Rais Samia achana na kuikumbatia CCM, fanya kazi zenye Maslahi mapana kwa Watanzania

Watanzania vigeugeu sana, mara hii mama kashakuwa dhaifu
Wengi wao hao ni wale MATAGA FC!!yaani siku 50, tu ndio ushushe lawama zote hizo?, si bora hata huyu anakubali madhaifu, na kuwa tayari kuyarekebisha??yule aliyekuwa kila kitu anajua yeye miaka 5 amefanya nini?kubwa?hata leo hajaongeza mishahara lakini watu amewapa matumaini, sasa meko, unaulizia haki yako, UNATISHIWA??
 
Watanzania vigeugeu sana, mara hii mama kashakuwa dhaifu
Tunahitaji katiba mpya kama nchi kwa sasa, Nchi ngumu sana hii kuongoza kwa sasa, Mtupoli kavunja vunja kila kitu, kwa kifupi kaivuruga. Mama salama yake ni katiba mpya tu.
 
Mimi naamini katika swala la muda. Ndio kwanza ana mwezi mmoja tu. Najua watanzania tuliumizwa sana kwa kipindi cha miaka mitano. Lakini je huyu rais ana nguvu kiasi gani kubadilisha maovu ya mtangulizi wake ya miaka mitano ndani ya mwezi mmoja? Tuwe wakweli.
 
Shujaa John Pombe Joseph Magufuli atabaki kuwa rais wa karne, mwamba, jasiri, mbeba maono na mtekelezaji...

Tusimlinganishe Rais Samia Suluhu Hassan na JPM. Sisi tuangalie utekelezwaji miradi na ilani ya kurasa 303

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan

Kazi iendelee
 
Watanzania vigeugeu sana, mara hii mama kashakuwa dhaifu
Tunawachora tu! Nadhani baadhi yetu hapa hatujuhi nini kinatakiwa kifanyika ili Tanzania iwe imara katika nyanja zote huku watanzania wakistawi kimaendeleo halisi ya kiuchumi.

Baadhi yetu tunapelekwa pelekwa na upepo....na kweli upepo unakuja na kupita. Tunabaki kubashiri eti upepo unafuata unatokea kusi ama kaskaz....!! Mleta mada ni mfano mzuri wa baadhi yetu.
 
1. Tunataka katiba mpya nzuri

2. Tunataka mabadilio ya sheria mbovu siyo maagizo ya rais tu, maagizo ni easily reversible

3. Tunataka Ukandamizaji wa kuwa na online Channel youtube uondolewe, kwa nini niilipe serikali hela kwa mimi kuwa na Channel yangu youtube?

4. Tunataka uhuru wa vyombo vya habari
 
Wengi wao hao ni wale MATAGA FC!!yaani siku 50, tu ndio ushushe lawama zote hizo?, si bora hata huyu anakubali madhaifu, na kuwa tayari kuyarekebisha??yule aliyekuwa kila kitu anajua yeye miaka 5 amefanya nini?kubwa?hata leo hajaongeza mishahara lakini watu amewapa matumaini, sasa meko, unaulizia haki yako, UNATISHIWA??
Technically ni mataga?

Utakuwa umeanza kufuatilia siasa kupitia twitter account ya kigogo
 
Mimi naamini katika swala la muda. Ndio kwanza ana mwezi mmoja tu. Najua watanzania tuliumizwa sana kwa kipindi cha miaka mitano. Lakini je huyu rais ana nguvu kiasi gani kubadilisha maovu ya mtangulizi wake ya miaka mitano ndani ya mwezi mmoja? Tuwe wakweli.
Maovu kama yapi?

Kwani Samia kafanya ovu gani?

Na mtachanganyikiwa sana nyie
 
Tunahitaji katiba mpya kama nchi kwa sasa, Nchi ngumu sana hii kuongoza kwa sasa, Mtupoli kavunja vunja kila kitu, kwa kifupi kaivuruga. Mama salama yake ni katiba mpya tu.
naishia kucheka sana. Ngoja ninyamaze. Una wazo jema la katiba ila unambebesha lawama asiyehusika
 
Technically ni mataga?

Utakuwa umeanza kufuatilia siasa kupitia twitter account ya kigogo
Vijana wengi wameshapoteza uwezo kuchanganua kwa akili yao bali wanachanganua kwa mlengo wanaoegemea.......mtu yoyote atakayetoa maoni yanayotofautiana na utashi wake ni adui yake......alafu wakati huo huo ndio wanaopigania demokrasia na uhuru wa kutoa maoni...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom