Rais Paul Kagame wa Rwanda, akagua gwaride la Jeshi la Tanzania (JWTZ)

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
11072720_706425619468415_6496588163067173375_n.jpg

Rais wa Rwanda Mhe.Paul Kagame akikagua gwaride la heshima.alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Mhe.Rais Kagame yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Ukanda wa Kati kuhusu Uwekezaji na Viwanda unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
 
Nimeipenda hii, Kagame kapokelewa na BERNARD MEMBE!!! bwahahahahahahahha! Cheki membe anavyotabasamu halafu kagame sura ilivyomshuka.

cc: Ngongo JokaKuu JustDoItNow.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
Ishara ya kumuomba radhi kidiplomasia na kijeshi....!

Nilidhani ni peke yangu niliyefikiri kama hivi, kumbe tuko wengi...

Kwa kumbukumbu zangu nakumbuka Kikwete alipokwenda kwenye Mkutano wa EaC pale Rwanda hakupokelewa kwa gwaride wala kutumiwa wazir wa mambo ya nje achia mbali Kagame kwenda kumpokea.!!! Sasa imekuwaje yeye kumpokea kwa Gwaride na kwa mapokezi ambayo kidipromasia ni halali yake (Kupokelewa na waziri wa mambo ya nje kama Rais hayupo ama katingwa)

Nadhani Kikwete ni kama anaomba radhi ama kubembeleza kwa namna fulani hivi... Kumbuka Baba yako akigundua kakuadhibu kwa bahati mbaya (hukukosa) kamwe hawezi kukuomba radhi, Bali kesho waweza kuta anakuja na Kiatu suruali ama chochote kile kama zawadi yako.. Naam kwa wenye akili kubwa watajua mzee anaomba radhi kwa mlango wa nyuma.

Hiki ndicho kinachofanywa na Kikwete???

BACK TANGANYIKA
 
Kukagua magwaride ni utaratibu wetu wa kawaida tu. Kama wao hawana huo utamaduni, sisi tunao, Tanzania hatuwezi kujishusha na kufanya petty competitions na wap.uu.zi! Tutampa heshima zake zote kama rais wa nchi ya Rwanda.
 
Back
Top Bottom