Rais Mwinyi asema atabeba gharama zote za Uwanja wa Amaan katika Fainali ya Simba Vs RS Berkane

Rais Mwinyi asema atabeba gharama zote za Uwanja wa Amaan katika Fainali ya Simba Vs RS Berkane

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,177
Reaction score
7,472
Ikulu Zenji.jpg
RAIS DKT. MWINYI ABEBA GHARAMA ZOTE UWANJA WA AMAAN COMPLEX MECHI YA SIMBA DHIDI YA RS BERKANE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa Zawadi Maalum kwa timu ya Simba Sports Club kwa kugharamia matumizi ya Uwanja wa New Amaan Complex bila gharama yoyote kwa ajili ya kucheza fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho la CAF, itakayofanyika siku ya Jumapili, tarehe 25 Mei 2025, saa 10 jioni.

Uamuzi huo wa Rais Dkt. Mwinyi unalenga kudhihirisha mapenzi yake ya dhati kwa michezo pamoja na kuhamasisha ushindi kwa timu ya Simba SC, katika mechi hii ya kihistoria dhidi ya RS Berkane kutoka Morocco. Hatua hiyo pia ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar za kuunga mkono maendeleo ya michezo na kuleta hadhi ya kimataifa.

Mbali na kuruhusu matumizi ya Uwanja huo bure, Rais Dkt. Mwinyi amechukua dhamana ya kugharamia maandalizi yote muhimu ya uwanja kwa mechi hiyo.

Aidha, fainali ya mechi hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya washabiki kutoka ndani na nje ya nchi.

Kwa kutambua uzito wa mechi hiyo kwa Taifa, Rais Dkt. Mwinyi ameahidi kuhudhuria fainali hiyo sambamba na Watanzania wote katika kuwaunga mkono Simba SC na kuhamasisha ushindi wa kihistoria.
 
Tanzania ni kigeu geu kupita kiasi..........kumbuka kuna watu waliuza tiketi ...........hivi huwa inakuwaje maana ehh
Hao wameshalizwa tayari, Kuna watu wailipia ya mkapa, na wakalipa tena ya Amaani, sasa imetangzwa Bure. Hzo pesa zinarudije na haliyakua Simba itapatiwa pesa kama mauzo kutoka kwa Raisi.
 
Hapa milio lazima iwe mingi
 
Hao wameshalizwa tayari, Kuna watu wailipia ya mkapa, na wakalipa tena ya Amaani, sasa imetangzwa Bure. Hzo pesa zinarudije na haliyakua Simba itapatiwa pesa kama mauzo kutoka kwa Raisi.
Haijatangazwa bure bali zile gharama za matumizi ya uwanja ndio zitalipwa na Raisi. Kwa maana hiyo ela ilipatikana kutoka kwa mashabiki haitagusa kabisa kugharamia mambo ya uwanja
 
Matumizi ya uwanja bure/Mashabiki bure?

mbona kuna confusion.

hii bure kwa timu au mashabiki?au wote
 
Back
Top Bottom