Inasikitisha sana hii nchi mtu anaweza Danganya hadi Maproff na wakaaa kimya ila ukweli wanaujua.
Bashe anazungumzia Block za Kilimo mara mapinduzi ya kilimo, hii ni hadaaa kubwa sana.
Huwezi zungumzia Mapinduzi ya Kilimo bila kuanza kuhakikisha vitu vifuatavyo;
1. Mapinduzi ya Elimu ya Kilimo- Kwa sasa kuna uhaba wa walimu wa Agricultire zile shule za michepuo ya kilimo zimebakia jina tu hakuna tena ile nguvu ya shule za Kilimo kama ilivyo kuwa enzi zile.
Vyuo vya kilimo- Tembelea vyuo hivi ya kilimo unaweza lia, vyuo ni tamabakia magofu tupu pale, Majengo choka mbaya, Wakufunzi wenyewe ni walisha kata tamaa, hakuna vifaa ya kujifunza na kufundishia.
Kama hujawekeza kwenye Elimu ya Kilimo, hayo pinduzi yanaletwa na nani?
2. Utafiti- Still bado hakuna uwekezaji wa maana kwenye utafiti wa mambo ya kikimo, taasisi za utafiti zina pesa tu ya kawaida.
3. Mapinduzi ya viwanda vya Kilimo ambavyo sana vitasababishwa na mapinduzi ya elimu za kilimo
Dhana za kilimo tunazo tumia asilimia 100 tunaagiza nje, wapi ile ZZK Mbeya? Si waliaha badilisha kuwa kiwanda cha Pombe?
4. Huwezi force watu wote vijana wakusanyike Dodoma na Kigoma kulima mazo mnayo taka nyie,
Kuna Kijana anataka kuwekeza labda kulima Tangawizi yuko Same huyu hana namna anapaswa kwenda kulima alzeti Dodoma kwenye zile Block.
Kijana yuko Rombo anataka kuwekeza zaidi kwenye kilimo cha migomba na yeye aende Dodoma?
Kijana yuko Rungwe pia huko Mbeya anataka kulima ndizi vipi aende Dododma.kwenye Block?
5. Je taasisi zote za Serikali zimeandaliwa kusapoti kilomo? Kuna Policy zimeandaliwa na wanapaswa kusaini? Ili basi wasapoti mapinduzi ya kilimo au ni hadaaa?
Vipi Policy ya TANESCO kuhusu kusapoti kililimo inasemaje?
Vipi policy ya TBS kwenye kukuza kilimo?
Vipi Policy ya mamlaka my be za maji safi na maji taka?
Vipi Policy ya Jeshi la Police hasa Trafiki, je wana mwongozo wa kusaidia kilimo hasa zile swagwa zao za kusimamisha simamisja magari hata yanayo wahisha mazao ya kilomo sokoni?
Commercial Bank kuna sehemu wanabanwa ili wasapoti Kilimo? au ni uamuzi wao?
Kama policy zipo je zisipo tekelezwa kuna watu wanawajibishwa?
Mapinduzi ya kilimo sio aina hio tunayo aminishwa na Bashe hapo, bado sana