Rais Mwinyi umetudhalilisha Wazanzibari. Waziri wa Michezo angetosha mazungumzo na Mamadou Sakho

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,921
3,801
Nimeona aibu sana na niliondoka kimya kimya huku nikisononeka inakuwaje Rais wa Nchi anajidhalilisha kwa mcheza mpira? Au ndio ukisikia itifaki imezingatiwa ndio huku?

Tena kwa red carpet kesho na kesho kutwa mchezaji anakunya mbovu inakuwaje hapo? Au kuna mtonyo wa 10%

Kusema kweli ni aibu ya mwaka hata kama angekuwa trilioneya bado Rais wa nchi asingejidhalilisha kiasi kile, inakuwaje yaani sijaelewa kabisa kabisa, wazee walisema akili ni nywele tatizo la sisi wenye vipara ni mtihani.

Wadau wa protokoli hili jambo mnalionaje?

Sakho.jpg
 
Ndio tumejaaliwa kuburuzwa, kama hamjaelewa ni lipi cha kueleweshwa?

Nimeuliza Raisi wa nchi kumpokea mcheza mpira kisa tu anakuja na ahadi kedekede, halafu ni juzi tu Rais huyo huyo amelalamika kwenye vyombo vya habari kuwa, yeye awe ndio mtu wa mwisho kutatua au kushughulika na jambo, kama yeye atakuwa wa mwanzo haina haja ya kuwa na Mawaziri wala wasaidizi.

Kwa alivyofanya amechukua kazi ya Waziri husika anaeshughulikia Michezo na kujitwisha yeye.

Tuchukulie Mchezaji wa Real Madridi anakuja TZB, Rais Samia awe kiguu na njia kuzungumza na mchezaji huyo kisa anakuja au anataka kuekeza. Inaelekea? Raisi wa nchi voo! Lakini sishangai ndivyo CCM inavyotupeleka ujingani.
 
Kwa Zanzibar ni aibu nasema kwa kinywa kipana ametudhalilisha Wazanzibar, inakuwaje mna tatizo la kutokujielewa na ndio maana CCM inawaburuza. Raisi? Aloo hivi hamna waziri? Mkitaka msitake ni kujidhalilisha.

lakini sio kosa lenu sababu ni umasikini ulioletwa na CCM.
 
Kudhalilisha vipi sasa, yaani star mkubwa duniani anatembelea kata ya Zanzibar unasema kadhalilisha, acha ujinga ww big names hao na uchumi wako mkubwa ulitaka Daimond ndio aje kutalii huko kwenu na kuleta mamilioni ya Dola? Majina makubwa siku zote bata zao ndio zinafanya maisha ya wengine yaende.
 
Kudhalilisha vipi sasa , yaani star mkubwa duniani anatembelea kata ya Zanzibar unasema kadhalilisha, acha ujinga ww big names hao na uchumi wako mkubwa ulitaka Daimond ndio aje kutalii huko kwenu na kuleta mamilioni ya Dola? Majina makubwa siku zote bata zao ndio zinafanya maisha ya wengine yaende

Hii mishamba imejipa kazi ya kukosoa kila kitu
 
Kudhalilisha vipi sasa , yaani star mkubwa duniani anatembelea kata ya Zanzibar unasema kadhalilisha, acha ujinga ww big names hao na uchumi wako mkubwa ulitaka Daimond ndio aje kutalii huko kwenu na kuleta mamilioni ya Dola? Majina makubwa siku zote bata zao ndio zinafanya maisha ya wengine yaende

Hii mishamba imejipa kazi ya kukosoa kila kitu
 
Rais yupo sawa kwa kigezo promo utalii, jamaa picha hizo atashare na wadau wake multiplier effect kuuza utalii.
 
Ndugu, Rais Dk. Mwinyi kafanya jambo kubwa labda liko juu ya uwezo wako wa kufikiri. Ameinadi Zanzibar kwa utalii lakini hata kuvutia Uwekezaji, ukiwemo wa michezo. Yule jamaa siyo kama mchezaji wa ndondo cup ujue..!😀😀😀
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom