Rais, Nakuomba tafadhali 2020 mchague Aggrey Mwanri kuwa Waziri Mkuu

Mpekuzi Tanzania

Senior Member
Mar 11, 2018
186
500
Uwaziri Mkuu ni Utendaji, hauitaji comedian. Kwa awamu ya tano ukiacha Majaliwa wengine wanaoweza kidogo ni wawili tuu. Simbachawene na Luhaga Mpina
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,777
2,000
nani kakudanganya, iwe jua iwe mvua, magufuli atapita tu, mtake msitake, hakuna upinzani wa kumsimamisha
Hivi unaamini kabisa ufipä wanatoa rais 2020? Hatari sana hizi ndoto..
Nani kasema habari za ufipa hapa? Mmesahau kuwa vita kuu ya kwanza ya CCM ni palepale Lumumba (Membe & co) kisha inakuja vita kuu ya Pili bila majenerali wa frontline (DED's) hapo ni kichapo tuu hadi Lukaya.
 

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,771
2,000
Nani kasema habari za ufipa hapa? Mmesahau kuwa vita kuu ya kwanza ya CCM ni palepale Lumumba (Membe & co) kisha inakuja vita kuu ya Pili bila majenerali wa frontline (DED's) hapo ni kichapo tuu hadi Lukaya.
Kwa akili zako Membe anaweza mziki wa Magu?
 

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
53,291
2,000
Tule mzee anapima hadi mbao.

Ila uwaziri hauwezi kwa sababu anasifia sana kupitiliza
 

GAS STATE

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
1,770
2,000
Mtoa uzi hivi unakijuwa vizuri cheo cha uwaziri mkuu, kifupi ni mtendaji mkuu wa serikali uraiani na bungeni. Mwanry ana uzima gani wa kumpa nafasi hiyo kapona lini kichwa chake. waziri mkuu ni mtu thinking na reasoanable sio soma hiyooooo, hovyo tupu usitujazie vichaa barabari ebo gari ikashindwa kutembea
 

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,562
2,000
Shkamoo Mh Rais, hongera sana kwa kufanikisha mkutano wa SADC, hongera kwa jukumu la uenyekiti, hongera sana kwa kubadilisha Tanzania. Nianze kwa kukiri kwamba 2015 sikukuchagua, nilimchangua Mh Lowassa, nilifikiri kwamba CCM haiwezi tena kuwa safi, nilifikiri ukiiingia utakuwa fisadi na utazidi kuididimiza nchi, hongera kwakuwa umenionesha kuwa nilikosea kufikiri hivyo, panapo majaliwa 2020 kwa mara yakwanza kura yangu ya Diwani, Mbunge na Rais ni CCM.

Lengo hasa la kuandika uzi huu ni kuwasilisha ombi langu la dhati kwako, naomba sana ikikupendeza 2020 umshauri ndugu Aggrey Mwanri agombee ubunge jimbo la Siha (najua atashinda kwa kishindo) na ndugu Mollel wa Siha apangiwe kazi nyingine au awe mbunge wa kuteuliwa, kisha baada ya ushindi wako wa kishindo kwa asilimia zaidi ya tisini (90%+) itakapofika wakati wa kumteua waziri mkuu nakuomba sana umteue ndugu Aggrey Mwanry

Sina maana kuwa ndugu Majaliwa hafai, la hasha, nadhani ndugu Mwanry atasaidia sana kukimbiza mchakamchaka wa maendeleo....

Najaribu kuwaza siku akitembelea mradi wa ujenzi wa reli na kukuta mkandarasi anasuasua, nawaza siku akitembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme, nawaza atakavyokuwa anawasimamia wakandarasi wa miradi mbalimbali, nawaza jinsi mtakavyo shirikiana kuikimbiza tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati, nawaza jinsi ma Rais wa nchi nyingi za Afrika watakavyo miminika Tanzania kujifunza.

Nawaza jinsi mafisadi watakavyopata tabu, nawaza jinsi watu watakavyo furika na kuangua vilio mtakapokuwa mnatuaga 2025, yani ni raha sana na naamini kipindi hicho watu kama Mh Sugu, Mh Lema, Mh Mbowe, Mh Mdee watakuwa makada wa wakutupwa wa CCM. Tafadhali tunaomba utufanyie hilo mkuu wetu wa nchi.

Mwisho niwaombe Moderator na Maxence Melo msifute uzi huu tafadhali, haya ni maoni yangu, naamini hakuna sheria ya nchi niliyovunja kuweka uzi huu, naamini sijavunja sheria za JF pia, naamini uzi ukifutwa mtakuwa mmenionea sana, ikiwapendeza mnaweza kuuvuta juu kwa maslahi ya taifa letu. Mungu awabariki sana

#VivaTanzania
#vivaMagufuli
#HapaKaziTu
#TanzaniaYaViwanda
[/QUOTE
Ili achaguliwe Waziri Mkuu inabidi ashinde ubunge. Kwa kuwa alishindwa ubunge katika uchaguzi wa mwaka 2015, una uhakika gani kwamba mwakani atashinda? Nafasi yake kushinda ilikuwa kubwa mwaka 2015 kuliko itakavyokuwa mwaka 2020.
 

Kifuna

JF-Expert Member
Aug 7, 2008
434
225
Mwisho niwaombe @Moderator na @Maxence Melo msifute uzi huu tafadhali, haya ni maoni yangu, naamini hakuna sheria ya nchi niliyovunja kuweka uzi huu, naamini sijavunja sheria za JF pia, naamini uzi ukifutwa mtakuwa mmenionea sana, ikiwapendeza mnaweza kuuvuta juu kwa maslahi ya taifa letu. Mungu awabariki sana
Nani kakwambia hujafanya kosa? subiri wanasheria waje utaona kosa liko wapi!!
 

Mkondo wa Nungwi

JF-Expert Member
Feb 16, 2019
213
250
Viongozi wakitumia kauli kali wananchi watumie nini? Viongozi wakitumia nguvu wananchi watumie nini?

Katiba ndio muafaka wa kutengeneza viongozi bora na wananchi watakaopata uelewa na sio mikwara.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom