GE2025 Rais Samia aendelea kuthibitisha kwamba anawajali wakulima, atoa onyo kwa wawekezaji wa zao la chai Rungwe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
291
Reaction score
281
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiwa wilayani Rungwe mkoani Mbeya, amesisitiza dhamira ya serikali yake kulinda maslahi ya wakulima kwa kuhakikisha rasilimali muhimu kama ardhi na mazao ya kimkakati yanabaki kwa manufaa ya wananchi.

Akizungumzia uwekezaji katika zao la chai, Rais Samia alisema baadhi ya wawekezaji akiwemo kampuni ya Mohamed Enterprises walishindwa kufikia matarajio ya serikali ya kuwa msaada kwa wananchi baada ya kupewa nafasi ya kuwekeza. Amesema licha ya kupewa fursa ya kuendeleza viwanda vya chai, wawekezaji hao wameshindwa kuviendesha na pia wanadaiwa mishahara na stahiki za wafanyakazi wao.

Rais Samia alisisitiza kuwa serikali haiwezi kukubali kuona ardhi na viwanda vinakaa bila tija huku wakulima wakihangaika, na kwamba msimamo wa serikali ni kuhakikisha rasilimali za taifa zinatumika kwa maslahi ya wananchi, si kwa faida binafsi za wachache.

Aidha, Rais Samia amevitaka viwanda hivyo kulipa mishahara ya wafanyakazi wake.
 
Attachments

  • rungwe6.png
    rungwe6.png
    7.3 MB · Views: 18
  • uyole3.png
    uyole3.png
    3.2 MB · Views: 14

Screenshot_20250901-172332~2.png
 
Mama amefunga barabara ya mbeya haipitiki malori yamezuiliwa Hadi amalize kuhutubia
 
Attachments

  • VID-20250905-WA0046.mp4
    5.8 MB
Back
Top Bottom