Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Akizindua Usafirishaji wa Mizigo kwa SGR Kwala Pwani, leo tarehe 31 Julai, 2025.
Update
Sehemu ya Hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan
Ili kuimarisha usafiri na usafirishaji wa mizigo serikali imewekeza takribani Ths. Bilioni 330 na milioni 200 kwa ajili ya ununuzi wa mabehewa 1430 ya mizigo ya SGR. Hivyo kuwataka wizara ya uchukuzi na TRC wahakikishe kuwa mabehewa hayo yatatumika ipasavyo kwani shughuli hizo ni za biashara.
Amehimizia pia kushirikishwa kwa wadau wa sekta binafsi wa ndani na nje ya nchi ili waweze kuchangamkkia fursa ya kuchangamkia miundombinu ya reli ya kusafirisha abiria na mizigo kwa kununua vichwa vya treni na mabehewa yao wenyewe.
Waziri wa Viwanda (Dkt. Selemani Jafo)
Amesema eneo la viwanda lililozinduliwa la Kwala industrial park lina hekta zaidi ya 1000, ambazo litapelekea zaidi ya viwanda 200 vitajengwa hapo ambapo vitakuwa na jumla ya uwekezaji wa Dola Bilioni 3 ambayo itazalisha jumla ya bidhaa zitakazokuwa na thamani ya Dola Bilioni 6.
Kati ya Dola hizo, Dola bilioni 2 zitatokana na export wakati dola Bilioni 4 zitakuwa kwa ajili ya matumizi ya ndani. Mradi huo una matarajio ya kutengeneza jumla ya 250,000 zisizo za moja kwa moja na ajira 50,000 zitakuwa ni za moja kwa moja.
Waziri wa Miundombinu Burundi (Captian Dieudonne Dukundane)
Ameeleza kuwa wapo tayari kuunganisha reli ya SGR kwenda DRC na hivyo kuifanya Burundi na DRC pamoja na Tanzania kuwa nchi za mfano.
Waziri wa uchukuzi (Prof. Makame Mbarawa)
Ameeleza kuwa TRC itaongeza idadi ya treni za mabehewa 30 kwa lengo la kubeba mizigo ya tani 210,000 hadi kufikia kiwango cha juu kilichosanifiwa.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne (Jakaya kikwete)
Amesema kuwa uwekezaji huo utakuw akichocheo kikubwa cha uchumi wa eneo hilo. Amesema kuwa maeneo ambayo yamepimwa katika maeneo ya huko yote yameshakwisha watu wamechukua.
==================================
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi Julai 31, 2025 amekagua na kuzindua rasmi Bandari Kavu ya Kwala Mkoani Pwani pamoja na kupokea mabehewa Mapya na yaliyokarabatiwa ya reli ya kati Meter-Gauge Railway (MGR).
Miradi yote hiyo ni kielelezo na uthibitisho wa dhahiri wa maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Tanzania inapiga hatua kubwa za kimaendeleo kwa kutumia fursa zilizopo, ikiwemo kuzungukwa na nchi jirani ambazo zinategemea Bandari za Tanzania kama lango lao kuu la Biashara ikiwemo Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambazo zimetengewa maeneo maalum ya kuhifadhi mizigo katika bandari hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Bw. Plasduce Mbossa amemueleza Rais Samia kuwa Bandari hiyo Kavu ya Kwale inatarajiwa kupunguza muda na gharama za usafirishaji wa mizigo pamoja na kupunguza msongamano wa magari kwenye Jiji la Dar Es Salaam.
Mbossa pia ameeleza manufaa mengine kuwa ni pamoja na kuchochea uwekezaji na uanzishaji wa Viwanda katika Ukanda wa Kwala pamoja na kuongeza mapato ya serikali kupitia huduma ya Bandari, akisema eneo zima la bandari hiyo linafikia Hekta 502, mara tano zaidi ya bandari ya Dar Es Salaam huku pia bandari hiyo ikiunganishwa na Reli ya Kisasa ya SGR, bandari ya Bagamoyo, Reli ya Kati na Reli ya TAZARA.