimo- Kwa sasa kuna uhaba wa walimu wa Agricultire zile shule za michepuo ya kilimo zimebakia jina tu hakuna tena ile nguvu ya shule za Kilimo kama ilivyo kuwa enzi zile.

Vyuo vya kilimo- Tembelea vyuo hivi ya kilimo unaweza lia, vyuo ni tamabakia magofu tupu pale, Majengo choka mbaya, Wakufunzi wenyewe ni walisha kata tamaa, hakuna vifaa ya kujifunza na kufundishia.

Kama hujawekeza kwenye Elimu ya Kilimo, hayo pinduzi yanaletwa na nani?

2. Utafiti- Still bado hakuna uwekezaji wa maana kwenye utafiti wa mambo ya kikimo, taasisi za utafiti zina pesa tu ya kawaida.

3. Mapinduzi ya viwanda vya Kilimo ambavyo sana vitasababishwa na mapinduzi ya elimu za kilimo
Dhana za kilimo tunazo tumia asilimia 100 tunaagiza nje, wapi ile ZZK Mbeya? Si waliaha badilisha kuwa kiwanda cha Pombe?

4. Huwezi force watu wote vijana wakusanyike Dodoma na Kigoma kulima mazo mnayo taka nyie,

Kuna Kijana anataka kuwekeza labda kulima Tangawizi yuko Same huyu hana namna anapaswa kwenda kulima alzeti Dodoma kwenye zile Block.

Kijana yuko Rombo anataka kuwekeza zaidi kwenye kilimo cha migomba na yeye aende Dodoma?

Kijana yuko Rungwe pia huko Mbeya anataka kulima ndizi vipi aende Dododma.kwenye Block?

5. Je taasisi zote za Serikali zimeandaliwa kusapoti kilomo? Kuna Policy zimeandaliwa na wanapaswa kusaini? Ili basi wasapoti mapinduzi ya kilimo au ni hadaaa?

Vipi Policy ya TANESCO kuhusu kusapoti kililimo inasemaje?

Vipi policy ya TBS kwenye kukuza kilimo?
Vipi Policy ya mamlaka my be za maji safi na maji taka?

Vipi Policy ya Jeshi la Police hasa Trafiki, je wana mwongozo wa kusaidia kilimo hasa zile swagwa zao za kusimamisha simamisja magari hata yanayo wahisha mazao ya kilomo sokoni?

Commercial Bank kuna sehemu wanabanwa ili wasapoti Kilimo? au ni uamuzi wao?

Kama policy zipo je zisipo tekelezwa kuna watu wanawajibishwa?

Mapinduzi ya kilimo sio aina hio tunayo aminishwa na Bashe hapo, bado sana
Pamoja na mapungufu yaliyopo bado ni mwanzo mzuri.
 
Pamoja na mapungufu kidogo ya Bashe, bado mimi ndio naona ndiye waziri bora wa kulimo toka tupate uhuru,na atakipeleka kilimo katika viwango vikubwa sana.
Lakini awe msikivu anapokosolewa sio awe anawasikiliza Chawa zaidi maana wale wapo kwa maslahi yao sio ya Nchi !!
 
Pamoja na mapungufu kidogo ya Bashe, bado mimi ndio naona ndiye waziri bora wa kulimo toka tupate uhuru,na atakipeleka kilimo katika viwango vikubwa sana.
Viwango gani bila kuandaa misingi imara kuhusu kilimo?
 
Bashe akiendelea kuwa Waziri wa Kilimo, mchele na mahindi yote yatasombelewa na kupelekwa Somalia na Kenya kila mwaka.

Wakati wa mavuno, atawaleta ndugu zake wafanyabiashara kuja kununua mazao ya wakulima kwa bei chee kwa kisingizio cha soko huria, na mwisho wa siku kuendelea kutusababishia mfumuko wa bei katika bidhaa za chakula.
 
Hizi program zimefanywa sana na Makanisa ya Kiroho kuanzia enzi za Kilimo Kwanza ya Kikwete

Askofu Gamanywa na wengine walifanya sana hii ikafeli
Kuna mambo ya msingi wanamficha "Mama" kwa maslahi binafsi! Huwezi ukataka kuijenga kesho huku unajisahaulisha kuwa unatakiwa kula leo na tunaambiwa vijana ni Taifa la leo sio kesho.
 
Back
Top Bottom