Rais Paul Kagame wa Rwanda, akagua gwaride la Jeshi la Tanzania (JWTZ)

Mkuu kuna tofauti kubwa sana.
Ukiangalia ya Kagame na JWTZ utagundua kabisa kuwa PK ameonekana ni mtu mwenye Mamlaka kabisa,askari na wote walio kando yake wamekaa kikakamavu kabisa Mfano Membe,hapo unaweza kudhan kuwa Membe ni Mmoja wa ma PSU guard wa PK.
Hiyo screenshot uliyoweka kwanza hao wala sio wanajeshi
Duh! Mi naona sasa unaleta ubishi usio na maana au unaleta ubishi wenye maslahi fulani! Sasa suala la PK kuonekana kuwa na mamlaka kamili kuna uhusiano gani kwenye mada hii? By the way, hivi ufahamu kwamba PK ni mwanajeshi kwa maana ya uanajeshi as compared to JK? Ina maana ulifahamu hili ndugu yangu? Hivi unatarajia muonekano wa JK mbele ya jeshi utakuwa sawa na na wa PK wakati JK ni raia na PK ni mwanajeshi kwa maana ya uanajeshi wenyewe?

Kisha unadai hao kwenye screenshot sio wanajeshi... ni nani basi? Ni waalimu, madaktari, wanasheria au? Naona ulichofanya hapo ni sawa na mtu aliyezoea kuona JWTZ wakiwa na kombati za mabaka mabaka halafu abishe hao wenye RED uniforms sio JWTZ... exactly ndicho unachomaanisha! By the way, ulidai hapakuwa na minister yeyote... je, na huyo mama ni nani kama sio Membe wa Rwanda?

Aidha, hebu angalia JK alipoenda Rwanda mwaka 2012 kisha niambie utofauti uliopo kati ya hili jeshi la mwaka 2012 ambalo JK "alilikagua" na hilo linaloonekana kwenye screenshot!
JK 2012.JPG

Aidha, linganisha na hili la wakati ya safari ya Rais Kenyatta:
Kenyatta.jpg

Kisha linganisha na hii video screenshot:
PK.jpg

Tofauti ninayoiona ni positioning. Wakati Wanajeshi wa Rwanda wanakaa mbali sana na red carpet, hawa wa Tanzania wanakuwa karibu mno red carpet. Hii ya Rwanda kiusalamu nadhani ni mzuri zaidi as compared to hii ya Tanzania ambao ni very simple kurukia mtu na kumpiga kabali at a surprise attack!
 
Hivi JK hana jema hata moja jamani? Kwani ni lazima rais apokelewe na rais mwenzake hata kama mwenyeji wake anadharura? Mbona JK alipokewa na gavana kule kenya hamkuandika Mpeni haki yake Rais wetu jamani

Mkuu hapo kwenye red nenda kwenye jukwaa la Kimataifa utakutana na thread yenye malalamiko kwa mapokezi aliyopewa Jk kule Kenya...

Ungekuwa makini kidogo ktk hiyo post uliyoni-quote ungegundua kwamba hatulalamikii Jk kutojitokeza kumpokea Kagame, Tunacholalamika sisi hapa ni mapokezi ya hali ya juu aliyopokewa Kagame Pamoja na Madharau yote kwa Rais wetu na nchi kwa ujumla. Wengi tulipenda kwa kiwango kile alichotudharau naye ANGEDHARAULIWA vilevile......!!
u
Naam, akupigaye ngumi ya jicho nawe mpige ya sikio... Akikuuliza unaonaje nawe muulize unajisikiaje...!!!! (Hiki ndicho wengi tulichokua tukiramani afanyiwe huyo mkondefu) Hakuna chuki yoyote kwa Kikwete hapo.

BACK TANGANYIKA
 
Mkuu NasDaz, heshima mbele...!!!

Awali wakati na-quote post yako sikuona kama kuna Attachment ya video hata baada ya kugundua kwamba kuna video kuifungua ikagoma..!!! So mpaka sasa sijathibitisha kwamba hiyo Video inasemaje au kufanyaje.

Hata hivyo wengi wetu humu ndani tunachukizwa sana ha huyu Kagame kutokana na Kumdharau Rais wetu kipindi kile alipopewa ushauri wa kukutana na wabaya wake.. (Kama utakuwa ukikumbuka ile speech alitoitoa mbele ya wanajeshi wake utaungana na mimi kumchukua huyu bwana) Kiukweli kwa speech ile hakumtusi tu Rais wetu, bali alilitusi Taifa kwa ujumla. Hivyo kiwango kile alichotudharau sisi wengine tungependa ADHARAULIWE vilevile... Kwahiyo yote tunayoyasema hapa ndani ni kutokana na vile tulivyojisikia pale tulipodharauliwa..!!

Hebu angalia Watanzania tulivyoungana kupinga namna Wakenya kupitia Rais wao walipoamua kupiga marufuku Magari ya kubeba watalii kuingia JOMO KENYATA, na angalia namna tukivoungana na Serikali yetu kuunga mkono punguzo la safari za Ndege za Kenya hapa kwetu... Unadhani ni kwanini??

Receive my Apology please.

BACK TANGANYIKA
Mkuu respect wa boda,
Sina hakika kama umeshawahi kukutana na mimi kwenye mijadala inayohusu Rwanda na Tanzania! Binafsi, mimi linapokuja suala la Tanzania na foreign country and in fact, even Tanzanians v/s foreign nationals nakuwaga radical sana... huyo PK humu nimesham-despise sana lakini inachoongea hapa siangalia historia inatukumbusha nini bali naongelea issue ilivyotokea! Kwa upande mwingine, mtu ukitaka kuonesha u-stupid wake usifanye vile vile kama alivyofanya yeye!!!

Ukija kwenye hiyo video, it's very unfortunate kwamba imeshindwa kufunguka lakini ingefunguka, ungeona amepokewa na Waziri wa mambo ya Nchi za Nje na pia kuna gwaride ambalo ndugu yangu Bramo hatimae ameliona lakini hivi sasa anadai sio wanajeshi!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwani kazi ya bodyguard ni zipi, kwa taarifa yako Bodyguards wote wanapitia mafunzo ya Kijeshi, kuvaa kwao kiraia aimaanishi ni raia. Kitu kingine PK anakagua gwaride la jeshi la Kigeni, we unategemea walizi wa PK wataji-conduct vipi wakiwa ugenini? in other words kati ya MEMBE na PK ni walinzi wapi wapaswa kuwa makini/macho zaidi?

Mkuu Kwan nani kazungumzia bodyguard hapa ?
 
Duh! Mi naona sasa unaleta ubishi usio na maana au unaleta ubishi wenye maslahi fulani! Sasa suala la PK kuonekana kuwa na mamlaka kamili kuna uhusiano gani kwenye mada hii? By the way, hivi ufahamu kwamba PK ni mwanajeshi kwa maana ya uanajeshi as compared to JK? Ina maana ulifahamu hili ndugu yangu? Hivi unatarajia muonekano wa JK mbele ya jeshi utakuwa sawa na na wa PK wakati JK ni raia na PK ni mwanajeshi kwa maana ya uanajeshi wenyewe?

Kisha unadai hao kwenye screenshot sio wanajeshi... ni nani basi? Ni waalimu, madaktari, wanasheria au? Naona ulichofanya hapo ni sawa na mtu aliyezoea kuona JWTZ wakiwa na kombati za mabaka mabaka halafu abishe hao wenye RED uniforms sio JWTZ... exactly ndicho unachomaanisha! By the way, ulidai hapakuwa na minister yeyote... je, na huyo mama ni nani kama sio Membe wa Rwanda?

Aidha, hebu angalia JK alipoenda Rwanda mwaka 2012 kisha niambie utofauti uliopo kati ya hili jeshi la mwaka 2012 ambalo JK "alilikagua" na hilo linaloonekana kwenye screenshot!
View attachment 238198

Aidha, linganisha na hili la wakati ya safari ya Rais Kenyatta:
View attachment 238206

Kisha linganisha na hii video screenshot:
View attachment 238211

Tofauti ninayoiona ni positioning. Wakati Wanajeshi wa Rwanda wanakaa mbali sana na red carpet, hawa wa Tanzania wanakuwa karibu mno red carpet. Hii ya Rwanda kiusalamu nadhani ni mzuri zaidi as compared to hii ya Tanzania ambao ni very simple kurukia mtu na kumpiga kabali at a surprise attack!

Humble apology Mkuu NasDaz
Nilikuwa nataka ufunguke tu.
Uwe na siju njema,pia kumbuka kuwa hata JK wetu ni Mwanajeshi,Kanali
 
Last edited by a moderator:
Humble apology Mkuu NasDaz
Nilikuwa nataka ufunguke tu.
Uwe na siju njema,pia kumbuka kuwa hata JK wetu ni Mwanajeshi,Kanali
Vitu vidogo tu hivi mkuu wangu... afadhali kama ninge-panic wakati mie nimechukulia poa tu sana sana nilitaka kukuuliza ikiwa ndugu yangu wewe ni Mlugulu!!!! Na kwa upande mwingine, ukanali wa JK huwezi kuulinganisha na PK manake ingawaje inasemekana eti JK alipigana vita vya Uganda, mie wala siamini lakini PK kila mtu anafahamu kwamba ni mpiganaji na hata na hata anapotembea unamuona kabisa mkakamavu! Na ukimwangalia Kenyatta, yeye ndo anatembea kiuboya zaidi afadhali ya JK mara elfu 1000!!!
 
11072720_706425619468415_6496588163067173375_n.jpg

Rais wa Rwanda Mhe.Paul Kagame akikagua gwaride la heshima.alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Mhe.Rais Kagame yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Ukanda wa Kati kuhusu Uwekezaji na Viwanda unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Jamani mmenote kuwa askari mmoja katika hili gwaride amekuwa nanga?
Singe yake haijakunjuliwa!!!!!
Mkuu wa majeshi msamehe bure.
 
..hapa protokali imefuatwa.

..mimi nampongeza JK kwa jinsi alivyo-handle mgogoro wa DRC na Rwanda.

..he has achieved a lot. kwanza amemaliza kiburi na unyama wa Rwanda kule DRC.

..pili, Tz imeanza ku-train askari wa DRC, ili waweze kuilinda nchi yao wao wenyewe. wakati wa utawala wa Mkapa tulikuwa tuna-host waasi wa DRC kama Prof.Wamba Dia Wamba, na kusafirisha silaha nzito za Uganda huku tukijua wameivamia Congo.

..tatu, amemaliza sintofahamu iliokuwepo kati yake na Kagame. Sasa Rwanda imerejea tena na kuwa fully committed kutumia reli na bandari za Tanzania. Leo Raisi Kagame amezindua treni ya mizigo ya Rwanda toka bandari ya Dsm.

..nne, Coalition of the Willing au CoW, imezikwa rasmi leo Dsm kwa ziara hii ya Raisi Kagame ambaye amepokelewa kwa heshima za kijeshi hapa Dsm.

..kwa hiyo katika hili kwa kweli nampa Raisi Jakaya Kikwete alama ya 100% au A++. Natamka kwamba JK amedhihirisha kwamba yeye ni Daktari, Professor, nguli, kinara, na bingwa wa siasa na mashirikiano ya kimataifa katika Afrika.

cc Ritz, Ben Saanane, Bukyanagandi, JustDoItNow, Talkandtalk, Nguruvi3, NasDaz, MwanaDiwani
Duh! Mkuu wangu JokaKuu unajua kutoa majibu ya kukomoana, wallah tena! Au ushaahidiwa ukuu wa wilaya ndugu yangu? Au ulisikia tetesi za JK kuteua wabunge wawili kwahiyo ukaamua kutengeneza mazingira.... hahahaaaaa!!

Ila nikija kwenye suala la Mkapa na kuhifadhi wapinzani wa DRC, hili sitakikulizungumzia lakini sehemu ambayo Mkapa nilimkubali sana ni pale wahuni walipoingia DRC! Endapo ningekuwa Rais wa nchi kipindi kile, sidhani kama ningevumilia kutoipeleka JWTZ nchini DRC kupambana na wahuni waliokuwa wanaongozwa na Rwanda na Uganda... am certain, ningepeleka jeshi uamuzi ambao sidhani kama ungekuwa wa busara tofauti na busara ambayo aliionesha Mkapa kwa kutopeleka jeshi DRC!
 
Last edited by a moderator:
Hivi bongo zetu zinakuwa zimefunikwa na ukawa........ Kagame ni rais?? Hivi rais gani anapokelewa duniani bila gwaride?.miaka yote hii naona viongozi wakubwa wa nchi wanapokelewa kwa gwaride.. Kwa pk kupokelewa hivyo kitu cha kawaida sana ... Ben wakati mwingine ubongo wako usiufinye
 
Ishara ya kumuomba radhi kidiplomasia na kijeshi....!

Hivi bongo zetu zinakuwa zimefunikwa na ukawa........ Kagame ni rais?? Hivi rais gani anapokelewa duniani bila gwaride?.miaka yote hii naona viongozi wakubwa wa nchi wanapokelewa kwa gwaride.. Kwa pk kupokelewa hivyo kitu cha kawaida sana ... Ben wakati mwingine ubongo wako usiufinye
 
ili iweje kwani wewe ni nani mpaka nikuthibitishie

basi sawa tufanye kagame aliposema hayo maneno ulikuwa naye. Hakuna haja ya wewe kuthibitisha madai mazito kama hayo kwa kuwa wewe ni mtu wake wa karibu sana.
 
Vijana wa dotcom waliozaliwa juzi hawajui maana ya vita. Wanavisikia tuu kwenye bomba.

They have never experienced living in a war-torn country zaidi ya kuona tuu kwenye TV.

Wanajifanya tuu hapa wakati juzi panya road waliwakimbiza kwenye stuli za baa mpka wote ukawa mweupeee.

Na kwa uchumi huu ambao unaumwa uko ICU, nani atalipia vita kama tutaanzisha vita leo? Kweli wanaopenda vita hawajui maana ya vita nini.
 
Bado tunawavalisha askari wetu OVERZIZED UNIFORMS na VIATU VYA MITUMBA

Hivi hatuna bunduki zingien zaidi ya hizo?

Kelele wee.... Pesa wanakusanyiwa kina Chenge, Gurumo, Tibaijuka n.k...... serikali hawezi kupoteza pesa kununua nguo mpya ilhali kuna mitumba ya kijeshi!!!
 
Back
Top Bottom