Ndio tumejaaliwa kuburuzwa, kama hamjaelewa ni lipi cha kueleweshwa?
Nimeuliza Raisi wa nchi kumpokea mcheza mpira kisa tu anakuja na ahadi kedekede, halafu ni juzi tu Rais huyo huyo amelalamika kwenye vyombo vya habari kuwa, yeye awe ndio mtu wa mwisho kutatua au kushughulika na jambo, kama yeye atakuwa wa mwanzo haina haja ya kuwa na Mawaziri wala wasaidizi.
Kwa alivyofanya amechukua kazi ya Waziri husika anaeshughulikia Michezo na kujitwisha yeye.
Tuchukulie Mchezaji wa Real Madridi anakuja TZB, Rais Samia awe kiguu na njia kuzungumza na mchezaji huyo kisa anakuja au anataka kuekeza. Inaelekea? Raisi wa nchi voo! Lakini sishangai ndivyo CCM inavyotupeleka ujingani.