Rais Ramaphosa akataa Rapa AKA kufanyiwa mazishi ya Kitaifa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
South-African-rapper-Kiernan-%E2%80%98AKA-Forbes-e1676098367286.jpg

Vyombo vya Habari vya #AfrikaKusini, vimeripoti kuwa Gavana wa Serikali ya #Gauteng, Panyaza Lesufi, alimwandikia Rais #Ramaphosa ombi la Msanii huyo kuzikwa kama Mtu mwenye mchango mkubwa kwa jamii na hivyo apewe heshima ya Kitaifa.

Gavana Panyaza hakuomba fedha za Serikali zitumike kwa ajili ya mazishi, bali Jeneza tu la Rapa huyo lifunikwe kwa Bendera ya Taifa pamoja na muda mchache wa Bendera kupepea nusu mlingoti kwa heshima ya rapa huyo.

Rapa #KiernanForbes 'AKA' aliuawa kwa kupigwa Risasi nje ya Mgahawa Februari 10, ikiwa ni muda mchache akijiandaa kusherehekea Siku yake ya Kuzaliwa pamoja na rafiki zake. #AKA atazikiwa Jumamosi Februari 17, 2023.

============

A request by a provincial government for state funeral to be given to a popular South African rapper murdered last week has been denied by the president, local media report.

Gauteng’s premier Panyaza Lesufi had written to President Cyril Ramaphosa requesting permission to give slain rapper Kiernan Forbes, popularly known as AKA, a state funeral.

On Thursday, Mr Lesufi said his request had been denied.

He said he had not requested for state funds for the funeral, but for the coffin to be draped with the national flag and flags to be flown at half-mast in honour of the rapper.

“We felt that the person of his international stature, person of his national stature, there must be some form of honour, and we want to clarify it is not a financial contribution,” he is quoted as saying.

The rapper will be buried on Saturday.

BBC
 
Safi kabisa, Ana mchango gani wa Taifa lao hadi bendera ipepee nusu mlingoti, Azikwe na Watu wake wa karibu yatosha.
International Arts wana mchango mkubwa kwa mataifa yao, kwa mfano, Muziki wa Congo umefika hapo ulipo leo sababu ya watu kama Franco ndio maana alipewa state funeral, wanamuziki wana mchango Mkubwa kwa Taifa kuliko wanasiasa wengi

Hapo Tanzania leo, Diamond ana mchango mkubwa kwa Taifa kuliko kina Nape na Mwigulu
 
Mada inamuhusu AKA, hayo mengine yametoka wapi?

Mpaka Rais anakataa ujue wameshachuja
 
International Arts wana mchango mkubwa kwa mataifa yao, kwa mfano, Muziki wa Congo umefika hapo ulipo leo sababu ya watu kama Franco ndio maana alipewa state funeral, wanamuziki wana mchango Mkubwa kwa Taifa kuliko wanasiasa wengi

Hapo Tanzania leo, Diamond ana mchango mkubwa kwa Taifa kuliko kina Nape na Mwigulu
Mzee umeingiza mpaka kina franco, diamond.. Hao wametofautiana saana.

Haya eleza mchango wa AKA
Hapo south kuna wasanii wanaopaswa kupata heshima hiyo.
 
Kwamba siku daimondo akirudisha namba apewe maziko ya kitaifa bendera nusu mlingoti kwa sababu aliimba "Paka mate joka liingie?”

Serious kabisa?
 
Matendo yako yata justify kupewa heshima hiyo sio umaarufu wako
 
Kwamba siku daimondo akirudisha namba apewe maziko ya kitaifa bendera nusu mlingoti kwa sababu aliimba "Paka mate joka liingie?”

Serious kabisa?
Sijasema hivo,mbona unanilisha maneno Mkuu😂 , nimetumia jina la Diamond kama mfano wa mchango wa msanii katika taifa lake

By the way, hata franco ana wimbo aliimba matusi na akapewa state funeral alipokufa
 
Mzee umeingiza mpaka kina franco, diamond.. Hao wametofautiana saana.

Haya eleza mchango wa AKA
Hapo south kuna wasanii wanaopaswa kupata heshima hiyo.
Ukisoma tena comment yangu sijamzungumzia AKA bali nimemzungumzia "Msanii" i wasn't specific, huyo AKA sijui wimbo wake hata mmoja ndio maana sijamzungumzia bali nimemzungumzia hasa franco ambaye alikufa

Na mwisho nimetafakari kwa kutumia mfano wa Diamond jinsi alivotoa mchango kwenye Taifa lenu kuliko baadhi ya wanasiasa, bila Diamond kina Mbosso ,Harmonize ,Rayvanny wasingekuwa hapo walipo ,Wasafi imeajiri vijana wengi kuliko Wanasiasa

And for the record nikwambie tofauti pekee iliyopo kati ya Franco na Diamond ni kwamba Diamond ana nyimbo nyingi za matusi,Franco ana mbili, lakini hawa wote ni wafanyabiashara wakubwa na matajiri kupitia music na wametangaza mataifa yao na kutoa ajira

Kuhusu AKA sitoi maoni yangu,mimi nazungumzia wasanii in general so sijui kama ni sahihi huyu jamaa kupewa state funeral sababu simjui
 
International Arts wana mchango mkubwa kwa mataifa yao, kwa mfano, Muziki wa Congo umefika hapo ulipo leo sababu ya watu kama Franco ndio maana alipewa state funeral, wanamuziki wana mchango Mkubwa kwa Taifa kuliko wanasiasa wengi

Hapo Tanzania leo, Diamond ana mchango mkubwa kwa Taifa kuliko kina Nape na Mwigulu
South Africa sio Taifa la kisanaa , kuna mataifa Sanaa ni nembo ya Taifa Lao , hlo ni Taifa la kisiasa Zaid , mfano hyo Congo ni Sawa , Argentina au Brazil Kwa mpira ni Sawa , Ila South Africa Kwa kuimba tuu , big noo
 
Mkuu ila wataalamu wa kupika beat mfano za amapiano na beat nyingine nyingi nyingi tunaiga kwao
 
Ukisoma tena comment yangu sijamzungumzia AKA bali nimemzungumzia "Msanii" i wasn't specific, huyo AKA sijui wimbo wake hata mmoja ndio maana sijamzungumzia bali nimemzungumzia hasa franco ambaye alikufa

Na mwisho nimetafakari kwa kutumia mfano wa Diamond jinsi alivotoa mchango kwenye Taifa lenu kuliko baadhi ya wanasiasa, bila Diamond kina Mbosso ,Harmonize ,Rayvanny wasingekuwa hapo walipo ,Wasafi imeajiri vijana wengi kuliko Wanasiasa

And for the record nikwambie tofauti pekee iliyopo kati ya Franco na Diamond ni kwamba Diamond ana nyimbo nyingi za matusi,Franco ana mbili, lakini hawa wote ni wafanyabiashara wakubwa na matajiri kupitia music na wametangaza mataifa yao na kutoa ajira

Kuhusu AKA sitoi maoni yangu,mimi nazungumzia wasanii in general so sijui kama ni sahihi huyu jamaa kupewa state funeral sababu simjui
Uko sahihi kwa yote. Lakini kuna eneo aidha sijakuelewa vyema au hujaeleweka vyema.

State Funeral hupewa mtu ambaye mchango wake wa kitaifa umeleta Mapinduzi na mchango wa Kipekee ambao hata watu wengine kwenye sekta hiyo wanaafiki; na kazi hiyo imekuwa na mchango wa kutambulika kwa jamii husika.

Madilu, Pepe Kalle hao walikuwa ni wasanii wakubwa, lakini Hawakufikia Franco. Franco aliubadili muziki, kuukuza na kuutambulisha nje kwa miaka karibu 30 na hatimaye kuitwa mfalme wa Rhumba. Lakini, sifa nyingine ni ushawishi wa mtu huyo kwa jamii. Baada ya kuwa ametambulika sana kwa kazi yake na heshima aliyoijenga, basi jamii inamsikiliza na kuweza kufuata ayasemayo—USHAWISHI.

Sasa mtu kama Franco alikuwa na uwezo wa kusimama na kusema mchagueni fulani na watu wakachagua. Pia kuna wanamuziki kama Umm Khulthum. huyu wamisri walikuwa wakimtazama kama alama ya taifa lao. Kuna wakati Rais Gamal El Nasser alikuwa hawezi ongea watu wakamuelewa hadi huyu mama azungumze. Alipofariki karibu Robo ya watu wa Misri waliingia barabarani kwenye msururu wa mazishi yake, alipewa hadhi ya kuwa Balozi (Diplomatic Status). Wanamuziki/wasanii wa kaliba hii ndio hupewa hadhi ya mazishi ya kitaifa.

Sasa wampime AKA kama anaweza kufika hadhi hiyo, au ni watu kama kina Yvyone Chaka Chaka kwa Afrika kusini ndio wanaweza kufikiliwa. Je, Diamond ana hadhi hiyo. Diamond amekuta Bongo Flava imeshaanza wala hakuna mapinduzi aliyoyafanya kwenye muziki zaidi ya kujisimamia yeye binafsi na kuwa model ya namna ya kuendesha biashara ya muziki wa bongo flava (kwa hili anastahili heshima).

Lakini hapa inabidi tufanye tafakari. Waasisi wa bongo flava ni watu wanaopaswa kuwa na hadhi ya kutambuliwa kutokana na kitu walichokileta kwenye jamii—watambulike Kiserikali na kitaifa—changamoto hapa ni moja, nani anasifa ya kuwa Icon wa Bongo flava.
 
Wewe ndio unastahili kizikwa kitaifa Kwasababu hujaimba "Paka mate joka liingie"
Nope!

Mimi hata nikiwa na ndugu star siwezi kulazimisha azikwe kitaifa coz siioni faida yoyote au hasara kwamba azikwe na serikali au jamii ndugu tukiwepo.
 
International Arts wana mchango mkubwa kwa mataifa yao, kwa mfano, Muziki wa Congo umefika hapo ulipo leo sababu ya watu kama Franco ndio maana alipewa state funeral, wanamuziki wana mchango Mkubwa kwa Taifa kuliko wanasiasa wengi

Hapo Tanzania leo, Diamond ana mchango mkubwa kwa Taifa kuliko kina Nape na Mwigulu
Huyu sio Luke Dube ama Yvonne Chakachaka
 
Back
Top Bottom