Rais Samia aagiza Mahakama itende Haki, baadhi ya wafuasi wa CHADEMA wampongeza

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,976
Baadhi ya wafuasi wa Chadema wameipongeza hatua ya Rais Samia kuitaka mahakama itende haki katika mashauri yanayoletwa mahakamani.

Baadhi ya wafuasi wa Chadema wamepongeza hatua hiyo ya Rais Samia na kusema sasa wana imani kesi za wanachama wao ambazo nyingi ni za kubumba zitapatiwa ufumbuzi wa haraka.
 
Amesema kweli. Sikiliza kwa umakini, kuanzia dakika 7 amelikazia kwa uzuri zaidi...

Na acha tuamini kuwa alimaanisha...

Karibu Freeman Aikael Mbowe uraiani tena...

TanPol imeponzwa na ujinga wa kutoielewa PGO...!!
 
Nimeanza kuhisi kauli za Samia hazina uzito, yeye atasema hivi wasaidizi wake watafanya vile, hana authority inayotakiwa kiongozi wa aina yake awe nayo, hii kauli yake nayo itapita tu, na polisi na mahakama zitaendelea kutumiwa na CCM kwa maslahi yake kama kawaida.
 
Amesema kweli. Sikiliza kwa umakini, kuanzia dakika 7 amelikazia kwa uzuri zaidi...
View attachment 1966040

Na acha tuamini kuwa alimaanisha...

Karibu Freeman Aikael Mbowe uraiani tena...

TanPol imeponzwa na ujinga wa kutoielewa PGO...!!
... maandalizi ya hukumu ya kesi ya kihistoria iliyoko mahakamani. In short ametoa mwelekeo wa hukumu na yeye kujitoa kimtindo!
 
Rais hawezi kuiagiza mahakama, labda kama katoa ushauri...
 
Hapa nakuunga mkono Bi Samia. Hili Swala la ukosekanifu wa haki ni swala Mtambuka, hata adhabu ambayo Mwenyezi Mungu ameiandaa kwa ulimwengu huu na watawala wake ni kwa sababu ya kushindwa, kwa kutokujua au kwa makusudi tu huku wakisukumwa na ulevi wa madaraka kuwapatia haki raia wao.

Kuna maala anaelekeza kwenye maandiko matakatifu ndani ya Biblia, kwamba wakati wa utoaji haki usimuangalie mtu masikini/mnyonge ukampendelea (kwa kumuonea huruma) kwa sababu ya umasikini/unyonge wake na wala usimuangalie tajiri/au mtu mwenye mamlaka ukampendelea kwa sababu ya utajiri wake.

Sasa kwa sababu wewe mwenyewe leo umeonyesha kuielewa vyema hekima hii ya mwenyezi Mungu, ni mategemeo yangu utaitendea haki imani hii iliyo ndani yako.

lakini hofu ya kuondoka madarakani kwa sanduku la kura ikikuzidia na kujikuta unasigina haki za wananchi wako kwa nguvu ya mamlaka uliyonayo kama alivyofanya aliyekutangulia, hakika Mwenyezi Mungu haabudiwi mwa maneno matupu, atakuadhibu.
 
Baadhi ya wafuasi wa Chadema wameipongeza hatua ya Rais Samia kuitaka mahakama itende haki katika mashauri yanayoletwa mahakamani.

Baadhi ya wafuasi wa Chadema wamepongeza hatua hiyo ya Rais Samia na kusema sasa wana imani kesi za wanachama wao ambazo nyingi ni za kubumba zitapatiwa ufumbuzi wa haraka.
Swali fikirishi je wanaotengeneza kesi ni nani mapolisi , mahakama ama vyote kwapamoja
 
Leo anasifiwa kesho mtaanza kulia lia tena kwa matendo yake kimtindo tu Mama anaupiga mwingi hadi raha.
Hata kichaa akiwa Rais wetu, yaani kichaa mla majalalani, akitupatia haki wananchi anaweza kututawala milele. hakuna mtu anamchukia Rais wake au kumlalamikia Rais wake kijinga jinga.

Rais ni kioo cha Taifa.

Wote tungependa Rais wetu afanikiwe katika mambo yake yote.

Lakini akielekea njia ya ubinyaji haki, hatutapiga kelele tu, tutampopowa na mawe pia.
 
Haki ndiyo ustawi wa jamii
 
Back
Top Bottom