Rais Mwinyi asema atabeba gharama zote za Uwanja wa Amaan katika Fainali ya Simba Vs RS Berkane

Rais Mwinyi asema atabeba gharama zote za Uwanja wa Amaan katika Fainali ya Simba Vs RS Berkane

Gharama ya uwanja mara nyingi huwa ni 15% ya Viingilio..

ZRA, ZFA na VAT ni palepale...

Kuhusu interest ya kisiasa nyuma ya support hii sidhani...

Mwinyi Jr ni muungwana sana.
Halafu isitoshe Wabara hawana haki ya kumpigia kura mgombea katika nafasi yeyote Zanzibar...

Badala yake wao, Wana haki ya kutuchagulia sisi...
Obviously watampigia Samia.
 
Inaonyesha jinsi Tanzania isivyokuwa nchi ya kufuat sheria. Rais anaweza kuamua lolote bila kupitia bunge, ambalo ndiyo chombo pekee cha kutunga sheria.
 
RAIS DKT. MWINYI ABEBA GHARAMA ZOTE UWANJA WA AMAAN COMPLEX MECHI YA SIMBA DHIDI YA RS BERKANE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa Zawadi Maalum kwa timu ya Simba Sports Club kwa kugharamia matumizi ya Uwanja wa New Amaan Complex bila gharama yoyote kwa ajili ya kucheza fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho la CAF, itakayofanyika siku ya Jumapili, tarehe 25 Mei 2025, saa 10 jioni.

Uamuzi huo wa Rais Dkt. Mwinyi unalenga kudhihirisha mapenzi yake ya dhati kwa michezo pamoja na kuhamasisha ushindi kwa timu ya Simba SC, katika mechi hii ya kihistoria dhidi ya RS Berkane kutoka Morocco. Hatua hiyo pia ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar za kuunga mkono maendeleo ya michezo na kuleta hadhi ya kimataifa.

Mbali na kuruhusu matumizi ya Uwanja huo bure, Rais Dkt. Mwinyi amechukua dhamana ya kugharamia maandalizi yote muhimu ya uwanja kwa mechi hiyo.

Aidha, fainali ya mechi hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya washabiki kutoka ndani na nje ya nchi.

Kwa kutambua uzito wa mechi hiyo kwa Taifa, Rais Dkt. Mwinyi ameahidi kuhudhuria fainali hiyo sambamba na Watanzania wote katika kuwaunga mkono Simba SC na kuhamasisha ushindi wa kihistoria.
Good move...

Pongezi kwa Rais wa Zanzibar na serikali yake.
 
Vipi,hela hiyo ataitoa kwenye akiba yake au akiba ya kadi za wananchi.
Utasikiq vilaza sasa.

"Safi sana,huyu ndo rais".
Yanasahu kuwa,ni kadi zao.
Na hawana dawa mahospitalini.
Nchi ya wajinga sana
 
Back
Top Bottom