Rais Samia amdhibiti Bashe, mradi wa Kilimo kwa Vijana ni kichaka cha upotevu wa pesa ya Umma

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,547
41,060
Daima nimemsifu Bashe kwa msimamo wake wa kutokuzuia wakulima kuuza mazao yao mahali popote, iwe ndani ya nchi au nje ya nchi. Kwenye hilo mpaka sasa namwunga mkono.

Lakini taarifa kwamba Serikali imetumia milioni 16 kwa kila ekari 1 kusafisha shamba/kuandaa shamba, ni upotevu wa pesa wa hali ya juu.

Namwomba Rais ateue kamati ndogo ya watu wachache, au amwombe CAG achunguze ili kujua gharama halisia za kuandaa shamba ekari 1, na kisha kuwapata wahusika wote waliohusika kwenye wizi huu wa pesa ya wananchi.

Pamoja na mambo mengine, nnafanya pia shughuli za kilimo. Nina ekari 657. Nazifahamu gharama halisi kwenye kilimo. Japo kuna utofauti mdogo wa gharama unaotegemea mahali shamba lilipo lakini kiuhalisia hakuna utofauti mkubwa katika gharama.

Uandaaji huu wa shamba unahusisha vitu gani hadi kufikia gharama hiyo?

Kwa ujumla wazo la kuiinua na kuiendeleza sekta ya kilimo, hakika ni wazo zuri sana lakini approach ni completely wrong. Na mpango mzima hautafanikiwa. Pesa hii yote inayopelekwa huko itapotea.

Mpango wa kuinua sekta ya kilimo ulistahili kwa kuwasaidia wale ambao tayari wanafanya shughuli za kilimo huko vijijini. Hao tayari kwanza wanakipenda kilimo, wana mipango, wana elimu ya kilimo iliyotokana na wao kufanya kilimo, na hivyo Serikali ilistahili kuwasaidia kwenye maeneo yale ambayo wao wakulima tayari wanayatambua kama kikwazo kwa wao kufanya kilimo kwa ufanisi. Mafanikio ya wakulima hao, yangewavuta wengine wengi kuingia kwenye kilimo.

Huu mpango wa kuwakokota vijana wa mjini kuwapeleka kwenye kilimo kwa ahadi nyingi za kusaidiwa, wengi watajitokeza, lakini baada ya mwaka mmoja, watabakia si zaidi ya 50% tu kwenye kilimo. Baada ya miaka 3, watakaobakia wakifanya kilimo hawatazidi 25%. Na hao watakaobakia kwenye kilimo, watakaofanikiwa kufanya kilimo chenye faida hawatazidi 10%.

Huu mradi, unaweza kuwa sawa na ule wa 'mabilioni ya Kikwete'; ambao uliishia kwenye upotevu wa mabilioni ya pesa.
 
Uko sahihi
 
Amesema mashamba yatawekewa hadi umeme na barabara, udomgo utampimwa .a kuwekewa irrigation system...umeconsider hizo Gharama?
Je, yote hayo ni lazima? Huo umeme utawekwa kwa kila ekari? Kwaajili ya nini? Barabara itawekwa kwa kila barabara au kwa kila block?

Kwa mtu anayekijua kilimo, huwezi kuingia kwenye gharama kubwa sana kwa wakati mmoja. Unatakiwa kwenda hatua kwa hatua huku ukipima mafanikio ya kila hatua. La sivyo, unaweza kutumia matrilioni ya pesa halafu baadaye unakuja kushtuka hakuna tija iliyotarajiwa.
 
Unaweza kukuta yeye hapo ana ekari 1000 Bashe ni mtu wa deal sana. Najua atakuja kujibu
Nimepita Nzega, jimboni kwa Bashe. Kuna mradi wa kilimo cha umwagiliaji wameuandaa, kwa kutumia maji ya bwawa la Kilimi. Maji yapo lakini eneo walililotenga halifai kabisa, na hakuna mtu atakayekwenda kulima eneo hilo.

Tayari mamia ya mamilioni yametumika kujenga uzio kuzunguka eneo hilo lisilofaa kwa kilimo. Siyo ajabu, hayo ndiyo yaliyopo maeneo mengi.
 
Je, yote hayo ni lazima? Huo umeme utawekwa kwa kila ekari? Kwaajili ya nini? Barabara itawekwa kwa kila barabara au kwa kila block?

Kwa mtu anayekijua kilimo, huwezi kuingia kwenye gharama kubwa sana kwa wakati mmoja. Unatakiwa kwenda hatua kwa hatua huku ukipima mafanikio ya kila hatua. La sivyo, unaweza kutumia matrilioni ya pesa halafu baadaye unakuja kushtuka hakuna tija iliyotarajiwa.
Umeme muhimu kwa ajili ya value addition na shughuli zingine
 
Daima nimemsifu Bashe kwa msimamo wake wa kutokuzuia wakulima kuuza mazao yao mahali popote, iwe ndani ya nchi au nje ya nchi. Kwenye hilo mpaka sasa namwunga mkono.

Lakini taarifa kwamba Serikali imetumia milioni 16 kwa kila ekari 1 kusafisha shamba/kuandaa shamba, ni upotevu wa pesa wa hali ya juu.

Namwomba Rais ateue kamati ndogo ya watu wachache, au amwombe CAG achunguze ili kujua gharama halisia za kuandaa shamba ekari 1, na kisha kuwapata wahusika wote waliohusika kwenye wizi huu wa pesa ya wananchi.

Pamoja na mambo mengine, nnafanya pia shughuli za kilimo. Nina ekari 657. Nazifahamu gharama halisi kwenye kilimo. Japo kuna utofauti mdogo wa gharama unaotegemea mahali shamba lilipo lakini kiuhalisia hakuna utofauti mkubwa katika gharama.

Uandaaji huu wa shamba unahusisha vitu gani hadi kufikia gharama hiyo?

Kwa ujumla wazo la kuiinua na kuiendeleza sekta ya kilimo, hakika ni wazo zuri sana lakini approach ni completely wrong. Na mpango mzima hautafanikiwa. Pesa hii yote inayopelekwa huko itapotea.

Mpango wa kuinua sekta ya kilimo ulistahili kwa kuwasaidia wale ambao tayari wanafanya shughuli za kilimo huko vijijini. Hao tayari kwanza wanakipenda kilimo, wana mipango, wana elimu ya kilimo iliyotokana na wao kufanya kilimo, na hivyo Serikali ilistahili kuwasaidia kwenye maeneo yale ambayo wao wakulima tayari wanayatambua kama kikwazo kwa wao kufanya kilimo kwa ufanisi. Mafanikio ya wakulima hao, yangewavuta wengine wengi kuingia kwenye kilimo.

Huu mpango wa kuwakokota vijana wa mjini kuwapeleka kwenye kilimo kwa ahadi nyingi za kusaidiwa, wengi watajitokeza, lakini baada ya mwaka mmoja, watabakia si zaidi ya 50% tu kwenye kilimo. Baada ya miaka 3, watakaobakia wakifanya kilimo hawatazidi 25%. Na hao watakaobakia kwenye kilimo, watakaofanikiwa kufanya kilimo chenye faida hawatazidi 10%.

Huu mradi, unaweza kuwa sawa na ule wa 'mabilioni ya Kikwete'; ambao uliishia kwenye upotevu wa mabilioni ya pesa.
Uko sahihi kabisa. Kwa style anayokwenda nayo Bashe upigaji utakuwa nje nje.
Hiyo mikopo ingetolewa kwa wakulima ambao tayari ni experienced kwa kuwa wanajua challenge halisi.
 
Umeme muhimu kwa ajili ya value addition na shughuli zingine
Usiende theoretically. Wewe unaenda kuandaa shamba, ni valye addition gani utaiongeza wakati unaanzisha shamba au unapoanza kulima?

Umeme unaweza kupelekwa kwenye eneo la mashamba, lakini huwezi kuupeleka kwa kila ekari. Eneo la mashamba umeme unaweza kuhitajika kwenye eneo la makazi na kuendeshea pump za umwagiliaji, lakini hutaqeka kwa kila ekari. Unaweza kuuhitaji umeme pia kwaajili ya uhifadhi wa mazao, lakini hayo yanakuja baada ya kuona maendeleo ya mazao.
 
Back
Top Bottom