Rais Samia aagiza Mahakama itende Haki, baadhi ya wafuasi wa CHADEMA wampongeza

Hata mm ninapata tumaini kwasababu sijawahi kusikia hyt. JPM akitamka neno HAKI na yeye SSH ndiyo leo namsikia akitamka neno hilo.
Hakuna amani ya kweli bila HAKI.

Sent from my A71 using JamiiForums mobile app

Kwa JPM ilikuwa: what you see is what you get. Kwa SSH inabidi tuvute subira kujua ukweli wake.
 
..inawezekana amesoma tu alichoandikiwa ktk hotuba.

..mimi nadhani hakumaanisha, na wala haamini hicho alichokisoma.

..kama mnabisha subirini muone kama mahakama zitaanza kutenda haki ktk nchi hii.
 
Nimeanza kuhisi kauli za Samia hazina uzito, yeye atasema hivi wasaidizi wake watafanya vile, hana authority inayotakiwa kiongozi wa aina yake awe nayo, hii kauli yake nayo itapita tu, na polisi na mahakama zitaendelea kutumiwa na CCM kwa maslahi yake kama kawaida.
Ni wangapi wameachiwa since kaingia madarakani? Ni mambo mangapi kayabadili? Kuwa positive mkuu, hii ishu moja ya Mbowe isiwatoe ufahamu
 
Baadhi ya wafuasi wa Chadema wameipongeza hatua ya Rais Samia kuitaka mahakama itende haki katika mashauri yanayoletwa mahakamani.

Baadhi ya wafuasi wa Chadema wamepongeza hatua hiyo ya Rais Samia na kusema sasa wana imani kesi za wanachama wao ambazo nyingi ni za kubumba zitapatiwa ufumbuzi wa haraka.
Kamama kanafiki haka, kakihojiwa BBC kalisema MBOWE ni gaidi.
Kalimuhukumu MBOWE kabla jaji hajatoa hukumu
 
Baadhi ya wafuasi wa Chadema wameipongeza hatua ya Rais Samia kuitaka mahakama itende haki katika mashauri yanayoletwa mahakamani.

Baadhi ya wafuasi wa Chadema wamepongeza hatua hiyo ya Rais Samia na kusema sasa wana imani kesi za wanachama wao ambazo nyingi ni za kubumba zitapatiwa ufumbuzi wa haraka.
Hao wafuasi wa Chadema ulikutana nao kwenye ofisi au tawi la wapi? Unakaa na mtu kwenye kijiwe cha bia kisha unatuletea eti baadhi ya wafuasi ambao walikusanyika bila kukamatwa na polisi! Sema rafiki zako wamepongeza.
 
Kinachoangaliwa mahakamani ni pesa sio haki,mahakama hizi za bongo hakuna haki kama huna pesa ya kuhonga,haki yako inafinyangwa waziwazi bila aibu
 
Nimeanza kuhisi kauli za Samia hazina uzito, yeye atasema hivi wasaidizi wake watafanya vile, hana authority inayotakiwa kiongozi wa aina yake awe nayo, hii kauli yake nayo itapita tu, na polisi na mahakama zitaendelea kutumiwa na CCM kwa maslahi yake kama kawaida.
Kuambizana kupo.... Ingawa kusikilizana hakupo
 
Rais ana mamlaka ya kuamrisha mahakama kutenda au kutotenda haki?Angewakumbusha kufuata sheria!
Jaji Mkuu mbona huwa anataka upelelezi wa kesi uharakishwe? Hii ni mihimili inayotegemeana siyo ILIYOTENGANA!

Tanzania mihimili yote ya dola inafanya kazi kwa maslahi ya watu na nchi. Mahakama siyo ya Majaji na Mahakimu ni ya wananchi wanaohitaji haki, Serikali ni ya wananchi na Bunge ni la wananchi# Agizo la Rais akiwa ni Mkuu wa nchi ni sahihi na halali.
 
Hivi Mahakama zetu zinahitaji kuelekezwa kutenda Haki ? Kama ndivyo ,basi kuna wakati zinaelekezwa kutokutenda Haki !
 
Rais anaagiza mahakama itende haki badala ya mahakama kusimamia sheria kutenda haki,kwa hali hii uhuru wa mahakama uko wapi? siku nyingine Rais akiagiza mahakama nyonga huyu, funga huyu kifungo cha maisha mahakama itashindwa kutekereza maagizo ya Rais?.

Huu ni ubabe wa muhimili mmoja kwa muhimili mwingine. Katiba mpya ndio tiba.
 
Nadhan hatukuelewa pale mwendazake aliposema mhimili wake umejichimbia chini zaid
Rais anaagiza mahakama itende haki badala ya mahakama kusimamia sheria kutenda haki,kwa hali hii uhuru wa mahakama uko wapi? siku nyingine Rais akiagiza mahakama nyonga huyu, funga huyu kifungo cha maisha mahakama itashindwa kutekereza maagizo ya Rais?.

Huu ni ubabe wa muhimili mmoja kwa muhimili mwingine. Katiba mpya ndio tiba.
 
Amenawa mikono
... exactly! Siku zijazo akihojiwa atajitetea alikuwa mhimizaji na muumini mkubwa wa haki sio tu itendeke bali ionekane inatendeka! Halafu mashabiki wake na media wata-propagate hii maneno duniani kote wakimwimbia sifa kedekede.
 
Ana haki na mamlaka ya kuagiza haki itendeke asichoweza na ambacho ni kuingilia uhuru wa mahakama ni kuagiza kesi iamuliweje.

Mtazamo wangu, angeanza na law enforcers kwanza maana wao wanawajibika moja kwa moja kwa wananchi na Rais, na ndio chimbuko la ama mtu kuelekea kupata au kukosa haki...
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom