Rais Samia achana na kuikumbatia CCM, fanya kazi zenye Maslahi mapana kwa Watanzania

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
15,162
2,000
Hakika mimi uwa nasema ukweli bila sisi kama nchi kuacha kuishi ya Uongo uongo hakuna maendelea ambayo tutakuja kupata.

Mama Samia alionekana ni mtu atakaye kuja kufanya mageuzi makubwa lakini nasikitika hakuna kitu chochote mpaka sasa ambacho amefanya.

Kwanza alitoa ahadi ya ukaguzi maalumu BOT ambapo pesa zilichotwa kinyemela mpaka sasa kimya.

Aliagiza kufunguliwa kwa vyombo vyote vya habari mpaka sasa kimya.

Ameleta tume ya walimu wameikataa na yeye kakubali.

Unamtoa mwizi hazina unampeleka viwanda na biashara kwa kuogopa nini?

Haya mambo 4 yanaonyesha kama taifa hatuna kiongozi mwenye msimamo.

Kutokana na picha hii naomba kutoa ushauri kwa mambo yafuatayo

1: Mama aombe msamaha taifa Kwa uharibifu ambao Magufuli aliufanya then.

2: Ahachane na baadhi ya elephant project kama ununzi wa ndege kwa cash uku mishahara ikikushinda kuongeza.

3: Rais aanzishe haraka mchakato wa katiba mpya lasivyo atakwama pakubwa.

4: Rais aongelee swala la Bandari ya bagamoyo ambayo inaonekana ni mradi wa kifisadi kama inawezekana initial contract iwekwe wazi ili Watanzania tuone yaliyomo.

5: Janga la covid19 nalo umepiga kimya mi nasema atakaye ichezea corona itaondoka na yeye.

Nimesikitishwa na Hotuba ya Rais leo kuongelea swala la wafanyakazi wa umma na kuacha wafanyakazi wa sector binafisi ambao ndio wengi zaidi mfano wafanyakazi wa sector binafsi.

Wamekuwa hawaunganishwi na mfuko wa taifa ya bima ya afya kwa lazima.

Wamekuwa hawaunganiswi na mfumo wa pension kwa lazima hivyo waajiri wanakiuka sheria za kazi.

Wamekuwa wanafanya kazi muda mrefu kwa malipo yaleyale yaani mtu analipwa laki 3 kwa mwezi halafu anafanya kazi kwa masaa 12 mpaka 18 kwa siku.

Tena kwa masikitiko malimbikizo ya mishahara yanakuwa makubwa mtu unakuta anadai kwa miezi 2 au 3 nyuma na kwa kulinganisha maisha ya sasa yalivyo magumu je tunawatetea.

Mikataba ya wafanyakazi wa sector binafsi imekuwa haipo wanaopewa ni chini ya 5% ya watu wote wanaofanya kazi sector binafsi hii inafanya watu wafukuzwe hovyo bila kupewa stahiki zao

Wakati yote haya yanafanyika Nchi ina Rais , Makamu, Mawaziri,Wabunge,Wakuu wa mikoa,Wakuu wa wilaya, wakurugenzi, Idara ya usalama wa taifa, polisi, Takukuru, Tume za wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi.

Nchi sasa inaonekana kama mtu anaongozewa na amewekwa Kama rubber stamp.

Usumbufu kwa wachimbaji wadogo umerudi kwa haraka sana why?

Vituo vya Mafuta baadhi hawatumii EFD tena why?

Ongezeko la madawa ya kulevya kwanini yameongezeka kwa haraka why?

Tunaongelea siku 50 tu za utawala wako mambo yamebadilika hivi je ndani ya miaka 5 hali itakuwaje?

Bila kifanya mageuzi makubwa ya kikatiba na kimfumo hakuna pahali mama samia ataenda.

Inawezekana anafanya either kwa kutokuwa na taarifa au anafanya makusudi.

Nchii hii kwanza mkubali ni yetu sote then tukiri tulikosea hapo nyuma kama nchi then hatujachelewa tuanze upya tusimike mifumo imara other wise kila rais atakuja na kuondoka maendeleo ya kweli hakuna.

Jiulize gharama za pesa zilizotumika leo kuwapeleka mwanza Rais, Makamo, waziri mkuu, Mawaziri wote, Wakuu wa mikoa kwenda kupiga polojo halafu kwenda kushusha kodi kutoka 9% kwenda 8%.

Mama samia akiendelea kukumbatia watu waovu ndani ya ccm atakwama pakubwa sana

Tunataka report ya CAG ya ukaguzi maalumu pale BOT.

Ukishindwa utakuwa Rais dhaifu zaidi kuwai kuongoza taifa hili mambo bado usilale.

Achana na kuikumbatia CCM Fanya kazi zenye Maslahi mapana kwa Watanzania.

Katika dharura nyingi:

1. Audit report BOT.
2. Covid 19.
3. Kusafisha genge la wale jamaa bila kumwacha mtu.

Haya yalikuwa ya dharura zaidi.

Mama na auvae ujasiri.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom