Rais Samia aagiza Mahakama itende Haki, baadhi ya wafuasi wa CHADEMA wampongeza

Chadema mbona mnakuwa vilaza hivi. Mnamuaminije Hangaya wakati alishamaliza kila kitu kuhusiana na Mbowe siku ya mazungumzo na BBC.
 
..inawezekana amesoma tu alichoandikiwa ktk hotuba.

..mimi nadhani hakumaanisha, na wala haamini hicho alichokisoma.

..kama mnabisha subirini muone kama mahakama zitaanza kutenda haki ktk nchi hii.
Kama nakumbuka vizuri, aliwahi kuviagiza vyombo vya dola vitende haki na viache kubambikia watu kesi. Nashukuru kuwa toka kauli hiyo hamna raia anayeonewa na vyombo vya dola na mambo ya kubambikiwa kesi yameisha kabisa nchini mwetu.

Amandla...
 
Mfumo unaotumika kuwapata hawa watafsiri sheria kama mahakimu na majaji ndio mbovu na ni chanzo kikubwa cha kukosekana kwa haki katika nchi hii.

Huo utaratibu ndio umepelekea leo hii tuna mahakimu na majaji wa kimkakati ambao serikali na chama chao vinawatumia katika kufanikisha malengo yao ya kisheria.

Kuna kipindi Lema alilazimika kukaa ndani kwa miezi minne baada ya hakimu kukataa kumpa dhamana kwa kutii agizo la rais Magufuli na vilevile Sugu alifungwa jela kwa amri ya Magufuli.

Kama hatuwezi kupata katiba mpya itakayoweka wazi utaratibu mzuri wa kuwaajiri watumishi wa mahakama na kutoa uhuru wa mahakama kufanya kazi bila kuingiliwa na rais, usalama wa taifa, polisi au ccm basi tutakuwa tunafanya usanii tu kama ilivyo zoeleka.
 
Ndugu yangu mahakama iko chini ya Rais, yeye ndiye uteua na kuapisha majaji, mahakama ikitoa hukumu leo, kesho na yeye anaweza toa hukumu ya kusamehe na hivyo kutengua maamuzi ya mahakama.

tusiitafsiri dhana ya mihimili mitatu kichwachwa, let us be realistic.
Kwanza mihimili mingine inautegemea mhimili wa serikali kuwezeshwa na watendaji wake wanateuliwa na kuapishwa na mhimili wa serikali.

Sasa huo uhuru wa kufanya maamuzi utatoka wapi.
 
Kuna mahala pa kufanyia marekebisho kuhusu ucheleweshaji wa kesi sio mahakama pekee hata ofsi ya DPP inahusika kwa sehemu kubwa,ofisi ya DCI inahusika Tena kwa sehemu kubwa,hivyo basi Kama maeneo haya yakifanyiwa marekebisho basi hakuna kesi itakaa mahakamani.
 
Baadhi ya wafuasi wa Chadema wameipongeza hatua ya Rais Samia kuitaka mahakama itende haki katika mashauri yanayoletwa mahakamani.

Baadhi ya wafuasi wa Chadema wamepongeza hatua hiyo ya Rais Samia na kusema sasa wana imani kesi za wanachama wao ambazo nyingi ni za kubumba zitapatiwa ufumbuzi wa haraka.

Maneno matupu lini yaliwahi kuvunja mfupa?

Kwani katiba, sheria, PGO nazo zinasema je?

Kwamba tutegemee utashi wa nafsi za watu?
 
Baadhi ya wafuasi wa Chadema wameipongeza hatua ya Rais Samia kuitaka mahakama itende haki katika mashauri yanayoletwa mahakamani.

Baadhi ya wafuasi wa Chadema wamepongeza hatua hiyo ya Rais Samia na kusema sasa wana imani kesi za wanachama wao ambazo nyingi ni za kubumba zitapatiwa ufumbuzi wa haraka.
Kama aliwahi kutoa magizo walio wekwa mahabusu kwa kesi za kuzushiwa waachiwe lakini bado wako mahabusu, una tegemea mahakama ita msikiliza??
 
Gaidi akifungwa msijekulialia hapa haki haijatendeka. Mama hahusiki.
 
Jaji Mkuu mbona huwa anataka upelelezi wa kesi uharakishwe? Hii ni mihimili inayotegemeana siyo ILIYOTENGANA!

Tanzania mihimili yote ya dola inafanya kazi kwa maslahi ya watu na nchi. Mahakama siyo ya Majaji na Mahakimu ni ya wananchi wanaohitaji haki, Serikali ni ya wananchi na Bunge ni la wananchi# Agizo la Rais akiwa ni Mkuu wa nchi ni sahihi na halali.
Hapana,sidhani kama ni sahihi!Kama Rais anaweza amrisha mahakama/bunge nadhani kuna tatizo!
 
Rais hajaamrisha mahakama. Amezungumzia umuhimu wa haki. Rais hajasema mahakama iamue kesi fulani hivi! Ni sawa na Spika au Jaji Mkuu wanapoweza kuzungumzia umuhimu wa Serikali kusimamia Polisi kuharakisha upelelezi unakwenda kwa wakati.

Ni kwa sababu katika suala la uendeshaji wa dola mihimili yetu inategemeana. Halafu kumbuka Rais ni Mkuu wa nchi.


Hapana,sidhani kama ni sahihi!Kama Rais anaweza amrisha mahakama/bunge nadhani kuna tatizo!
 
Huyu Mama anajielewa?Mahakama ipo huru kwa mujibu wa katiba yetu.Rais hana haki wala wajibu wa kuiamrisha mahakama itende haki au isitende haki.
 
Nimeanza kuhisi kauli za Samia hazina uzito, yeye atasema hivi wasaidizi wake watafanya vile, hana authority inayotakiwa kiongozi wa aina yake awe nayo, hii kauli yake nayo itapita tu, na polisi na mahakama zitaendelea kutumiwa na CCM kwa maslahi yake kama kawaida.
Yeye mwenyewe hajui hata anaongea nini
 
Back
Top Bottom